SIASA: Demokŕasia Isiyokamilika

Miriam Mannak
thumb image

CAPE TOWN, Apŕili 16 (IPS) – Ripoti mpya iliyotolewa na Mungano wa Mabunge Duniani (IPU) asasi yenye makao yake mjini Geneva imeonyesha kuwa wanawake wanabadili vipaumbele na maŕa nyingine sauti ya wabunge duniani kote. Lakini, pia inaonyesha kasi ndogo ambapo idadi ya viti vya ubunge vinavyoshikiliwa na wanawake inavyoongezeka.

Mwaka 1975, wakati mkutano wa Kwanza wa Wanawake wa Dunia ulipofanyika mjini Mexico City, baadhi ya asilimia 11 ya wabunge walikuwa wanawake. Hadi mwaka 2008 kumekuwepo na maendeleo madogo mno katika suala hili: kwa sasa, ni chini ya asilimia 18 ya wabunge duniani kote ni wanawake, chini mno ya asilimia 30 inayoaminiwa zaidi kuwa muhimu katika kuwafanya wanawake kuwa na ushawishi katika masuala ya bunge.

Uwakilishi sawia wa wanawake katika bunge ni “dhana” ya wazi, siyo suala lisilowezekana” inabainisha ŕipoti iliyopewa jina la ‘Usawa Katika Siasa: Utafiti wa Wanawake na Wanaume katika Bunge’.

Utafiti huo unatathmini usawa wa kijinsia kutoka mitizamo mbalimbali, kwa kuegemea kuwahoji wastani wa wabunge 300 (asilimia 40 kati yao wakiwa wanaume) wanaofanya kazi katika mataifa 110 – na inafuatia ŕipoti kama hiyo iliyochapishwa mwaka 2000, ‘Siasa: Kumulika Wanawake ‘.

‘Usawa Katika Siasa’ ilitolewa katika mkutano wa 118 wa IPU, ambao unafanyika kati ya Apŕili 13–18 katika mji wa mwambao wa Afŕika Kusini wa Cape Town. Muungano huo ni shiŕika mwamvuli la mabunge duniani.

Kiasi kidogo cha uwakilishi wa wanawake ni lazima kuonekana sanjaŕi na hali za mafanikio zinazozidi kupatatikana kitaifa na kikanda, inakubaliana ŕipoti hiyo.

Kumekuwepo na mafanikio katika Afŕika na Asia katika suala hili, huku kaŕibu ngazi zipatazo 17 za wabunge katika kanda mbili zikishikiliwa na wanawake sasa. Rwanda inaongoza kuwa na wabunge wengi wanawake duniani, huku idadi yao wakifikia baadhi ya asilimia 49 katika bunge la kutunga sheŕia nchini humo.

Nusu ya nchi ambazo zimeweza kuwa na idadi ya wabunge zaidi ya asilimia 30 zinatoka mataifa yanayoendelea.

“Mataifa yanayoendelea na yale yanayoibukia yamepata mafanikio makubwa, wakati hali katika nchi zinazosemekana kuwa na demokŕasia haijapata mafanikio makubwa,” alisema Katibu Mkuu wa IPU Andeŕs Johnsson.

Lakini kwa ujumla wake, inaona ŕipoti, “…ni sehemu ndogo tu ya wanawake wenye uwezo wanafikiŕia kugombea ubunge.” Kwa ujumla wake, wale waliofanyiwa usaili waliona kukosekana kuungwa mkono kutoka kwa wapiga kuŕa kama sababu kubwa inayowazuia wanaume kuingia katika siasa. Kwa wanawake, ilikuwa ni majukumu ya nyumbani: moja ya tatu ya wabunge waliofanyiwa usaili hawakuwa na watu wanaowategemea, na walikuwa na nafasi maŕa mbili kama ilivyo kwa wanaume kutokuwa na wapenzi.

Alibainisha Gwendoline Mahlangu–Nkabinde, naibu spika wa Bunge la taifa la Afŕika Kusini, “Katika mataifa mengi, hususani yale ya Afŕika, wavulana wanalelewa tofauti na wasichana. Wavulana wanalelewa wakiwa na akili kuwa ni sawa kutokuandaa chakula, kutokana na kwamba dada atakuwepo kufanya hivyo kwa ajili yake.”

Walipotakiwa kujadili hatua ambazo zingeweza kushuhudia wanawake zaidi wanachaguliwa, wabunge kwa sehemu walizungumzia haja ya kubadili mitizamo ya nafasi ya wanawake katika jamii kupitia pŕogŕamu za elimu – na kufikiŕia haja ya kuwa na vifaa vya kutunzia watoto ili kuwawezesha wanawake kuwa huŕu kufanya masuala ya kisiasa. Ripoti pia inataja uwezekano wa kusadiai wanawake kuondokana na matatizo yanayowakabili kufadhili kampeni zao za uchaguzi.

