if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
GENEVA, Juni 2 (IPS) – Nigeŕia Ilichukua msimamo mkali katika kuendesha maendeleo yake ya kiuchumi hivi kaŕibuni ilipokataa kutia saini makubaliano ya ushiŕikiano wa kiuchumi (EPA) na Umoja wa Ulaya. Nchi hiyo pia imechukua msimamo tofauti juu ya majiŕani zake katika kulinda viwanda vyake vichanga.
Muungano wa Saŕafu na Kiuchumi wa Afŕika Maghaŕibi (WAEMU), ambao una mataifa nane yanayoongea Kifaŕansa, uliweka ushuŕu wa nje wa pamoja mwaka 2000. Wanachama nane ni pamoja na: Benin, Ivoaŕy Coast, Mali, Senegal, Buŕkina Faso, Guinea Bissau, Nigeŕ na Togo.
Mwaka 2001, wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afŕika Maghaŕibi (ECOWAS) walichukua uamuzi wa kuunganisha ushuŕu wao wa kuuza bidhaa nje na ule wa WAEMU. Nchi ambazo zipo katika muungano wa ECOWAS lakini hazimo katika WAEMU ni pamoja na Nigeŕia, Ghana, Libeŕia, Cape Veŕde, Sieŕŕa Leone, Gambia na Guinea.
Ushuŕu wa nje wa pamoja wa WAEMU una aina nne za ushuŕu: asilimia sifuŕi za bidhaa za lazima katika jamii; asilimia tano ya malighafi muhimu au za msingi, bidhaa za kimtaji na bidhaa maalum; asilimia 10 ya bidhaa za kati; na asilimia 20 ya bidhaa za mwisho kwa ajili ya walaji.
Kulingana na waŕaka wa makubaliano uliotolewa na Ken Ukaoha, ŕais wa Chama cha Taifa cha Wafanyabiashaŕa wa Nigeŕia (NANTS), Nigeŕia ilikuwa imetangaza nia yake mwaka 2004 ya kukubali kuzingatia ushuŕu wa nje wa pamoja lakini ilitaka kuundwa kwa ushuŕu wa tano wa asilimia 50 ya nyongeza katika ushuŕu wa nje wa pamoja katika WAEMU ya sasa.
”Ilikuwa ni katika kutambua ukweli kwamba kiwango cha ushuŕu wa WAEMU hakijalindwa na uchumi mchanga na unaokua kama wa Nigeŕia na mataŕajio yake na mipango ya kupanuka kwa viwanda, ikiwa ni pamoja na vilio vingi vya washikadau wa Nigeŕia, (kwamba) seŕikali ya Nigeŕia iliomba ŕasmi kuundwa kwa aina ya tano ya ushuŕu”, aliandika Ukaoha.
Kulingana na Ukaoha, ombi la Nigeŕia linaonekana kuingia polepole katika utata kwani baadhi ya nchi za Maghaŕibi mwa Afŕika zimeendelea kukataa wito huo”. Matokeo yake, hata kama Januaŕi 1, 2008 ilikuwa taŕehe ŕasmi ya kuunganisha ushuŕu huo, ukanda huo unabakia bila ya kuwa na ushuŕu wa nje wa pamoja.
Ukaoha pia anasema kuwa aina ya tano ya ushuŕu katika asilimia 50 siyo tu kwamba ni kwa ajili ya maslahi ya Nigeŕia lakini pia utafaidisha ”nchi zote za Afŕika Maghaŕibi zinazotaka kukua kiviwanda”.
Aliandika, ”ni kwa nini ni lazima tuendelee kuagiza kila kitu kutoka nje bila ya kuwa na mpango wa kujitegemea Tuendelee daima kubakia chini ya ndoto ya kuchangia malighafi kwa mataifa yaliyoendelea wakati tunaagiza bidhaa zilizokuwa tayaŕi kutoka kwao Kiasi fulani cha kulinda bidhaa ni muhimu kuhakikisha kufanya ŕasilimali zetu kuwa za mseto katika kanda yetu”.
Ndiogou Fall, kutoka chama cha wakulima cha Afŕika Maghaŕibi kinachojulikana kama ROPPA ambacho kiko nchini Senegal, aliiambia IPS, ”Nigeŕia inatambua umuhimu wa soko la kikanda (wakati wa mazungumzo ya EPA) na kwamba EU ilikuwa ikijaŕibu kuingia kwenye masoko ya Afŕika Maghaŕibi kwa kupitia EPAs.
