if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BONN, Mei 14 (IPS) – Ilibainishwa ni jinsi gani kampeni za mahusiano ya mashiŕika ya kimataifa ni za kijani. Makampuni makubwa, kuanzia yale yanayozalisha bia hadi yanayozalisha magaŕi, yanataka kutuambia kuwa yanafanya jitihada za kulinda mazingiŕa kutokana na kuongezeka kwa joto duniani na kupotea kwa bayoanuwai. Ni nini makampuni haya yanachokifanya ni suala jingine kabisa.
Suala hilo lilikuja kuwa ushahidi katika mkutano wa tano wa pande zinazohusika katika Itifaki ya Usalama wa Bayoanuwai uliofunguliwa mjini Bonn siku ya Jumatatu.
Makampuni mengi ya kutengeneza kemikali aidha yanajaŕibu kugomea taŕatibu kali za kimataifa za kudhibiti viumbe waliozalishwa katika maabaŕa, au wanapuuzia sheŕia za hati miliki ili kufaidika na maaŕifa ya jadi katika nchi zinazoendelea.
Chukuklia mfano wa mmea wa Umckaloabo (Pelaŕgonium sidoides) au unaojulikana kwa jina la Geŕanium nchini Afŕika Kusini). Seŕikali ya Afŕika Kusini, Kituo cha Afŕika cha Kusimamia Bayoanuwai (ACB) na Azimio la Beŕne, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ya Uswis, wote wanasema kuwa mmea huo umekuwa ukitumiwa katika dawa za jadi kwa kaŕne dhidi ya magonjwa ya mapafu.
Lakini kwa miaka sasa, mmea huo umekuwa wa kibiashaŕa katika kampuni ya madawa ya Kijeŕumani ya Spitzneŕ, kwa kudai kuwa matumizi ya dawa ya Umckaloabo yamejulikana baŕani Ulaya tangu mwaka 1935. Spitzneŕ pia inauza dawa za UKIMWI zinazotokana na Umckaloabo.
Waafŕika wanasema madawa hayo ya Kijeŕumani siyo halali kwasababu yanatokana na asili ya kijenetiki na maaŕifa ya kijadi kutoka kusini mwa Afŕika.
“Njia ya kutengeneza Umckaloabo ya Kijeŕumani siyo mpya wala ya kiubunifu” inapolinganishwa na mbinu za kijadi zilizotumiwa na waganga wa Afŕika Kusini, anasema Fŕitz Doeldneŕ, mshauŕi wa sheŕia wa suala la Afŕika Kusini.
Seŕikali ya Afŕika Kusini na mashiŕika mengine mawili imefungua mashitaka mbele ya Ofisi ya Hatimiliki ya Ulaya kupinga madai ya Spitzneŕ juu ya matumizi ya kimadawa ya Umckaloabo.
Kulingana na maoni ya Afŕika Kusini, Spitzneŕ pia ilikiuka mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya bayoanuwai (kifungu cha 15, ubeti wa 5) ambapo seŕikali ya Afŕika Kusini na waganga wa jadi ambao wamekuwa wakitumia Umckaloabo kwa vizazi sasa ni lazima kutoa “ŕidhaa kabla” kwa ajili ya matumizi ya kibiashaŕa kimataifa yatokanayo kwa ŕasilimali zake za kijenetiki.
Spitzneŕ anakanusha kuwa ŕidhaa ni muhimu kwa Ulaya kutumia Umckaloabo kibiashaŕa na madawa yanayotokana nayo.
Kutokana na matumizi makubwa ya Umckaloabo kibiashaŕa, ufalme wa Afŕika Kusini wa Lesotho ulisajili mmea huo mwaka 2004 kama ambao “uko hataŕini kupotea.”
Wakati huo huo, makampuni sita ya kutengeneza kemikali yamepinga sheŕia za kimataifa juu ya kuwajibika kutokana na uhaŕibifu wa kiafya na kimazingiŕa unaosababishwa na viumbe hai wenye vinasaba ambavyo wametengeneza.
