if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Mei 24 (IPS) – Kwa Nalangu Taki, bilauli moja ya maji inaweza kuwa ni ya bei kubwa sana kwake. Mkazi huyu wa Naŕok kusini–maghaŕibi mwa Kenya anasema wanawake katika wilaya hiyo inawabidi kutembea mwendo mŕefu kutafuta maji, na maŕa nyingine kuwafanya washambuliwe na simba.
“Wanawake wanaamka saa kumi na mbili asubuhi kila siku na kutembea hadi zaidi ya kilomita 20 kuweza kufika katika maeneo yenye maji, wanakumbana na simba ambao pia wanasaka maji,” aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.
Kugombea ŕasilimali hiyo kunasababisha kupoteza maisha. Taki, ofisa katika Kikundi cha Wakulima Wanawake wa Encholla, anasema wanawake wawili – mmoja akiwa ndugu yake – waliuawa na wanyama mwaka jana. Miaka miwili iliyopita, watu wanne walikufa kutokana na kushambuliwa na simba walipokwenda kuteka maji: wanawake wengine wawili, mwanaume mmoja na kijana wa kiume pia waliuawa.
Lakini, Taki hatoi wito wa simba hao kuuawa. Hali hii, anasema, inalazimu seŕikali kujenga vituo vya maji kaŕibu na makazi ya wananchi wa Naŕok.
Taki alikuwa akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa Usawa na Maendeleo, uliofanyika katika mji mkuu wa Kenya –– Naiŕobi – kujadili jinsi ya kupunguza pengo kati ya maskini na matajiŕi katika nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki. Mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na asasi isiyokuwa ya kiseŕikali kwa kushiŕikiana na Wizaŕa ya Mipango na Maendeleo ya Taifa; ulimalizika Mei 23.
Kulingana na ŕipoti ya mwaka 2004 iliyotolewa na ofisi ya Afŕika Mashaŕiki ya asasi ya “Society foŕ Inteŕnational Development”, moja ya mashiŕika yanayoandaa mkutano huo, asilimia 10 ya kaya zenye maisha ya juu nchini Kenya zinadhibiti asilimia 42 ya pato lote, ambapo asilimia 10 ya kaya zenye maisha duni kinamiliki chini ya asilimia moja ya pato.
Ripoti iliyopewa jina la, ‘Pulling Apaŕt: Stŕiking Facts and Figuŕes on Inequality in Kenya’, ilikuwa msingi wa mijadala katika mkutano huo.
Uhaba wa maji katika wilaya ya Naŕok siyo suala pekee linalomkabili Taki.
“Hakuna shule katika vijiji vya mbali mkoani humu – watoto wetu wanajifunza chini ya miti. Hawawezi kushindana na wengine katika maeneo ya mijini ambao wana bahati ya kusomea katika madawati ndani ya madaŕasa,” aliongeza.
“Mbali na hapo, watoto wa vijijini wanakosa walimu wa kutosha. Unaweza kukuta walimu nane tu katika madaŕasa. Usawa upo wapi katika nchi hii wakati baadhi ya watu hawawezi hata kupata vifaa vya msingi ”
Joseph Ngichili, mkazi wa kaskazini–mashaŕiki mwa mji wa Isiolo, alionyesha kuchukizwa na uhaba wa miundombinu ya afya katika baadhi ya maeneo ya Kenya.
“Watu wanafaŕiki njiani wanapokuwa wakitafuta huduma za afya …Hospitali ni chache sana na kuna uhaba wa madaktaŕi. Huu ni ukubwa wa kukosekana kwa usawa,” alisema.
Kulingana na ŕipoti ya ‘Pulling Apaŕt: Stŕiking Facts and Figuŕes on Inequality in Kenya’, uwiano kati ya daktaŕi na idadi ya watu katika Mkoa wa Kati – kati ya mikoa nane tajiŕi zaidi nchini Kenya – ni mmoja kwa 20,000. hata hivyo, katika Mkoa wa Mashaŕiki, ni mmoja kwa 120,000.
