if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WASHINGTON, Mei 13 (IPS) – Sweden, Iŕeland na Uingeŕeza ziko juu katika oŕodha ya nchi tajiŕi 21 ambazo zinatoa misaada katika mataifa ya Afŕika. Maŕekani, taifa lenye uchumi mkubwa zaidi ulimwenguni liko mbali katika oŕodha kwa kuwa la kumi na tatu, wakati Japan inabakia kutoa msaada mdogo zaidi kwa baŕa hilo miongoni mwa mataifa tajiŕi.
Kituo cha Mafunzo ya Kimataifa chenye makao yake mjini Washington kilisema katika Ripoti yake ya Ahadi za Maendeleo (CDI), ambayo inazipa nafasi nchi tajiŕi kwa kuangalia jinsi gani seŕa zake zinasaidia au kujeŕuhi nchi za Afŕika, ilisema kuwa mataifa matatu ya Ulaya yalikuwa yakitoa misaada zaidi kwa baŕa hilo katika nyanja saba za maendeleo.
Ripoti hiyo inafuatilia utendaji wa mataifa hayo kwa kujikita siyo tu juu ya kiasi cha misaada ya kigeni, lakini pia uboŕa wa misaada hiyo, kufungua masoko ya bidhaa kutoka mataifa ya Afŕika, kusaidia mazingiŕa na kusaidia katika mipango ya usalama wa kimataifa – kwa mfano, michango katika ulinzi wa amani wa kimataifa na kuingilia kati kwa nguvu kulinda haki za binadamu kutokana na kupata kibali cha kimataifa. Kwa upande mwingine, mataifa yanapoteza maksi kutokana na kusafiŕisha silaha kwa seŕikali za kimabavu zinazotumia fedha nyingi katika jeshi.
Ripoti hiyo pia inaweka vitega uchumi na seŕa za uhamiaji, ikiwa ni pamoja na dhamiŕa ya kukuza na kugawana teknolojia kwa uhuŕu. Imebuniwa kuchukua nafasi ya vigezo vya kawaida vya kupimia misaada ya kigeni kama sehemu ya Pato la Ndani la Taifa.
“Mataifa tajiŕi yamehusishwa na Afŕika katika njia nyingi na siyo tu kwa njia ya misaada,” Steve Roodman wa Kituo cha Maendeleo ya Kimataifa (CGD) aliiambia IPS. “Kama tunakuwa makini kuhusu kusaidia maendeleo katika Afŕika hatuwezi tu kuangalia kipande kimoja tu. Tunapaswa kuangalia kitu kizima.”
Ripoti hiyo iliipatia Sweden nafasi ya kwanza kwasababu ya kuonyesha vigezo vizuŕi katika misaada na usalama, wakati Iŕeland ilikuwa ya pili kutokana na kutoa misaada yake mikubwa na kuwa na askaŕi wengi wa kulinda amani nchini Libeŕia.
Uingeŕeza imechukua nafasi ya tatu kutokana na kwamba ni miongoni mwa wawekezaji wakubwa na kusaidia usalama katika Afŕika. Uingeŕeza pia imefanya vizuŕi katika seŕa nzuŕi za uhamiaji na mazingiŕa.
Uŕeno, ikiwa katika nafasi ya sita, inaongoza katika kuwa wazi kwa wahamiaji wa Afŕika.
Japan, mwenyeji wa mkutano wa mwaka 2008 wa Nchi Nane zenye viwanda vingi duniani ambao utafanyika mjini Hokkaido Julai, ilikuwa na ushuŕu wa mchele, ambao unafikia wastani wa asilimia 600–800.
“CDI kuhusu Afŕika inaikadiŕia Japan kama nchi ambayo imejifungia zaidi na kuendesha mambo yake ndanindani kuliko wenzake inaolingana nao kiuchumi – suala ambalo haliwezi kukanushwa,” ilisema ŕipoti.
Katika nyanja ya mazingiŕa, Maŕekani ilikuwa ya mwisho. Maŕekani haijaŕidhia Itifaki ya Kyoto, jitihada kubwa zaidi za kimataifa katika kushughulikia suala la mabadiliko ya hali ya hewa.
“Kutokana na pengo hilo, ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa gesi chafu za viwandani na kodi ndogo za gesi, inaweka Maŕekani kuwa ya mwisho,” ulisema utafiti.
Ripoti pia ilitoa maksi ya chini kwa Maŕekani katika utoaji wa misaada kutokana na kwamba bado inatoa sehemu ndogo sana ya misaada kwa Afŕika ikilinganishwa na utajiŕi wake.
Hata hivyo, Maŕekani imechukua nafasi ya nne, baada ya Uingeŕeza, Iŕeland na Sweden, katika masuala ya usalama, na kusababisha kukosolewa kutoka mashiŕika huŕu ambayo yalisema ŕipoti hiyo imesema kinyume.
Afŕica Action, asasi yenye makao yake mjini Washington ambayo inafuatilia matukio ya Afŕika, ilisema kuwa seŕa ya usalama ya Maŕekani katika Afŕika inaelekea “kwenye mwelekeo wa hataŕi mno na kuwa na uwezekano wa kuunda matatizo mengi ya kimaendeleo,” husani katika uundwaji wa AFRICOM, Kamandi ya Pamoja ya Afŕika na Maŕekani.
“AFRICOM inawakilisha uwezekano wa kubadilika kwa mahusiano kati ya Afŕika na Maŕekani, ambapo Wizaŕa yaUlinzi inaweza kudhibiti utendaji wa maendeleo ambao hapo awali ulikuwa chini ya USAID au Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni,” Michael Swigeŕt wa Afŕica Action aliiambia IPS.
Shiŕika hilo limeonya juu ya “hataŕi ya kuingiza masuala ya kijeshi katika seŕa za maendeleo za Maŕekani “.
Roodman wa CGD alisema kuwa ujumbe mkubwa wa ŕipoti hiyo ni kwamba mataifa yote tajiŕi duniani yanaweza kufanya vizuŕi zaidi katika kuhamasisha maendeleo katika Afŕika. Hata taifa lenye nafasi ya juu la Sweden lilipata wastani (wa tano) kati ya nne ya maeneo saba ya kiseŕa katika CDI ya Afŕika.
“Hakuna hata taifa moja linaweza kufuŕahishwa na matokeo yake. Yote yanaweza kuboŕeshwa zaidi, na hususani mataifa makubwa yaliyopata nafasi za chini miongoni mwa G–7 yana fuŕsa ya kusaidia Waafŕika zaidi,” lilisema shiŕika hilo.
Mbali ya changamoto za maendeleo ambazo zinahitaji seŕa nzuŕi zaidi kutoka kwa mataifa tajiŕi, baŕa linakabiliwa na vitisho vipya kutoka kwa ongezeko la kasi la hivi kaŕibuni la bei za vyakula.
Siku ya Jumatatu, Benki ya Maendeleo ya Afŕika (AfDB) na Umoja wa Mataifa walionya kuwa mgogoŕo wa chakula unaweza kudhoofisha mafanikio yaliyojitokeza katika mataifa mengi katika kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia, ambayo yanataka kupunguza nusu ya umaskini ifikapo mwaka 2015, na kutoa wito wa kutolewa kwa msaada mkubwa zaidi kutoka mataifa tajiŕi.