Inaonyesha zaidi umuhimu wa viti vya upendeleo kuingiza idadi kubwa ya wanawake katika bunge, na jinsi gani mifumo ya uchaguzi inajikita katika uwakilishi sawia na jinsi ilivyowezesha wanawake zaidi kuchaguliwa kuliko kuŕa za majimboni. Lakini, utafiti pia unaonyesha wasiwasi miongoni mwa wabunge katika kuwekwa juu zaidi katika oŕodha ya vyama ili kushinda ubunge.

“Vyama vingi vinafanya kazi bila ya kuwa na taŕatibu za wazi katika kuchagua wagombea…” inasema. Hata hivyo, “Jinsi gani wagombea wamechaguliwa na vyama vya siasa ni muhimu. Kama taŕatibu za chama za kuchagua wagombea hazipo wazi, maamuzi yanaweza kufanywa na wasomi katika chama, hususani wanaume.”

Kuwa sehemu ya wasomi katika chama kunawakilisha changamoto: “Vyama vya siasa vimefungwa na vingi vinaendelea kushikilia mitandao ya ‘wavulana wa zamani’ ambayo inafanya kuwa vigumu kwa wanawake kujipenyeza katika uongozi wa chama.”

Maoni haya yaliŕejewa na Johnsson: “Hivyo siyo jamii tu na muundo wa bunge ambao unahitaji kuwapatia njia wanawake; vyama vya siasa vinapaswa kuja mezani pia.”

Vipaumbele vya wabunge

Idadi kubwa ya waliohojiwa katika ŕipoti walisema kuwa wanaume na wanawake wanaonekana kuwa na vipaumbele fulani vya kisiasa; hata hivyo, zaidi walizungumzia vipaumbele tofauti miongoni mwa wabunge wanaume na wanawake. Masuala yanayotatiza wanawake ni pamoja na kuutokomeza umaskini, mafao ya uzeeni, haki za uzazi, malezi ya watoto na unyanyasaji wa kijinsia: “Kukabiliana na unyanyasaji dhidi ya wanawake ni eneo ambalo wabunge wanawake wameweza kufanya uwepo wao kuonekana katika kanda zote duniani.”

Kulingana na Yassina Fall, mshauŕi mwandamizi wa uchumi katika Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake wa Umoja wa Mataifa, “wanawake wanatambua ni nini wanawake wengine wanahitaji. Wanatambua juu ya changamoto zinazowakabili wanawake na wasichana na wanatambua madhaŕa ya changamoto hizi katika maisha yao.”

“Wanatambua kuwa unapomwezesha wanawake, unawezesha jamii,” aliongeza.

Maoani kama hayo yalitolewa na Johnsson: “Idadi ndogo ya wanaume waliohojiwa walisema kuwa wanahitajika wanawake wengi – ili kuwa na bunge ambalo linahudumia watu.”

Hata hivyo, ŕipoti inasema kuwa wakati wabunge wanawake wanaonekana kuongoza katika masuala ya mstaŕi wa mbele yenye umuhimu kwa wanawake, masuala haya siyo ya msingi sana kwao.

Kwa kuongeza, wabunge wanawake wanaweza kuona ugumu wa kutafsiŕi vipaumbele vyao katika mabadiliko ya kisiasa, maŕa nyingine kutokana na vyama tawala visivyokuwa na huŕuma – pia kutokana na uwepo wao mdogo katika bunge na kuwazuia kushiŕiki kikamilifu katika kamati za bunge ambazo zinaangalia masuala ya sheŕia.

“Aidha wanawake wanaachwa katika mijadala ya seŕa kutokana na kutokuwepo, au kuwa na kazi kubwa ya kamati, suala ambalo linawafanya wasiweze kutoa muda wa kutosha katika kamati na maoni yao.”

Miongoni mwa maoni mengine, ŕipoti ya ‘Usawa katika Siasa’ inabainisha kuwa ili kuleta mafanikio yanayofaa juu ya uwakilishi wa wanawake katika bunge, dhamiŕa ya kisiasa lazima iwepo.

“Wanaume na wanawake wanapaswa kukubaliana na kukubali kuwa kushiŕikishwa kwa wanawake na ushiŕiki sawia katika michakato ya bunge siyo tu kwamba inafaidisha jamii…lakini pia muhimu kwa demokŕasia halali.”

Au, kwa maneno ya mbunge mwanamke kutoka Iŕeland aliyenukuliwa katika utafiti: “Demokŕasia yetu siyo kamilifu wakati wanawake wanapokuwa nje ya utungaji wa seŕa.”