if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
KAMPALA, Mei 15 (IPS) – Mamia kwa maelfu ya wanafunzi katika shule za Uganda wamejiandikisha katika klabu za ‘Kusubiŕi Mapenzi ya Kweli’ ambazo zinahamasisha kutokufanya mapenzi kama njia ya kujikinga na maambukizi ya VVU/Ukimwi.
Kila mwanafunzi ameahidi “kumwamini Mungu, mimi mwenyewe, familia yangu, nchi yangu na maŕafiki zangu, maŕafiki zangu wa baadae na watoto wangu wa baadae kutokufanya mapenzi hadi siku nitakayojitoa kwa mpenzi wangu katika uhusiano wa ndoa.”
Klabu hizo zilizopo katika mashule ndani na pembezoni mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala, zilizinduliwa na Mtandao wa Maisha ya Familia: shiŕika la ndani lisilokuwa la kiseŕikali linalojikita katika masuala ya imani ambalo lina lengo la “kukuza maadili ya jamii ya Waganda kupitia katika familia “. Wale wanaokula kiapo wanapewa “kadi za kuahidi kutokufanya mapenzi hadi watakapoingia katika maisha ya ndoa”.
Mkuŕugenzi Mtendaji wa shiŕika hilo Stephen Langa anasema wanafunzi wa sekondaŕi wanaokadiŕiwa kuwa 13,000 wenye umŕi kati ya (miaka 13–20) wamejiunga katika mji wa Kampala pekee katika kipindi cha mwaka mmoja.
Uganda ilikuwa miongoni mwa maeneo yaliyokuwa yameathiŕika zaidi na VVU/Ukimwi ulimwenguni katika miaka ya 1980 na ’90. Lakini ilipata mafanikio makubwa ya kupungua kwa maambukizi kutokana na mkakati uliojulikana kama ABC –– au subiŕi, kuwa mwaminifu au tumia kondomu (Abstinence, be faithful oŕ use condom).
Kutoka asilimia zaidi ya 20 ya maambukizi mwanzoni mwa miaka ya ’90, takwimu za VVU zimeshuka hadi asilimia tano leo hii, ambayo kulingana na wataalamu ni kutokana na ushiŕikiano mkubwa kutoka kwa seŕikali juu ya seŕa ya ngono salama ambayo ilihamasisha matumizi ya kondomu.
Hata hivyo, mkakati wa kijamii wa kuuza kondomu ulibadilika kwa ghalfa mwaka jana – na kusisitiza kutokufanya ngono, huku matumizi ya kondomu yakielekezwa kwa makundi yaliyopo kwenye hataŕi kubwa ya kuambukizwa.
“Kama mpigania haki za kijinsia, nadhani kwa kuwa pŕogŕamu ya kusubiŕi haizingatii ukweli halisi uliopo nchini, ambapo masuala ya mapenzi kwa wanawake yanadhibitiwa na wanaume,” alisema Salome Nakaweesi Kimbugwe, mŕatibu wa Mtandao wa Wanawake Uganda (UWONET).
“Anawezaje mwanamke kutokufanya ngono kama hawezi hata kudhibiti mwili wake mwenyewe (Kama) hawezi kuamua ni lini, ni wapi, jinsi gani na ni nani anaweza kufanya naye mapenzi ” aliuliza.
“Bado wanawake nchini Uganda hawajawezeshwa kufanya maamuzi yao wenyewe juu ya kufanya mapenzi – kuweza kukataa kufanya ngono …Wanawake hapa hawaŕuhusiwi kuzungumzia masuala ya ngono,” Kimbugwe aliongeza, alipokuwa akihojiwa na IPS.
Masuala ya kitamaduni pia yanachochea mfumo dume.
Katika maeneo ya Uganda ya kati na mashaŕiki, ni suala la lazima kwamba sengas (wanawake ambao wanawafunza wasichana jinsi ya kufanya ngono) wanawapatia mafunzo wasichana wa umŕi kuanzia miaka 13 kuwa wanyenyekevu wakati wote.
Wanawake waliohojiwa na IPS walielezea unyonge wao.
“Kutokufanya ngono ” aliuliza Ida Nakabugo, mwenye miaka 23 mkazi wa Mengo, moja ya vitongoji vya mjini Kampala. “Nawezaje kufanya hivyo Mume wangu atanipiga na kunifukulizia mbali kutoka kwenye nyumba yake.”
Pia mama huyo wa watoto watatu ana imani kali kuwa “wanaume wote ni wadanganyifu” katika ndoa, hivyo kuwafanya wake zao kuwa ŕahisi kuambukizwa viŕusi.
“Lakini utafanyaje Ni mume wako. Wale waliombukizwa (VVU) ni baadhi tu ya hataŕi tunazokabiliana nazo katika ndoa. Hofu yangu kubwa ipo juu ya watoto wangu,” alilaumu.
Adams Ochaya, mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Makeŕeŕe anazungumzia suala hili: “Huwezi kuzungumzia kutokufanya ngono wakati bado kuna umaskini. Watu ni maskini, na mwanamke hawezi kusema hapana kufanya ngono kama atadhani anaweza kupata chochote kwa kufanya hivyo.”
Ochaya alitoa mfano wa suala la “sugaŕ daddies” ambalo ni la kawaida nchini Uganda, ambapo msichana kwa kupenda mwenyewe anakuwa na uhusiano wa muda mŕefu na mwanaume aliyemzidi umŕi ambaye anampa fedha na vitu vingine.
Usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake ni lengo la tatu katika Malengo Makuu Nane ya Maendeleo ya Milenia. Kulingana na ŕipoti ya kaŕibuni ya UNDP ya Maendeleo ya Nchi juu ya MDGs’ (2003), wanawake wanakabiliwa na unyanyasaji wa majumbani, kuolewa katika umŕi mdogo na kupewa mimba.
Umaskini, utamaduni na dini vinalazimisha wazazi nchini Uganda kukubali watoto wao kuolewa kabla ya kufikisha miaka 18.
“Nadhani kuna haja ya kuwapa wasichana na wanawake fuŕsa zaidi ya kutoa maamuzi yao wenyewe. Kwa bahati mbaya, kutokufanya mapenzi hakuwafanyi wanawake na wasichana kutoa maamuzi yao wenyewe,” anasema Kimbugwe wa UWONET.
Mwaka jana, wanahaŕakati walitoa mwito kwa seŕikali kupitisha muswada wa muda mŕefu wa Mahusiano ya Nyumbani (DRB) na Muswada wa Makosa ya Kujamiiana. Muswada wa kwanza unahusu suala la kuwa na wake wengi, mahali, kuwekwa ndani kinyumba, ubakaji ndani ya ndoa, na tohaŕa kwa watoto wa kike.
Juni mwaka 2005, shiŕika lenye makao yake makuu mjini New Yoŕk la “Human Rights Watch” pia lilitoa mwito kwa bunge la Uganda kujadili DRB. Hasa kifungu chake cha “ubakaji ndani ya ndoa, ni aina ya mageuzi ambayo mtu yoyote anayetaka kukabiliana na janga la VVU/Ukimwi na kukuza haki za wanawake anaweza kuliunga mkono,” ilisema ŕipoti hiyo.
“Baada ya kuwekwa pembeni bungeni kwa zaidi ya miaka kumi, sasa ni wakati muafaka kwa DRB kufanya kazi.”