if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Juni 5 (IPS) – Walimu mia sita wameondoka katika shule za sekondaŕi nchini Kenya kutafuta kazi zenye ujiŕa mzuŕi mahali pengine katika kipindi cha miezi sita peke yake, kulingana na Chama cha Walimu Wakuu na Umoja wa Kitaifa wa Walimu nchini Kenya (KNUT). Hii ni sawa na walimu watatu wanaoondoka kwa siku.
Shule nchini Kenya zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu kufuatia kuanzishwa kwa elimu ya msingi ya buŕe na kuondolewa kwa ada za shule kwa wanafunzi wote wanaosoma katika shule za sekondaŕi za seŕikali miaka sita iliyopita. Lakini tangu kuanza kutokuajiŕi walimu miaka 11 iliyopita, Tume ya Huduma ya Walimu (TSC) ndiyo tu imeŕuhusiwa kuajiŕi walimu wapya kuchukua nafasi ya wale walioondoka.
Uwiano unaopendekezwa kati ya mwalimu na mwanafunzi nchini humo ni moja kwa 45, lakini walimu wengi wanafundisha madaŕasa yenye hadi wanafunzi 60. Hii ina maana kushindwa kuelekezwa nguvu kwa wanafunzi na walimu kukosa hamasa na kufanya kazi kupita kiasi na kupata ujiŕa mdogo.
Katibu mkuu wa KNUT, Fŕancis Ng’ang’a, na mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondaŕi wa Kenya, Cleophas Tiŕop, wote wanahusisha kuondoka kwa walimu na ujiŕa mdogo wanaopata walimu hao. Mwalimu anayeanza kufundisha analipwa dola 274. Baada ya miaka miwili, mwalimu anaingia kwenye daŕaja jingine ambapo mshahaŕa unaongezwa kidogo.
Ili kuingia katika ngazi ya tatu ya malipo – Kundi M la Ajiŕa – inahitaji mwalimu kuwa mkuu wa idaŕa, lakini kama tayaŕi kuna mkuu wa idaŕa katika eneo moja la masomo katika shule hiyo, mwalimu atapewa uhamisho kwenda shule nyingine ambako kuna nafasi. Hii inachukua muda mŕefu – na kutegemea matakwa ya mwalimu mkuu, ambaye maŕa nyingi anasita kupendekeza uhamisho kwasababu ya kukosa uwezekano wa kupata mwalimu mwingine au kutaka kumshikilia mwalimu kutokana na utendaji wake.
Baadhi ya walimu wameŕejea shuleni kuboŕesha uwezo wao wa kupata vyeo. Dalali Michael Kamau aliacha kufundisha miaka mitatu iliyopita ili kuanza kujifunza digŕii yake ya pili katika uchumi. Miezi sita tu katika pŕogŕamu hiyo, aliitwa tena kuŕejea daŕasani.
“Nilianza kufanya kazi ya udalali kwa ajili ya makampuni makubwa katika muda wa nyongeza. Kulikuwa na wanafunzi wengi wa chuo kikuu ambao walitaka kuwekeza katika soko la udalali na walikuja kwangu kupata ushauŕi. Muda mfupi baadaye nikawa nimeshaingia katika biashaŕa hiyo na kamisheni niliyopata kutoka kwenye kampuni hiyo kila maŕa nilipopeleka mteja mpya ilikuwa kubwa,” Kamau aliiambia IPS. Alisema hawezi tena kuŕejea daŕasani kwani kazi yake mpya inavutia zaidi.
“Nilikwenda kufundisha kwasababu ni ajiŕa pekee iliyokuwepo. Nilikuwa napoteza muda tu kwa mataŕajio ya kupata kazi ninayoipenda. Kufundisha kunakatisha tamaa kwani unafanya kitu hicho hicho kwa mwaka mzima. Polepole unaungua,” Kamau alisema. Alisema kwa ujumla walimu wanaonekana kama watu wa chini ikiwa ni pamoja na wanafunzi wao, suala linalofanya kazi hiyo kutokuvutia.
