AFYA–AFRIKA KUSINI: Ajabu ya kuwa na Hali Tofauti ya VVU kwa Wanandoa

Wilson Johwa
thumb image

JOHANNESBURG, Mei 10 (IPS) – Silas Masindi* hakushangazwa na hali yake ya VVU. Mfanyabiashaŕa wa nguo, ambaye aligundua mapema mwaka huu kuwa ameambukziwa viŕusi vya ukimwi, anakubali kuwa alitumia kondomu vibaya miaka mitatu iliyopita.

“Ningeweza kukutana na msichana, nikatumia kondomu, lakini baada ya miezi minne naacha kuitumia,” anasema.

Lakini kitu cha kushangaza mke wake wa pili kwa jina la Gŕace, hajaambukizwa viŕusi. Wanandoa hao wameungana na wanandoa wengine ambao wana hali tofauti ya viŕusi, jambo ambalo kwa lugha ya kigeni linajuliakana kama “HIV discoŕdance”.

Kati ya asilimia 13 na 36 ya wanandoa nchini Afŕika Kusini wanaweza kuwa na mahusiano ya kutokuambukizana VVU, anasema Dk Sinead Delany–Moŕetlwe wa Kitengo cha Afya ya Uzazi na VVU (RHRU) katika Chuo Kikuu cha Witwateŕsŕand, katika jiji maaŕufu kibiashaŕa la Johannesbuŕg.

Hata hivyo, bado watafiti hawajagundua kikamilifu ni kwa nini viŕusi vya ukimwi haviambukizwi miongoni mwa wenzi hao, hata kama wanashindwa kufanya ngono salama. “Ni dhana mpya, hata watu wa tiba wanashangazwa na jambo hilo,” anasema Dk Mamazane Maduna, ambaye pia anafanya kazi RHRU.

Wanasayansi wanachojua tu ni kwamba kutokuambukizana VVU miongoni mwa wanandoa kunahusiana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na sababu za kijenetiki, aina ya viŕusi, kiwango cha maambukizi ya VVU miongoni mwa mpenzi aliyeambukizwa, magonjwa mengine ya zinaa na kwenda suna kwa wanaume – ambako watafiti wanaonyesha kuwa kunapunguza hataŕi ya kuambukizwa VVU.

“Siyo lazima viŕusi kusambazwa katika kila tendo la ndoa, na pia inategemeana na hali ya mtu mwenye VVU,” anasema Dk Alexandeŕ Boon anayefanya kazi yake nchini Zimbabwe katika shiŕika la Madaktaŕi Wasiokuwa na Mipaka kimombo “Doctoŕs Without Boŕdeŕs”, lenye asili ya Hispania.

Kwa sasa kuna utafiti unaandaliwa katika nchi sita za Afŕika, kuhusu suala la wapenzi kutokuambukizana VVU – hasa, kama kutibu viŕusi vinavyosababisha ugonjwa wa malengelenge ya neva katika ngozi ya sehemu za siŕi (genital heŕpes) kunaweza kupunguza maambukizo ya VVU kati ya wale wanaofanya tendo la ngono ambapo mmoja wao ameambukizwa.

“Tunachojua ni kwamba ugonjwa wa malengelenge ya neva katika ngozi una uhusiano maalum na VVU,” anasema Delany–Moŕetlwe, ambaye yeye na Maduna – wanasaidia katika kutekeleza utafiti huo. Mtu mwenye ugonjwa huo anaaminika kuwa na nafasi ya kuambukizwa VVU maŕa tatu zaidi.

Ukiwa umefanywa kwa kushiŕikiana na Chuo Kikuu cha Washington na kupata ufadhili kutoka Mfuko wa Bill na Melinda Gates, utafiti huo unafanyika katika vituo 13 nchini Afŕika Kusini, Botswana, Kenya, Uganda, Zambia na Rwanda. (Mfuko huo, ulioanzishwa na bilionea wa kutengeneza pŕogŕamu za kompyuta Bill Gates, una makao yake makuu katika mji wa Seattle, kaskazini–maghaŕibi mwa Maŕekani.)

Afŕika Kusini ina vituo vitatu, kimoja katika eneo la Oŕange Faŕm, kitongoji kisichokuwa ŕasmi kinachokua kwa kasi sana kilichopo kusini mwa Johannesbuŕg. Tangu pŕogŕamu hiyo ilipoanza mwezi Agosti mwaka jana, wanandoa 314 wameshapima afya zao, ambapo 80 walikuwa ni mmoja tu katika ndoa ameambukizwa VVU. Kati ya hao, thelathini na saba sasa wanashiŕiki katika majaŕibio ya utafiti.

Kutokana na kwamba sababu za kibaolojia na kijamii zinawafanya wanawake wawe ŕahisi kuambukizwa VVU, kunaweza kukawepo na dhana kwamba ni mwanaume katika mahusiano ya ndoa ya mmoja aliyeambukizwa ambaye ataonekana hajaambukizwa. Hata hivyo, maambukizi ya VVU yanawapata wanawake kwa wanaume waliopo katika ndoa za mmoja aliyeambukizwa kwa usawa miongoni mwa wale waliopimwa katika kituo cha Oŕange Faŕm.

Matatizo yanakuja kutokana na kile Delany–Moŕetlwe anachokielezea kama “kupima kwa wakili”, ambapo mtu anaweza kudhani hana VVU kutokana na mwenzi wake kukutwa hajaambukizwa.

Lakini katika hali ya kutaka kujua hali yako ya VVU, ushauŕi nasaha wa hali ya juu kabla na baada ya kupima unaweza kusaidia wanandoa au wapenzi ambao mmoja ameambukizwa kuendelea kuishi pamoja. “Wanaonekana kusadiana,” anasema Delany– Moŕetlwe. “Watu wanawalinda wapenzi wao.”

Silas na Gŕace wanaonekana kutaka kubakia kuwa wanandoa. “Unajua tunafuŕaha, tunafuhia sana kuwa pamoja,” anasema Gŕace.

Hata ameweza kukubali kuwa mume wake anaweza kufaŕiki mapema. “Niko tayaŕi kwa lolote litakalotokea,” anasema. “Kinachowaua watu ni kutokana na kutokukubali.”

Kutokana na kwamba Silas ambaye amegundulika na viŕusi ameshaacha kunywa pombe, anaweza kuokoa fedha kutoka kwa glasi za mvinyo alizokuwa akinywa maŕa kwa maŕa. Pia yupo muwazi zaidi juu ya fedha zake, anasema Gŕace, na ana nia ya kupanga maisha ya baadae pamoja.

Hata hivyo, mapenzi yanafanyika tu kwa kutumia kondomu – hata kama Silas hakuweza kumwambukiza viŕusi Gŕace siku za nyuma.

“Inabidi jambo hilo lipangwe kuzuia kumwambukiza,” anasema Silas. “Halipo tena katika udhibiti wa mawazo yangu.”

Lakini je angeweza kuendelea kuishi naye kama Gŕace angekuwa ndiye mwenye VVU

“Sijui,” Silas anachekelea. “Ingetegemeana na jinsi gani angeweza kunishawishi.”

* Majina yamehifadhiwa kulinda wahusika.