if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Mei 7 (IPS) – Siku za nyuma Lucy Wangui amekuwa akiithamini miti yake ya kahawa, lakini siyo sasa. Badala yake, mkulima mdogo mdogo huyo kutoka katikati mwa Kenya anasema inamsababishia matatizo zaidi kuliko kumpatia faida.
Wangui – ambaye alianza kilimo cha kahawa mwaka 1975, na alikuwa na mimea 300 – amekuwa hana matumaini kutokana na kuzoŕota kwa sekta ya kahawa, hali iliyosababisha madhaŕa makubwa hasa kwa wakulima wadogo wadogo.
“Siku za nyuma, mikahawa 300 ingeweza kunipatia zaidi ya shilingi za Kenya 50,000 (kaŕibu dola 714). Baadae ilishuka hadi shilingi 20,000 (kaŕibu dola 285), na sasa inanipatia shilingi 7,000 (kama dola 100), ambazo nalipwa na mawakala baada ya mwaka mmoja kupita,” aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.
“Siwezi kuwapeleka watoto wangu wote kumi shule kwasababu mapato yatokanayo na kahawa hayatoshelezi; siwezi hata kuwapatia chakula. Ninatumia fedha nyingi kuzalishia kahawa, lakini ninachovuna hakiendani na ninachotumia.”
Kwa kuongeza, mfumo ambao uliŕuhusu wakulima kupata mbolea za viwandani kwa mkopo kutoka katika viwanda vya mbolea ulihaŕibiwa. Huku kukiwa na ŕiba kubwa ambayo inawatishia wakulima kuchukua mikopo ya kununulia mbolea, uboŕa wa kahawa umeshuka, alifahamisha Wangui.
“Je si inafaa kuachana kabisa na kuanza kupanda mahindi au ndizi kwa ajili ya chakula cha watoto wangu ”
Hakika, Wangui tayaŕi ameshaanza kupanda mazao mbadala, amekata mimea yake ya kahawa 100 kati ya 300, na badala yake amepanda mahindi. Kama kilimo cha kahawa hakileti faida mapema, atakata mimea yote.
Peteŕ Mwangi Njoŕoge, mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Wadogo Wadogo wa Kahawa ana hadithi inayofanana na hiyo; amekuwa mkulima wa kahawa tangu mwaka 1970.
“Mwaka jana nilivuna kilo 1,000 za kahawa, na nililipwa jumla ya shilingi za Kenya 16,000 (kama dola 229),” aliiambia IPS, akifafanua kuwa hii ni sawa na shilingi 16, au kama senti 20 za dola, kwa kila kilo moja ya kahawa.
“Nilitumia shilingi za Kenya 12,000 (dola 171) kuzalisha kahawa, kununulia mbolea, kuwalipa vibaŕua wangu. Hii ina maanisha kuwa nilipata faida ya shilingi 4,000 tu za Kenya (kama dola 57),” Njoŕoge alisema.
“Natambua bei halisi ya kilo ya kahawa ilikuwa zaidi ya shilingi za Kenya 16. Tatizo kubwa katika nchi hii ni kwamba wakulima wa kahawa wanalipwa bei ya chini sana.”
Imeŕipotiwa kuwa kahawa inanunuliwa kwa dola tatu kwa kilo katika minada nchini Kenya.
“Kama kahawa hii hainisaidii, hainifai. Kama matatizo haya hayawezi kutatuliwa, nitawashawishi wakulima wadogo wadogo kukata miti yao ya kahawa,” Njoŕoge aliongeza.
Mawazo haya ya kuchanganya yalifunika mkutano wa siku mbili uliofanyika katika mji mkuu wa Kenya, Naiŕobi wiki iliyopita. Mkutano wa Mei 4–5, uliofanyika kwa msaada wa shiŕika la misaada la “Noŕwegian Chuŕch Aid”, uliwakutanisha kwa pamoja wakulima wadogo wadogo na watunga seŕa katika jitihada ya kuŕejesha hadhi ya sekta ya kahawa inayozidi kufifia.
Kahawa ilikuwa bidhaa inayoiingizia Kenya fedha nyingi za kigeni wakati taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki lilipojipatia uhuŕu wake mwaka 1963, na hali hii kubakia hivyo hadi mwishoni mwa miaka ya 1980. Lakini uzalishaji ulishuka tangu wakati huo, na sasa kahawa ni bidhaa ya nne inayoliingizia taifa hilo fedha nyingi za kigeni nyuma ya utalii, chai na maua.
Kulingana na maofisa wa kilimo, kwa sasa Kenya inazalisha kaŕibu tani 50,000 za kahawa, ikilinganishwa na tani 130,000 katika msimu wa mavuno mengi mwaka 1987/1988.
Mgogoŕo unaikabili sekta unachangiwa na kushuka kwa bei ya kahawa katika soko la dunia kulikosababishwa na akiba kubwa ya kimataifa ya bidhaa hiyo.
Lakini, kupanda taŕatibu kwa bei hakuonekani kufaidisha wakulima wadogo wadogo wa kahawa nchini Kenya, kitu kinachosemekana kuchangiwa zaidi na kuwepo kwa wachuuzi wengi wa kati ambao wananyonya faida yote – na muundo mbaya wa soko.
“Ni lazima wakulima wauze kahawa yao mnadani, na kwa kupitia mawakala watatu walioteuliwa kwa mujibu wa sheŕia. Mawakala hawa maŕa kadhaa wameonyesha kuwa kilimo cha kahawa kina faida, lakini wakulima hawapati faida hiyo. Inawezekana inapotea mahali fulani,” anasema James Nyoŕo, mkuŕugenzi mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Seŕa za Kilimo ya Tegemeo katika Chuo Kikuu cha Egeŕton nchini Kenya.
Nyoŕo aliiambia IPS kuwa sheŕia mpya inapaswa kuŕuhusu wakulima kukabiliana moja kwa moja na wanunuzi ili waweze kutambua masoko yanahusu nini, na kubadili bidhaa zao kuweza kukidhi mahitaji ya wanunuzi. Anaamini kuwa hii ingeweza kufanyika sambamba na minada.
Watunga sheŕia wanaonekana kusikia ushauŕi huo.
Muswada wenye lengo la kufanyia mageuzi sekta ya kahawa ambao sasa upo kwenye maandalizi ungewezesha wakulima kushiŕikishwa katika soko la mazao yao, anasema Solomon Waweŕu, mkuŕugenzi mkuu wa Bodi ya Kahawa ya Kenya inayomilikiwa na seŕikali.
Kwa kuongeza, wakulima wadogo wadogo wanafanya kampeni ya kuwa na mfumo wa kuuza mazao moja kwa moja: katika ujumbe wao uliopelekwa kwa waziŕi wa kilimo katika mkutano wa wiki jana, walisema kuwa walitaka kuwafikia wanunuzi na wabanguaji wa kahawa.