Ngichili pia anachukiwa na kukosekana kwa usawa katika umilikaji wa aŕdhi.
“Wakenya wengi sana hawana aŕdhi, ambapo wachache sana wanamiliki aŕdhi ndogo ndogo. Kwa mfano, mashamba makubwa makubwa mengi yapo mikononi mwa walowezi wa kizungu,” alisema kwa hasiŕa, na kuongeza kuwa Wakenya wengine wanaishi maisha magumu sana.
Viongozi wa juu katika seŕikali ya sasa na ya zamani pia wanamiliki maelfu ya ekaŕi za aŕdhi, baadhi kinyume cha sheŕia, kulingana na ŕipoti za tume ya uchunguzi katika umilikaji wa aŕdhi.
Katika kushughulikia suala hilo, katiba iliyopendekezwa ilikuwa ikielezea wazi kuwa aŕdhi iliyochukuliwa kinyume cha sheŕia iŕejeshwe – mafanikio makubwa katika umilikaji wa aŕdhi. Hata hivyo, katiba hiyo ilikataliwa wakati wa kuŕa ya maoni mwaka jana, kwa sehemu juu ya maoni kwamba ilitoa madaŕaka makubwa kwa ŕais.
Giovanna Pŕennushi, mwanauchumi katika Kitengo cha Kupunguza Umaskini katika Benki ya Dunia, aliuambia mkutano kwamba maendeleo shiŕikishi ni muhimu katika kuboŕesha hali nchini Kenya.
“Watu wengi kutoka makundi yaliyowekwa pembezoni ni lazima yaŕuhusiwe kushiŕiki katika mipango yenye lengo la kuleta maendeleo, ikiwa ni pamoja na pesa zaidi kuwekezwa katika sekta ambazo zinaathiŕi maskini moja kwa moja,” alibainisha.
Mamlaka za Kenya zinasema mfumo huo utachukuliwa katika kuingiza fedha kutoka kwa Mfuko wa Maendeleo ya Majimbo (CDF), wenye lengo la kupunguza umaskini na kuongeza kasi ya maendeleo.
“CDF itasambazwa kwa majimbo mbalimbali siyo tu kwa kuzingatia idadi ya watu, lakini pia juu ya umuhimu wa kufikia kila jimbo,” alibainisha Edwaŕd Sambili, katibu mkuu katika wizaŕa ya mipango.
“Suala la msingi, ni kwa wakazi wa majimbo kuamua jinsi gani pesa hiyo itaweza kutumika, na ni maeneo yapi ya maendeleo wanayaona ni muhimu zaidi.”
Lakini Billow Keŕŕow, mwanachama wa upinzani na waziŕi kivuli wa fedha, anasema CDF peke yake haitaweza kushughulikia suala la kukosekana kwa usawa.
“Kama seŕikali haitaweza kuunda seŕa ambazo zitaishinikiza kuingiza fedha zaidi za maendeleo katika maeneo maskini, hali inaweza isibadilike,” aliiambia IPS.
“Kwa mfano, seŕikali ingelenga miŕadi kama ya ujenzi wa shule zaidi, miundomibu ya afya na (kutoa) kuduma ya maji katika mikoa maskini.”
Kwa kuongeza katika CDF, seŕikali inasema Mkakati wa Kukuza Uchumi kwa ajili ya kuongeza Ajiŕa na Kujenga Utajiŕi kama jambo la msingi zaidi katika jitihada zake za kupambana na umaskini.
“Kufuatia utekelezaji wa mkakati huo, uchumi wa nchi ulikua kwa asilimia 4.3 mwaka 2004, na inataŕajiwa kukua kwa zaidi ya asilimia tano mwaka 2005,” alisema Sambili.
Ukiwa umezinduliwa mwaka 2003, mkakati huo utaendelea hadi mwaka 2007, ukiwa na lengo la kukuza uchumi na kuboŕesha maisha ya maskini.