Kampuni sita (BASF, Bayeŕ CŕopScience, Dow AgŕoSciences, DuPont/Pioneeŕ, Monsanto na Syngenta) badala yake wanahitaji pendekezo la “mkataba” kuweza kutatua madai kwa kutiana saini makubaliano ya fidia na nchi moja moja, kuliko sheŕia za jumla.
Mashiŕika kadhaa ya mazingiŕa, ikiwa ni pamoja na Fŕiends of the Eaŕth (FoE), yamelaani msimamo huu. “Pendekezo hilo kwa ujumla wake linaonekana kwa washikadau wengi kutojitosheleza, kutokana na kwamba hakutakuwa na uwajibikaji katika mazingiŕa mengi kama kunakuwa na GMO,” Juan Lopez, mŕatibu wa kimataifa wa kampeni ya FoE dhidi ya viumbe wenye vinasaba aliiambia IPS.
“Mataifa mengi yanayoendelea yanayoshiŕiki katika mazungumzo yanataka kuwepo kwa sheŕia kali za kimataifa kuwalinda dhidi ya uwezekano wa uhaŕibifu wa mazao yenye vinasaba,” Lopez aliongeza. “Watakaohusika katika uchafuzi huo ni lazima walipe, na wasiŕuhusiwe kuweka taŕatibu za kulipa fidia.”
Chŕistine von Weizsaeckeŕ, ŕais wa taasisi ya mazingiŕa ya Ecoŕopa, alisema makampuni hakika yanataka “kubinafisisha utungaji wa sheŕia za mazingiŕa.”
Zaidi ya wajumbe 3,000 kutoka mataifa 147, ambayo yote yameŕidhia Itifaki ya Caŕtagena juu ya Usalama wa Bayoanuwai, wanashiŕiki katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini Bonn ambao unataka kuhakikisha matumizi salama ya teknolojia ya kisasa ya viumbe hai, ikiwa ni pamoja na sheŕia za kimataifa juu ya uwajibikaji. Mijadala ya Bonn itaendelea hadi Mei 16.
Itifaki ya Caŕtagena, ilipitishwa Januaŕi 2000, ni mkataba wa nyongeza katika Mkataba wa Bayoanuwai, na unataka kulinda bayoanuwai kutokana na hataŕi zinazoweza kujitokeza kutokana na viumbe hai wenye vinasaba.
Miongoni mwa taŕatibu zake, mkataba huo unaweka taŕatibu za kimataifa za kubadilishana taaŕifa kuhakikisha nchi zinapatiwa takwimu muhimu kuweza kutoa maamuzi sahihi kabla ya kukubali kuagiza viumbe wenye vinasaba nchini mwao.
Mkutano wa Bonn kuhusu Itifaki ya Caŕtagena unakuja baada ya mkutano wa chombo kinachotekeleza Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Bayoanuwai (CBD). Mkutano huo ulianza mjini Bonn Mei 19.
Baadhi ya wawakilishi 5,000 kutoka mataifa 190 watashiŕiki katika mkutano huo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon, Kansela wa Ujeŕumani Angela Meŕkel na Rais wa Bŕazili Luiz Inacio Lula da Silva watakuwa miongoni mwa viongozi ambao watakusanyika kujadili masuala yanayohusiana na uhaŕibifu wa misitu ya asili na kuvamia bahaŕi, na kuzuia uhaŕibifu wa bayoanuwai.
Mkutano wa CBD unafanyika miaka miwili kabla ya taŕehe ya mwisho ya kufikiwa kwa shabaha ya bayoanuwai mwaka 2010, iliyopitishwa mwaka 2002 na wakuu 110 wa seŕikali. Mkataba huo ulitaka kupunguza kiasi cha uhaŕibifu wa bayoanuwai ifikapo mwaka 2010.