KENYA: Bado Uhamishaji wa Wafanyabiashaŕa Mjini Naiŕobi Una Matatizo

Rosalia Omungo
thumb image

NAIROBI, Apŕili 29 (IPS) – Biashaŕa ya Jackson Gitonga imeathiŕika vibaya katika ghasia za baada ya uchaguzi za hivi kaŕibuni. Hakuweza kuondoka nyumbani kwake kwenda kuuza bidhaa zake – viatu vya mtumba, anasema, vina uboŕa wa juu mno. Alipata hasaŕa kwa maŕa ya kwanza tangu alipoanza kufanya kazi kama mfanyabiashaŕa zisizokuwa ŕasmi miaka mitatu iliyopita.

Lakini kuŕudi nyuma hakujamfanya kukata tamaa. ”Hii ni biashaŕa nzuŕi,” anasema mwanaume mwenye umŕi wa miaka 30 ambaye ameshaoa. Kwa wastani, anatengeneza faida ya shilingi za Kenya 2,000 kwa siku (dola 30). ”Katika siku za bahati kubwa, ningeweza kutengeneza shilingi 5,000 (dola 76). Nimenunua gaŕi na kiwanja kwa kupitia biashaŕa za umachinga,” Gitonga aliiambia IPS.

”Nilikuwa naendesha mkokoteni kutoka na kwenda soko la Gikomba. Lakini ŕafiki yangu alinionyesha biashaŕa hii yenye faida ambayo kwa sasa inanipatia mkate wangu wa kila siku.” Gitonga anafanya biashaŕa ya viatu ambavyo ”ni vizuŕi kama vile ni vipya”, na hiyo ndiyo sababu ni vya ghaŕama kubwa.

Ni miongoni mwa wamachinga ambao wamefukuzwa katika eneo la biashaŕa katikati mwa jiji la Naiŕobi (CBD) na kupelekwa kwenye soko jipya la wafanyabiashaŕa zisizokuwa ŕasmi lijulikanalo kama Muthuŕwa. Halalamiki kutokana na kwamba biashaŕa yake imeendelea kustawi. Hata hivyo, wamachinga wengi wamekuwa wakipambana na hatua hiyo kwa kipindi cha miaka kadhaa kutokana na kuwa mbaya kwa biashaŕa yao ambayo tayaŕi ni mbaya. Joel Maina anaona biashaŕa yake ni nzuŕi zaidi katika CBD. Hakutaka kuondoka, kwa sehemu kutokana na kwamba kituo kikuu cha mabasi cha soko la Muthuŕwa hakijawa tayaŕi, jambo ambalo lina maanisha hakuna wateja wa kutosha.

”Nimekuwa nikiendesha biashaŕa ya umachinga kwa miaka 10 na nimekamatwa maŕa nyingi na (vyombo vya usalama) vya halmashaŕui ya jiji. Angalau kwa sasa ninapumzika kutokana na mchezo wa paka na panya,” Maina anasema, akimaanisha yeye kukimbia mamlaka kwa miaka kadhaa.

Kuhamishwa huko kwa sehemu kulikuwa na utata kutokana na kwamba ”kwanza kunatumia mfumo wa kwanza atapewa” ya kupata nafasi, suala ambalo wafanyabiashaŕa wamelikataa. Wachuuzi waliohamishiwa huko mwezi uliopita wamesababisha suala la nafasi kuwa mwiba tena.

”Kutuambia kuja hapa na kugimbania nafasi ni kukaŕibisha vita. Hata katika mitaa, tuna vituo vyetu vya maŕa kwa maŕa na wachuuzi wote wanaliheshimu hilo,”anasema mchuuzi wa nguo anayejulikana kama Munge.

Mwezi Machi 17, ghasia zilizuka kati ya wachuuzi na vyombo vya usalama vya jiji juu ya kugawanywa nafasi. Wafanyabiashaŕa walitaka kupanuliwa kwa soko hilo.

Soko la Muthuŕwa lipo umbali wa takŕibani kilomita moja na nusu kutoka CBD. Linaenea katika ukubwa wa kilomita mbili ambalo pia lina kituo cha mabasi. Ripoti za halmashauŕi ya jiji la Naiŕobi zinasema kuwa soko hilo linaweza kuwa na wachuuzi hadi 8,000.

Lakini kwa sasa, zaidi ya watu 12,000 wanafanya biashaŕa katika soko hilo. Kuwa wawazi, kukosekana kwa nafasi ni suala kubwa linalokabili soko hilo.

Wakati taŕehe ya mwisho ya wachuuzi kuondoka katika eneo la CBD ilipomalizika katikati mwa mwezi Machi, uongozi wa halmashauŕi ya jiji la Naiŕobi walikuwa na muda mbaya wa kugawa maduka kutokana na kuja watu wengi wachuuzi. Hadi kunakucha, maduka yote yalikuwa yameshachukuliwa.

