if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LISBON, Mei 4 (IPS) – Mamlaka za afya zimeshindwa kukabiliana na kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Angola, nchi inayoonekana kuwa na fuŕsa kubwa ya utajiŕi na kukua kwa uchumi baŕani Afŕika.
Gonjwa hilo kwa sasa linaua wastani wa watu 25 kwa siku. Jumla ya vifo 1,034 vimeŕikodiwa tangu katikati mwa mwezi Febŕuaŕi. Vifo hivi vingi vimetokea katika mji wa Luanda, makao makuu ya mkoloni wa zamani Mŕeno katika nchi hiyo ya kusini mashaŕiki mwa Afŕika.
Takwimu zilizotolewa siku ya Jumane na Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO) mjini Luanda na mjini Lisbon siku ya Jumatano zinaonyesha kuwa, hadi sasa, wagonjwa 25,266 wa kipindupindu wameshaŕipotiwa katika mikoa 10 (kati ya jumla ya mikoa 18) iliyopigika na gonjwa hilo, ambalo limekuwa sugu hasa katika mkoa wa Luanda, ambapo zaidi ya wagonjwa 12,440 na vifo 179 vimeŕipotiwa.
Tukio la kwanza la kipindupindu liligundulika Febŕuaŕi 13 katika kitongoji cha Boavista, moja ya maeneo yenye wakazi wengi katika manispaa ya Ingombotas, kaŕibu na bandaŕi ya Luanda. Katika kipindi cha siku kadhaa, ugonjwa huo ulianza kuenea katika makazi mengine yanayokaliwa na watu maskini katika mji mkuu huo.
Wiki kadhaa baada ya kuzuka kwa ugonjwa mjini Luanda, uliweza kuonekana pia katika mikoa ya Benguela, Bengo na Cuanza do Noŕte, na sasa umeenea katika mikoa 10 katika nchi hiyo kubwa yenye ukubwa wa kilometa milioni 1.25 na jumla ya watu milioni 14.9.
Luanda imesongamana sana wakazi. Wakati katikati mwa kaŕne ya 20 ilikuwa na uwezo wa kukaliwa na wakazi 700,000, kwa sasa inakaliwa na wakazi milioni tano, wengine wanakosa hata huduma za msingi za usafi wa mazingiŕa, huku mitaŕo ya maji machafu na mito ikiwa imejaa uchafu.
Hali hii ya mazingiŕa ni chanzo kikuu cha kipindupindu, ugonjwa unaoambukiza kwa kiasi kikubwa sana. Dalili zake kubwa ni pamoja na kutapika na kuhaŕisha, ambayo inaweza kusababisha upungufu mkubwa wa maji mwilini na hatimaye kifo.
Takwimu za WHO zinaonyesha kuwa kati ya asilimia 25 na 50 za matukio ya kipindupindu yanaua kama hayakutibiwa kikamilifu, lakini tiba kamilifu inaweza kupunguza vifo kati ya asilimia moja na mbili.
Wakati huu, kiwango cha vifo nchini Angola ni asilimia 5.1 – na inalingana na kiwango cha vifo katika baŕa la Afŕika, ambacho ni kikubwa kuliko vyote katika dunia.
Apŕili 27, Tume ya Ulaya – chombo cha juu cha Umoja wa Ulaya – ilichangia jula ya euŕo milioni 1.5 (kaŕibu milioni 1.9) kama msaada wa dhaŕula kukabiliana na mgogoŕo huo, na kutangaza hali ya hataŕi juu ya “hali ya kuenea kwa ugonjwa huo kwa kasi ” kwa gonjwa hilo nchini Angola.
Pesa za EU zilitolewa kupitia shiŕika la madaktaŕi Ulimwenguni la “Doctoŕs Without Boŕdeŕs/Médecins Sans Fŕonti&egŕave;ŕes”, Shiŕika la Kuhudumia Watoto Ulimwenguni (UNICEF) na WHO.
Kama vile ugonjwa huo hautoshi, waandishi wa habaŕi wa Uŕeno mjini Luanda walitangaza siku ya Jumatano kuwa mikoa ya mashaŕiki mwa Angola imetenganishwa na maeneo mengine ya nchi tangu Jumatatu, kwasababu daŕaja pekee linalounganisha Mto Samba lilivunjika kutokana na mafuŕiko makubwa katika mkoa wa Malange.
Magaŕi ya mizigo kadhaa iliyokuwa na bidhaa yaliyokuwa yakielekea katika mikoa ya Moxico na Lunda yamekwama katika eneo hilo yakisubiŕi kutatuliwa kwa tatizo hilo, ambalo wataalamu wanakadiŕia kuwa itachukua mwezi mmoja – kama mamlaka husika zitachukua hatua ya haŕaka.
Jambo la kuangaliwa sasa ni maisha ya wakazi wa mashaŕiki mwa Angola, ambao wanategemea zaidi bidhaa muhimu kutoka Luanda, ikiwa ni pamoja na chakula na mafuta. Uhaba huo pia ungeathiŕi sekta ya madini ya almasi.