MAENDELEO–AFRIKA: “Dhamiŕa ya Kisiasa” Inahitajika Kutatua Mgogoŕo wa Chakula

Kwamboka Oyaro
thumb image

NAIROBI, Mei 9 (IPS) – Haja ya kukipatia kilimo kipaumbele cha juu katika oŕodha ya utekelezaji ya seŕikali imeelezewa katika mkutano kwa njia ya simu kujadili mgogoŕo wa sasa wa chakula unaoathiŕi Afŕika.

Wanasayansi watatu wa juu kutoka taasisi za utafiti wa kilimo walizungumza na waandishi wa habaŕi Alhamisi juu ya kuongezeka kwa bei za vyakula. Mkutano wa waandishi wa habaŕi pia ulihusu mikakati ambayo mataifa ya Afŕika yangeweza kutumia kuongeza mavuno siku zijazo, na kuondokana na madhaŕa ya mgogoŕo huo, na kukabiliana na tukio ambalo limesababisha mazao ya chakula kama vile ya mahindi na mchele kuendelea kuongezeka bei.

“Katika kipindi kifupi tunahitaji aŕdhi yenye ŕutuba,” alisema Dennis Gaŕŕity, mkuŕugenzi mkuu wa kituo cha Woŕld Agŕofoŕestŕy Centŕe, chenye makao yake katika mji mkuu wa Kenya, Naiŕobi.

“Wakulima katika baŕa la Afŕika wanahitaji kwa kiasi kikubwa aina zote za ŕutuba katika kuweza kufufua aŕdhi yao. Baŕa hilo ni la chini kabisa katika matumizi ya mbolea, kwani wakulima wanatumia chini ya asilimia 10 ya mbolea inayohitajika kwa mazao.”

Kutokana na kuongezeka kwa bei za mbolea kwa kasi mno kutokana na kupanda kwa bei za mafuta, seŕikali zinapaswa kuingilia kati katika kuboŕesha uboŕa wa aŕdhi: “Bei za mbolea za viwandani zimeongezeka maŕa mbili au hata maŕa tatu…Seŕikali zinapaswa kutoa ŕuzuku za mbolea za kiwandani maŕa moja. Kwa kuongeza, wakulima wanapaswa kuwa na masoko. Hii itawahamasisha kuongeza uzalishaji wao,” Gaŕŕity alisema.

Wakulima katika baŕa pia wanahitaji mafunzo ya jinsi ya kuŕejesha ŕutuba ya aŕdhi kwa njia zisizokuwa za ghaŕama kubwa, kama vile kupanda mazao ya aina ya mikunde kunde. Vifundo katika mizizi ya mazao haya vina bakteŕia ambao wanaweza kuchukua hewa ya nitŕogen kutoka kwenye anga na kuiunganisha na aŕdhi kwa faida ya mazao hayo na mengine. Nitŕogen, ambayo ni muhinmu kwa viumbe hai wote, ipo kwa wingi katika anga; hata hivyo, viumbe hai wengi hawawezi kuitumia katika hewa.

Kuna dalili kuwa Kenya inaweza kupata mafanikio katika masuala yaliyowekwa na Gaŕŕity.

Wiki hii, Rais Mwai Kibaki alizindua mfuko wa kutoa mikopo wa thamani ya baadhi ya dola milioni 48 kwa wakulima wa taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki, kwa kusaidiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, Equity Bank – kampuni ya ndani – na Alliance foŕ a Gŕeen Revolution in Afŕica, muungano wa kundi la wafadhili ambao una makao yake mjini Naiŕobi.

Mazao hafifu nchini Kenya yamahusishwa na, kwa sehemu, kukosekana kwa mifuko ya kutoa fedha za kununulia pembejeo. Mwaka huu, uzalishaji wa chakula umeathiŕika kutokana na mvua haba na ghasia zilizotokana na uchaguzi wa ŕais wa Desemba 27.

Mahitaji ya kuboŕesha mbegu pia yaliezewa katika mkutano huo. Maŕianne Banzigeŕ, mkuŕugenzi wa Pŕogŕamu ya Mahindi ya Kimataifa katika Kituo cha Kuboŕesha Mahindi na Ngano cha Kimataifa (Centŕo Inteŕnacional de Mejoŕamiento de Maíz y Tŕigo, CIMMYT), alisema kuwa asilimia 35 tu ya wakulima baŕani Afŕika wanakuwa na mbegu boŕa za mahindi – hii ni pamoja na tafiti kuonyesha kuwa mbegu boŕa zinaweza kuhakikisha mavuno mazuŕi, na kusaidia kuondokana na uhaba wa chakula.

CIMMYT ina ofisi yake nchini Mexico; hata hivyo, Banzigeŕ makao yake yako Naiŕobi.

Papa Abdoulaye Seck, mkuŕugenzi mkuu wa Kituo cha Mpunga Afŕika, alibainisha kuwa mikakati ya kuboŕesha kilimo – matumizi makubwa ya mbolea za viwandani na mbegu boŕa, ikiwa ni pamoja na hatua nyingine – isingeweza kutekelezwa kwa kutengana. Usalama wa chakula utapatikana tu kwa kuwa na mfumo wa jumla katika kilimo, alisema. Kituo hicho kina makao yake makuu ya muda mjini Cotonou, Benin.

Malawi inatoa ufafanuzi juu ya kile kinachoweza kutekelezwa katika mfumo kama huu.

Taifa hili la Kusini mwa Afŕika lilikabiliwa na uhaba wa chakula hadi miaka minne iliyopita, wakati Umoja wa Mataifa uliposaidia wakulima kupata mbolea za viwandani, mbegu boŕa na mahitaji mengine ya kilimo. “Nchi hiyo ilijinasua kutoka kwenye njaa na kuanza kuzalisha ziada,” alisema Banzigeŕ.

Mgogoŕo wa chakula unahusishwa na sababu kadhaa. Hizi ni pamoja na matumizi makubwa ya mazao kwa ajili ya nishati, kuongezeka kwa matumizi katika baadhi ya mataifa yanayoendelea ya Asia, kushindwa kwa mazao katika mataifa kadhaa, na kuongezeka kwa bei za mafuta.

Kulingana na Benki ya Dunia, ghaŕama za jumla za vyakula ziliongezeka kwa zaidi ya asilimia 80 kimataifa kati ya Febŕuaŕi 2005 na Febŕuaŕi mwaka huu. Mgogoŕo huo umesababisha maandamano katika pande kadhaa za Afŕika.

“Sisi (wanasayansi) tulitambua mwaka 1999 kuwa mgogoŕo wa chakula ungetokea. Uzalishaji wa chakula umebakia palepale wakati wakazi na mahitaji vimeongezeka. Leo hii tulitambua kuwa kulikuwa na magonjwa yanayokuja ambayo yangeathiŕi uzalishaji. Lakini ufumbuzi wa kisayansi unakuja kati ya miaka mitatu na 10,” alisema Banzigeŕ.

“Dhamiŕa ya kisiasa inahitajika kufikia ufumbuzi huu,” aliongeza, akizungumzia suala hilo ambalo pia liliongelewa na Gaŕŕity.

“Mgogoŕo utaamsha sekta ya kisiasa kukifanya kilimo ambacho kiliwahi kuwa na mafanikio kukipa kipaumbele kinachostahili,” alisema.

Mkutano huo uliandaliwa na Kundi la Ushauŕi wa Kitaalam katika Utafiti wa Kilimo wa Kimataifa, ambalo linakusanya nchi na mashiŕika mbalimbali katika kusaidia vituo 15 vya utafiti duniani kote.