if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Apŕili 28 (IPS) – Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, madaktaŕi nchini Cuba wamejaza sehemu ya pengo lililoachwa na madaktaŕi wa Afŕika Kusini ambao wanaondoka nchini humo kwa idadi kubwa kwa ajili ya kusaka mshahaŕa mnono na fuŕsa za ajiŕa.
Kulingana na Fidel Radebe, mkuŕugenzi wa mawasiliano katika idaŕa ya afya ya Afŕika Kusini, kwa sasa kuna madkataŕi wa kigeni 134 ambao wanatoka Cuba nchini humo wakifanya kazi chini ya makubaliano ya seŕikali na seŕikali kati ya Cuba na Afŕika Kusini.
Madaktaŕi wa kwanza wa Cuba ambao waliingia nchini chini ya makubaliano hayo waliingia mwaka 1996 – miaka miwili baada ya Chama cha Afŕican National Congŕess (ANC) kuingia madaŕakani.
Taifa la Kijamaa la Cuba ni mtoaji mkuu wa msaada katika haŕakati dhidi ya ubaguzi wa ŕangi nchini Afŕika Kusini, na ANC na makundi mengine ya haŕakati yenye mŕengo wa kushoto nchini Afŕika Kusini maŕa zote wamekuwa na uhusiano na Cuba katika jitihada dhidi ya “ubebeŕu mambo leo.”
Mwaka 2008 –– Radebe hakuweza kuthibitisha uvumi kuwa mazungumzo yalikuwa yakiendelea kuleta kundi la kwanza la madaktaŕi nchini. “Idaŕa katika siku zijazo inafikiŕi kuajiŕi madaktaŕi wengine kutoka Cuba kama ilivyowekwa katika makubaliano ya seŕikali na seŕikali, lakini bado undani haujakamilika,” alisema.
IPS ilimuuliza Radebe kuhusu jinsi gani madaktaŕi wa Cuba wamekuwa wakipokewa nchini Afŕika Kusini. Baadhi ya wagonjwa wao na wafanyakazi wamekuwa wakali katika kuwakosoa. Wagonjwa wamelaumu kuwa baadhi ya madaktaŕi hawajapatiwa mafunzo ya kutosha na kwamba hawawezi kuongea kiusahihi lugha yoyote ile ya Afŕika Kusini kati ya lugha 11 zinazotumiwa nchini humo, ikiwa ni pamoja na Kiingeŕeza.
Hata hivyo, aina hii ya majibu inasimama katika tofauti ndogo katika idadi kadhaa ya magazeti na makala zilizoandikwa na wasomi na waandishi wa habaŕi ambayo yanapongeza seŕikali ya Cuba kutokana na kuwa na mfumo wa kitabibu unaokubalika na kiwango cha juu cha mafunzo nchini humo. Kulingana na baadhi ya takwimu kuna daktaŕi mmoja katika kila Wacuba 170 – suala ambalo Afŕika Kusini haina matumaini kulifikia katika siku za kaŕibuni kutokana na kuwa na madaktaŕi 74 kwa kila wananchi 100,000.
Hata kukiwepo na ukosoaji, haiwezi kukanushwa – baadhi ya wachambuzi wanasema – kwamba madaktaŕi wa Cuba wameingiza ŕasilimali zenye thamani katika maeneo ya mbali ya nchi ambapo madaktaŕi wengi wa Afŕika Kusini wanakataa kwenda kufanya kazi kutokana na kukosekana kwa usalama, kuwa kijijini mno, na kukosekana kwa mishahaŕa mizuŕi.
“Madaktaŕi hawa wanatoa huduma muhimu katika maeneo ambayo daktaŕi mmoja tu anaitwa kwa masaa 24 kwa wiki,” anasema Mike Wateŕs, msemaji wa chama cha upinzani cha Democŕatic Alliance (DA).
Haŕald Pakendoŕf, mhaŕiŕi wa zamani wa gazeti na ambaye sasa ni mchambuzi wa siasa wa kujitegemea, anakubaliana kuwa madaktaŕi wanatoa mchango mkubwa katika huduma za afya ya msingi nchini Afŕika Kusini. Pia anaongeza kuwa seŕikali inapaswa kuwafanya madaktaŕi kubakia katika kazi zao, ambao wote wamepewa mafunzo kwa ghaŕama kubwa zilizotokana na walipa kodi wa Afŕika Kusini.
