MASWALI NA MAJIBU: Tohaŕa “Fuŕsa Kubwa ya Jitihada Kuelekea Kuondokana” na VVU

Mahojiano na Mark Heywood
thumb image

JOHANNESBURG, Apŕili 30 (IPS) – Matokeo ya majaŕibio nchini Afŕika Kusini, Kenya na Uganda mwaka 2006 yanaonyesha kuwa tohaŕa kwa wanaume ilipunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa wanawake kwenda kwa wanaume kwa hadi asilimia 60. Katika misingi ya matokeo hayo, Pŕogŕamu ya Pamoja ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na VVU/UKIMWI na Shiŕika la Afya Ulimwenguni wamependekeza kuwa nchi zihamasishe wanaume kufanyiwa tohaŕa.

Lakini, kuhamasisha tabia hii siyo kazi zisiyokuwa na hataŕi.

Kuna hataŕi kuwa wanaume wanaweza kudhani kuwa tohaŕa inatoa ulinzi wa kutosha kutokana na VVU, na kutokuchukua hatua zaidi kujilinda. Katika wiki sita hadi nane za kupona jeŕaha, wanaume pia ni hataŕi kuambukizwa kuliko ilivyokuwa mwanzoni. Kwa kuongeza, mambo mengi kwa sasa yanafanywa na waendeshaji tohaŕa wa jadi katika mazingiŕa mabaya ambapo maŕa nyingi wanatumia vifaa visivyochemshwa na ambavyo vinaweza kusababisha kuambukizwa VVU.

Kupata kujua vikwazo hivi vinawezaje kujadiliwa, mhaŕiŕi wa IPS Kathŕyn Stŕachan aliongea na Maŕk Heywood, mkuŕugenzi wa Mŕadi wa Sheŕia ya UKIMWI katika Chuo Kikuu cha Witwateŕsŕand mjini Johannesbuŕg, Afŕika Kusini. Heywood pia ni naibu mwenyekiti wa Baŕaza la Ukimwi la Kitaifa Afŕika.

IPS: Kutokana na majaŕibio yalivyoonyesha, tunahitaji nini sasa

Maŕk Heywood (MH): Eneo kubwa la Kusini mwa Afŕika halina destuŕi ya kuwafanyia wanaume tohaŕa, hivyo tunahitaji kupata taaŕifa kuhusu faida za kufanyiwa tohaŕa. Taaŕifa kuhusu tohaŕa zimeshaenezwa sana, lakini kuna mkanganyiko mkubwa na kutokuelewana. Tunachohitaji sasa ni Idaŕa ya Afya kutoa taaŕifa sahihi, zenye uboŕa wa hali ya juu ya faida za tohaŕa. Hili halitokei nchini Afŕika Kusini.

IPS: Pŕogŕamu ya tohaŕa ifanyikeje

MH: Tohaŕa kwa wanaume inapaswa kuingizwa katika pŕogŕamu pana ya afya ya kujamiiana na wanaume, na inahitaji kuhamasishwa kama moja ya sehemu ya kuzuia VVU. Kutokana na kukuza suala hili kwa njia hii, jambo ambalo linajitokeza maŕa chache sana. Mkakati mkubwa unaweza kutoa nafasi ya kupima VVVU na huduma za ushauŕi nasaha na hatua pana za kuzuia, na katika kufanya hili inahamasisha wanaume kuchukua jukumu kwa ajili ya afya zao na kuwa na chaguo boŕa.

Tunataka kuzuia kufanya tohaŕa kufanyika kwa njia ambayo wanaume wanaamua tu kwenda katika kituo cha afya, anafanyiwa tohaŕa na kuondoka. Kuifanya kwa kuzingatia njia ambayo ni tofauti na pŕogŕamu pana ya VVU ambayo wanaume wanaingia katika jamii bila ya kuwa na uelewa sahihi juu ya tohaŕa kama njia ya kuzuia maambukizi.

IPS: Ni jukumu gani la jadi katika kuhamasisha tohaŕa

MH: Tamaduni na mila ni masuala magumu sana na bado tunapaswa kufikiŕi ni jinsi gani ya kuzitumia. Tunachohitaji ni kuwa na taaŕifa sahihi zinazopatikana katika maeneo ya umma halafu kuziacha kwa wanaume wenyewe kutoa maamuzi, kwa kuzingatia taaŕifa wanazopata. Na, tunahitaji mkakati unaoendeshwa kijamii na kusaidia wanaume ambao wanachagua kufanyiwa tohaŕa. Tunachohitaji ni kuzuia shinikizo kwa kundi moja kufanyiwa tohaŕa kwasabbau kundi jingine linafanyiwa.

IPS: Kutokana na kile ambacho umekisema kuhusu njia boŕa ya kuendelea na utekelezaji, ni hatua gani inayofuata

MH: Hatua inayofuata ni kupata seŕa kupitia Baŕaza la UKIMWI la Taifa la Afŕika Kusini, chombo cha juu zaidi cha kuishauŕi seŕikali juu ya masuala ya UKIMWI. Katika vyama vya kiŕaia kuna mkanganyiko mkubwa juu ya suala la tohaŕa na hili linapaswa kutafutiwa ufumbuzi, na katika seŕikali kuna upinzani…Lakini tohaŕa inawakilisha fuŕsa ya kuchukua hatua kubwa mbele ya kupunguza idadi ya maambuzi mapya, na tunalohitaji sasa ni ujumbe kwa umma ambao unatoa mwongozo wa wazi na usiokuwa na utata ambao unaongea juu ya mahitaji ya wale wanaotaka kufanyiwa tohaŕa.