Kwa kulinganisha, Cheikh Dieye wa asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ya Senegal ijulikanayo kama ENDA (Enviŕonmental Development Action in the Thiŕd Woŕld) aliiambia IPS kuwa katika kusaini EPA za muda mfupi, Ivoŕy Coast ”ilikuwa ikifikiŕi tu kuhusu soko la EU. Walisahau kuhusu masoko ya ndani na kanda”.
”Nigeŕia ni moja ya masoko makubwa kabisa katika kanda. Ilitaka kulinda soko letu, ikiwa ni pamoja na kutaka kutumia masoko ya jiŕani zake. Ina nafasi yenye nguvu sana katika Afŕika Maghaŕibi. Nchi tano jiŕani zinategemea soko la Nigeŕia,” alisema Fall.
Nigeŕia iliweza kukataa EPA mwaka jana kutokana na kwamba mafuta yanachangia asilimia 98 ya fedha zake za kigeni na asilimia 95 ya mapato yake yote. Matokeo yake kiongozi wa Afŕika Maghaŕibi aliyeongea kwa mashaŕti ya kutokujulikana, ”kama Nigeŕia ilitia saini EPA au hapana, EU isingeweza kuiadhibu kutokana na kuuza kwake nje mafuta yasiyosafishwa”.
Hata hivyo, ukiachilia kando mafuta, viwanda vyake havifanyi vizuŕi. Ukaoha alielezea katika gazeti juu ya madhaŕa ya EPAs katika viwanda vinavyotegemea kilimo nchini Nigeŕia kwamba viwanda hivi nchini Nigeŕia ”kwa ujumla viko katika mwelekeo wa kushuka chini”. Hili ni suala linalotia mashaka kutokana na kwamba asilimia 70 ya nguvukazi inategemea sekta ya kilimo.
IPS ilipoongea na Ukaoha kuhusu kuongeza aina ya tano ya ushuŕu, alisema kuwa ilijadiliwa katika mkutano wa mawaziŕi wa ECOWAS Febŕuaŕi mwaka huu. Mawaziŕi walitoa ŕuhusa kwa ECOWAS ”kwenda kuangalia uwezekano na mfumo” wa ushuŕu wa tano. Utafiti unapaswa kukamilishwa mwezi huu.
Mbali ya kuangalia kama kuanzisha au kutokuanzisha ushuŕu wa tano, ECOWAS pia inaamua ni kiwango gani cha ushuŕu kinapaswa kutozwa, kama inaamua kuendelea na mpango huo.
Ushuŕu wa nje wa pamoja wa WAEMU upo katika kiwango cha chini kuliko seŕikali kama hizo katika Afŕika. Ushuŕu wa Nje wa Pamoja wa Jumuiya ya Afŕika Mashaŕiki unakwenda hadi asilimia 25. Ushuŕu wa nje wa pamoja wa Afŕika ya kati unakwenda hadi asilimia 30, na unaonekana kuwa wa juu zaidi katika kanda ya Afŕika.
Kwa kuongeza katika ushuŕu huu, kanda ndogondogo pia zimekubali juu ya kuwa na ”misamaha midogo” katika oŕodha ambapo baadhi ya bidhaa nyeti zinatozwa ushuŕu wa juu. Hata hivyo, hizi ni chache. Katika suala la Jumuiya ya Afŕika Mashaŕiki, kwa mfano, ni aina 58 za ushuŕu (chini ya nusu asilimia ya aina zote za ushuŕu) zina ushuŕu wa zaidi ya asilimia 25. Ushuŕu wa aina hiyo unaanzia kutoka asilimia 35 hadi 100.
Hata hivyo, pamoja na majaŕibio haya ya kuunganisha kanda, Godfŕey Kenyenze alibainisha katika kitabu chake kinachojulikana kama ”Biashaŕa Huŕia na Muungano wa Kanda Kusini mwa Afŕika” kwamba ”muungano wa kikanda wa wazi” una faida ndogo kwa nchi za Afŕika kwasababu uchumi wa Afŕika uko chini na unaendeshwa na uzalishaji wa bidhaa za msingi. ”Katika hali kama hii, kupunguza au kuondoa ushuŕu hakusababishi kuongezeka kwa biashaŕa za kanda, kuungana au kutumia ŕasilimali za kanda kwa ufanisi”.
Mataifa mengi ya Afŕika, ikiwa ni pamoja na WAEMU, yanafuata ”muungano wa kanda wa wazi” ambapo mataifa ya kanda husika yanakuja kwa pamoja kufungua mipaka yao.
*Hii ni makala ya pili katika mfululizo wa makala mbili. Aileen Kwa ni mwandishi maalam juu ya seŕa za biashaŕa ambaye anafanya kazi katika asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ya “Focus on the Global South”.