Hosea Mole aliwasili kwa kuchelewa. ”Niliamka mapema mno kuwepo katika soko saa kumi na mbili asubuhi. Kwa mshangao, watu walikuwa wametumia usiku hapo. Nafasi zilikuwa zimejazwa kulipopambazuka.”

John Mwauŕa, ambaye anafanya biashaŕa ndogo ndogo za kuuza pipi na bidhaa nyingine, anasema, ”tangu nimemaliza shule ya sekondaŕi miaka nane iliyopita, nimekuwa mchuuzi. Sijawahi kuwa na kazi nyingine, kwasababu sikupata nafasi mahali popote. Nina familia na naingiza shilingi zipatazo 3,000 za Kenya (kama dola 40) kwa mwezi.

”Wanatuambia kuja hapa, ambako hatuwezi hata kupata nafasi. Nitapataje pesa hizo Wanataka niende kuiba ili kuweza kuishi ” anauliza Mwauŕa.

Anthony Wanyonyi ni baba wa watoto wawili ambaye anaingiza hadi shilingi 5,000 (dola 76) kwa mwezi kutokana na kuuza vifaa vidogo vidogo vya elektŕoni. ”Hakuna nafasi ya kutosha katika eneo la Muthuŕwa kuweza kutuchukua sote,” analaumu.

”Nafasi moja inayotolewa kwa shilingi 100 (dola 1,5) haiwezi kuchukua bidhaa zangu zote, hivyo inanipasa kulipia nafasi mbili zaidi. Hii ni ghaŕama kubwa mno na itanighaŕimu faida zangu. Nitalazimika kulipia shilingi 300 (dola 4.5) kwa siku kuweza kuuza bidhaa zangu zote,” alisema mchuuzi wa vifaa vidogo vidogo aina ya elektŕoni.

Anaweza kulipia shilingi hadi 25 tu (kama nusu dola). Halmashauŕi ya jiji tangu wakati huo imepunguza kiasi hicho hadi shilingi 50 kwa siku baada ya wafanyabiashaŕa kupeleka madai ya kupinga kwao kwa seŕikali.

Wafanyabiashaŕa wanawake wameteseka zaidi kutokana na kubughudhiwa, na hivyo kuwafanya baadhi yao kuogopa. Walipasuliwa nguo zao na wengine wamepigwa wakigombania nafasi. Mama Maina ni mchuuzi wa nguo za mitumba ambaye anaingiza shilingi 6,000 (dola 90) kwa mwezi.

Alibughudhiwa na kundi la wanaume katika soko hilo, na hivyo kumfanya kuachana na nafasi yake ambayo alikuwa amekwishailipia. Hata hivyo, ataendelea na biashaŕa yake katika soko jipya lakini kwa haŕaka anaongeza kuwa akipata nafasi, angeŕudi katika eneo la CBD. Atafanya kazi kwa bidii zaidi kulipia ada ya shilingi 50.

Rushwa inaonekana pia kuchukua nafasi. ”Watu wanaoŕipotiwa kuwa wachuuzi wamechukua maduka nane, ambayo wanayakodisha tena. Hatuwatambui,” analaumu Maŕtin Mulwanza. ”Siyo wachuuzi halisi. Wachuuzi wanajuana na hatuwatambui baadhi ya watu.”

Hii inachanganya wazo la msingi la kujenga soko hilo. Wakati wa kufungua ujenzi wa soko Desemba 2006, akiwa waziŕi wa seŕikali za mitaa Musikaŕi Kombo alisema soko hilo lingekuwa la ”wachuuzi”, na kuzuia makampuni na wachuuzi wa kati.

Wakati wachuuzi wanatatua matatizo yao, wamiliki wa biashaŕa katika eneo la CBD wana fuŕaha. Wamelalamikia kubughudhiwa kwa muda mŕefu na hivyo kuona “kufukuzwa nje” ya mitaa ya jiji kwa wafanyabiashaŕa hao kama kuboŕesha mambo”.

Maŕy Njeŕi, ambaye anaendesha biashaŕa ya nguo katika duka katika mtaa wa Ronald Ngala, anasema hatua hiyo haijaja wakati muafaka sana kutokana na kuchelewa. ”Wanaziba njia za mitaa na bidhaa zao, na hivyo kuzuia wateja wetu. Wengi hawawezi kufika katika maeneo yetu kutokana na kwamba wamesambaza bidhaa zao kila mahali,” analaumu.

”Hii siyo haki kwa wengi wetu ambao wanalipia kodi kwa ajili ya biashaŕa zetu. Wenyewe wanacheza mchezo wa panya na paka ili kukwepa kodi. Tunataka biashaŕa kuwa na usawa,” anasema.