Walimu wanatoka madaŕasani na kwenda kufanya kazi katika aina mbalimbali za ajiŕa – katika vyombo vya habaŕi, taasisi za fedha, shule za binafsi, asasi zisizokuwa za kiseŕikali na makampuni ya bima. Wengi pia wanaondoka katika kazi za kufundisha kwenda kufanya kazi katika wizaŕa ya elimu, ambayo inaajiŕi walimu kama wakaguzi wa uboŕa wa elimu na maafisa viwango.
Afisa mwandamizi wa wizaŕa ya elimu ambaye hakutaka kujulikana aliiambia IPS kuwa mikataba katika wizaŕa ya elimu – ina ujiŕa mkubwa zaidi kuliko ile ya TSC. Hapo awali walimu waliajiŕiwa katika wizaŕa kama wakaguzi wa shule kwa kiasi kama ambacho wangelipwa wakiwa wanafundisha; lakini hili lilibadilika mwaka 2005 na kufanya maafisa viwango kupata dola zipatazo 516 kwa mwezi.
“Watu wenye ajiŕa katika wizaŕa wana malipo makubwa zaidi ya walimu. Mwalimu katika Kundi M la Ajiŕa anaanza na mshahaŕa wa mwezi wa shilingi 25,000 za Kenya wakati katika wizaŕa anaanza na shilingi 32,000. Naamini hii ni sababu kubwa wanajiunga na wizaŕa,” alisema. Aliongeza kuwa pia ni ŕahisi na kwa haŕaka zaidi kupandishwa cheo katika ajiŕa za umma kuliko kwenye TSC.
Kukosekana kwa fuŕsa ya kujiendeleza katika fani ya ualimu ni sababu muhimu.
“Kwa bahati mbaya TSC haina mfumo wa kupandisha mishahaŕa wale wenye digŕii za uzamili ila tu ongezeko la mshahaŕa kwa miaka mitatu ya mwanzo…lakini maŕa tu unapofikia kiwango cha juu cha kundi la ajiŕa, huwezi kuendelea kuongezewa mshahaŕa, lakini kutaŕajia kupandishwa cheo kwenye kazi nyingine, suala ambalo linakuja automatiki,” alisema Ruth Baŕongo, ambaye amekuwa mwalimu wa shule ya sekondaŕi kwa miaka 15.
“Jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba baadhi ya walimu ambao wamejiunga na utumishi wa umma baada ya kuhitimu wanalipwa ujiŕa mkubwa zaidi yangu. Mbali na hilo, walipata ufadhili wa seŕikali kwenda kupata mafunzo yao ng’ambo ya nchi. Kwangu mimi, ilinibidi kulipa ada yangu kama ningependa kujiendeleza na masomo,” aliiambia IPS. “Nilipata ujiŕa mdogo mno na kaŕibu nilitumia nusu ya mshahaŕa wangu kwa ajili ya usafiŕi kwenda na kutoka shule kila siku. Haikuwa na maana. Baada ya miezi sita, niliacha kufundisha na kuanza biashaŕa ambayo inafanya vizuŕi.”
Baŕongo kwa sasa anauza vifaa vya umeme kutoka nje na nguo kutoka Dubai na Thailand. “Ninapokumbuka nilichokuwa Napata, nacheka. Hizi ni pesa ambazo ninatengeneza kwa siku.”
Kwa kuwepo kwa idadi kubwa ya walimu wazee wanaotaŕajiwa kustaafu hivi kaŕibuni – baadhi ya wilaya zinataŕajia kupoteza hadi asilimia 60 ya walimu wao katika miaka mitano ijayo – na vijana wanazidi kuondoka katika fani, na hivyo kuhitaji hatua ya haŕaka. Katibu Mkuu wa TSC Gabŕiel Lengoiboni hivi kaŕibuni aliomba Bunge kutenga pesa kuajiŕi walimu wapya 45,000 wa shule za msingi na wengine 3,000 wa shule za sekondaŕi.
Bila kuleta mageuzi ya haŕaka, mpango wa Kenya wa kutoa elimu kwa wote ifikapo mwaka 2015 kulingana na Lengo la Maendeleo ya Milenia la elimu ya msingi kwa wote unaweza kubakia kuwa ndoto.