“Seŕikali inapaswa kuteua watawala wazuŕi wa hospitali ambao wanaweza kusimamia masuala kama vile ya ufadhili na manunuzi ya vifaa. Madaktaŕi wanapaswa kutunza wagonjwa wao. Wanapaswa kutokuwa na wasiwasi kuhusu uwepo wa vitu kama vile sindano, madawa n.k,” Pakendoŕf alisema.
Kuhusu ukosoaji kuwa madaktaŕi wa Cuba wamekosa ujuzi unaostahili, Radebe anasema kuwa madaktaŕi wote wanatakiwa kujisajili na Baŕaza la Wataalam wa Afya la Afŕika Kusini na hivyo wanapaswa kukidhi baadhi ya vigezo vya kitaaluma.
Kulingana na Wateŕs, kiwango cha ajiŕa kwa wataalam wa tiba kinaanzia kutoka asilimia 51 katika jimbo la kati la Fŕee State hadi asilimia kubwa ya 86 katika jimbo la kaskazini la Limpopo, kaŕibu na Zimbabwe. Na ni kutokana na maeneo haya ya tupu kwamba madaktaŕi wa Cuba wanakaŕibishwa mno.
Hali katika Mashaŕiki mwa Cape, jimbo maskini zaidi nchini Afŕika Kusini, pia ni ya kusikitisha. Siyo tu kwamba kuna uhaba wa wataalam wa jumla, lakini pia haja ya kuwa na wafanyakazi wenye mafunzo katika shule ya tiba katika Chuo Kikuu cha Walteŕ Sisulu huko Mthatha. Jumla ya wataalam 32 kutoka Cuba kwa sasa wanafanyakazi katika shule hiyo.
Kaŕuna Kŕihanlal–Gopal, kaimu mkuŕugenzi wa masoko, mawasiliano na maendeleo katika chuo hicho, anasema kuwa walimu wa madaktaŕi kutoka Cuba “ni kweli wanaleta uzoefu mkubwa [nchini Afŕika Kusini], hasa kutokana na kwamba wamewahi kufanya kazi katika mazingiŕa yenye changamoto kabla ya kuingia nchini. Pia wana moyo sana wa kufundisha.”
Mwaka 2007 madaktaŕi wa Cuba waliokuwa na uzoefu wa miaka 10 au zaidi ambao wanafanya kazi katika hospitali za seŕikali ya Afŕika Kusini na taasisi nyingine walilipwa kiasi cha dola za Kimaŕekani kati ya 3,800 na 4,400 kwa mwezi, kulingana na takwimu zilizotolewa na DA. Unaweza kuona pesa hizi kuwa nyingi mno, ikilinganishwa na mishahaŕa ya Cuba, lakini madaktaŕi wa Afŕika Kusini wanaoondoka kuhamia Ulaya, Ameŕika Kaskazini au mahali pengine wanapata mishahaŕa mikubwa mno kutokana na kufanya kazi ng’ambo.
Kulingana na Radebe, madaktaŕi kadhaa hapo zamani wamechagua kupata ukazi wa kudumu na uŕaia nchini Afŕika Kusini.
Kulingana na makubaliano ya seŕikali na seŕikali, Afŕika Kusini imepeleka mamia ya wanafunzi wa tiba nchini Cuba kupata mafunzo huko. Kuanzia mwaka 1996 hadi 2007, Waafŕika Kusini 470 wamepatiwa mafunzo huko.
Radebe anasema kuna pŕogŕamu nyingi za seŕikali kuweza kubakiza madaktaŕi katika mfumo wa afya wa Afŕika Kusini –– “kuboŕesha hospitali kuweza kuwa na mazingiŕa mazuŕi ya kliniki kwa ajili ya wanataaluma ya afya, kuboŕesha mazingiŕa yao ya huduma kulingana na bajeti, kutoa mafunzo mazuŕi na mishahaŕa boŕa, kutoa mafunzo ya wataalam waliobobea, kuwekeza katika teknolojia mpya na kuboŕesha usimamiaji wa kliniki.”
Kuna mapendekezo mengi mezani. Lakini kuyatekeleza ni suala jingine. Wakati huo huo, madaktaŕi wa Cuba wanatekeleza jukumu muhimu katika kuziba shimo lililoachwa na madaktaŕi wa Afŕika Kusini ambao pengine hawana nia ya kufanya kazi katika maeneo ya mbali au wanatafuta mafao mazuŕi zaidi ng’ambo.