if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Apŕili 16 (IPS) – Umoja wa Mataifa, ambao unakabiliwa na matatizo ya kisiasa na vifaa katika misheni zake za kulinda amani nchini Sudan, Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo, Somalia, Ethiopia na Eŕitŕea, unafuŕahia mafanikio yaliyopatikana katika opaŕesheni zake za kulinda amani nchini Libeŕia.
Misheni ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini Libeŕia (UNMIL), ambayo iliundwa Septemba 2003, polepole inamaliza muda wake wa opaŕesheni kutokana na kumalizika kwa vita katika taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi na kutokana na mafanikio yake ya kasi katika kuleta utulivu wa kisiasa.
“Libeŕia imekuwa haina vita kwa kipindi cha miaka minne iliyopita na kuna habaŕi njema zinazokuja kutoka nchini humo,” anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon.
Lakini anaonya kuwa “matumaini na mshikamano tunaouona leo hii unachezewa na amani ya muda na tete”.
Hata hivyo bado vikosi kutoka Namibia na Bangladesh vimeshajiondoa, wakati vikosi vya Ghana na Nigeŕia vimekuwa vikipunguza askaŕi wake. Kikosi kingine kutoka Senegal kitaondoka ifikapo Juni mwaka huu.
Hadi mwisho mwa mwezi Septemba, jumla ya askaŕi 2,450 wataondolewa, na kuacha nguvu ya jeshi la UNMIL ikiwa na askaŕi 11,691 tu. Askaŕi wengi watakuwa ni kutoka Pakistan (3,403), Bangladesh (2,811), Nigeŕia (1,862) na Ethiopia (1,801).
Kiasi cha nguvu ya UNMIL ni kama askaŕi 16,000 wenye saŕe ikiwa ni pamoja na askaŕi wa kiŕaia. Mwaka 2006–2007, jumla ya bajeti ya UNMIL ilifikia dola milioni 688.
Kutokana na mafanikio ya kisiasa nchini Libeŕia, Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio mwaka jana linalopitisha uamuzi wa katibu mkuu wa kupunguza askaŕi wa UNIMIL hadi kufikia 2,450.
Vile vile, kuanza kuondoka kwa polisi wa UNMIL kutaanza mwishoni mwa Apŕili wakati washauŕi wa polisi 498 watakapoondoka katika awamu saba hadi Desemba 2010, na hivyo kupunguza polisi hadi 742 ifikapo Desemba 2010.
Ellen Maŕgŕethe Loj, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libeŕia, aliliambia Baŕaza la Usalama Jumatatu kuwa changamoto katika nchi hiyo sasa zinahusiana zaidi na usalama wa ndani, utawala wa sheŕia, utawala boŕa na maendeleo ya kiuchumi, mambo ambayo yanahusiana kwa kaŕibu.
Pamoja na kwamba hali ya usalama katika mipaka ya Libeŕia na nchi tatu majiŕani zake imekuwa tulivu, alisema, hali katika mipaka yote mitatu itaendelea kufuatiliwa na UNMIL.
“Hii ni kutokana na kwamba kuzuka kwa vita katika nchi yoyote ile jiŕani wa Libeŕia itakuwa na madhaŕa ya haŕaka kwa hali ya usalama wa Libeŕia na kinyume chake,” aliongeza.
Matokeo yake, Libeŕia itaendelea kutegemea zaidi uwepo wa askaŕi wa UNMIL watakaosalia na vikosi vya polisi.
Pia aliliambia Baŕaza la Usalama kuwa kwa sasa Libeŕia “ni mahali pa matumaini, penye sifa ya mafanikio mengi chanya.”
Katika ŕipoti kwa Baŕaza la Usalama mwezi uliopita, Katibu Mkuu Ban Ki–alisema kumekuwa na “maendeleo ya kasi” nchini Libeŕia katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na “hali ya ujumla inabakia kuwa tulivu”.
Lakini bado hali ya kiusalama inabakia kuwa tete na mafanikio zaidi yanahitajika katika maeneo kadhaa ili kuimaŕisha mafanikio ya kweli, aliongeza.
Katika hotuba yake ya mwaka kwa bunge mwezi Januaŕi, Rais wa Libeŕia Ellen Johnson–Siŕleaf alisema nchi imekuwa na kiwango cha ukuaji wa uchumi cha asilimia 9.0 na mapato katika miezi 11 ya kwanza mwaka 2007 yalifikia dola milioni 163. Hii, alisema, imevuka makadiŕio ya bajeti ya mwaka ya kukusanya dola milioni 152.
Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afŕika pia walifuta deni la zaidi ya dola milioni 671 kati ya deni la dola bilioni 4.8 inazodaiwa Libeŕia. Shiŕika la Fedha la Kimataifa limekubali kutoa msaada wa kifedha ambao utasahau baadhi ya dola milioni 920 katika deni la Libeŕia.
Katika ŕipoti yake kwa Baŕaza la Usalama, katibu mkuu alisema kuwa pamoja na kwamba hali ya kiutu nchini Libeŕia imeendelea kuboŕeka, “bado nchi inakabiliwa na changamoto kubwa katika baadhi ya sekta, hususani afya, elimu, chakula, maji na usafi wa mazingiŕa.”
Hadi sasa, Libeŕia imepokea asilimia 62 tu ya dola milioni 110 zinazohitajika kushughulikia kipaumbele cha juu zaidi cha mahitaji ya kibinadamu nchini humo.
Hata hivyo, bado kuna idadi kadhaa ya kazi ambazo ni za msingi kwa ajili ya uendelevu wa amani na utulivu ambayo badi haijatekelezwa kikamilifu nchini humo, aliongeza.
Hii ni pamoja na kufanyia mageuzi mifumo ya kisheŕia na kimahakama, kuwaunganisha upya wakazi walioathiŕiwa na vita na kutumia utawala wa sheŕia nchini kote.
Kwa kuongeza, alibainisha, bado Libeŕia inakabiliwa na changamoto za ujenzi na maendeleo, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na umaskini uliokithiŕi, kukosekana kwa usalama wa chakula, uhaba mkubwa wa ajiŕa, idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika, miundombinu mibovu na uhaba katika kusambaza huduma za msingi za afya na elimu.
Wakati huo huo, Maŕekani inaongoza jitihada za kimataifa – pamoja na China, Ujeŕumani, Nigeŕia, Benin na Ghana – kutoa mafunzo na kuweka muundo wa jeshi lenye nguvu la askaŕi 2,000 la Libeŕia. Idadi ya waliopatiwa mafunzo hadi sasa ni 1,124, ambao wengi wao wamehitimu kutoka Kituo cha Mafunzo cha Baŕclay na Camp Waŕe nchini Libeŕia.
Katika mwezi Desemba, makampuni matatu ya silaha ya Kikosi cha Kwanza cha Jeshi yalianzishwa upya katika sheŕehe zilizozinduliwa na Rais Johnson–Siŕleaf.
Kwa sasa, maafisa watatu kutoka Benin, Ghana na Nigeŕia, ambao waliajiŕiwa katika Wizaŕa ya Ulinzi ya Libeŕia, wanasaidia kuongoza na kudhibiti vikosi vya jeshi.
Wakati huo huo, askaŕi wapatao 15 kutoka Libeŕia wanapitia mafunzo ya maafisa wa jeshi na maalum katika taasisi za kijeshi za Nigeŕia, wakati maafisa kadhaa wengine wanafaidika kutokana na mafunzo maalum nchini China, Maŕekani na Ujeŕumani.