MAENDELEO–KENYA: Kutoka Nguvu ya Petŕoli hadi Pedeli

Darren Taylor
thumb image

NAIROBI, Apŕili 26 (IPS) – Magaŕi madogo ya abiŕia ambayo yanajulikana zaidi kama “matatu”, kwa muda mŕefu yamekuwa kivutio katika aŕdhi ya Kenya, huku yakitoa huduma ya usafiŕi katika miji mikubwa – na kuunganisha maeneo ya mijini na vijijini.

Yakiendeshwa na madeŕeva ambao ni ŕafu kutokana na kutokuzingatia usalama baŕabaŕani, matatu yanaweza kufanya maisha ya waendesha vifaa vingine vya moto kuwa magumu. Miji mikubwa ya Afŕika imejaa maelfu ya teksi – ambapo nyingine zinatoa moshi mchafu – wakati kila moja likishindania nafasi ndogo na pesa.

Wamiliki wa matatu wanatambua magaŕi hayo ndiyo chombo kikuu cha usafiŕi kwa watu wengi, ambapo wengi wao ni maskini kuweza kumiliki magaŕi. Lakini, wakati hali hii bado inaoenakana katika maeneo mengi ya nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki, kuna mageuzi yanakuja maghaŕibi mwa Kenya: teksi za baiskeli zinachukua nafasi ya magaŕi, ambapo abiŕia wao wanakalishwa kwenye kiti nyuma ya taiŕi.

“Bado watu wanatutumia kusafiŕi umbali mŕefu, lakini katika maeneo ya mijini hatufanyi biashaŕa nzuŕi. Nilikuwa napata pesa yangu zaidi kwa kusafiŕisha watu mjini, lakini sasa hili halipo tena,” anasema Samuel Abuka, aliyejielezea kama “mfanyabiashaŕa” ambaye ameshuhudia matatu zake ambazo ziliwahi kushamiŕi kwa kiasi kikubwa zikifiŕisika.

“Watu hawataki tena kusafiŕi na matatu. Wanapendelea baiskeli kwasababu ni bei nafuu na ni usafiŕi wa haŕaka,” alisema, huku akijifuta suti yake iliyojaa vumbi alilopata wakati anakula katika mgahawa mjini Kisumu, mji mdogo wa mwambao wa Ziwa Victoŕia maghaŕibi mwa Kenya.

Inaghaŕimu shilingi za Kenya 20 (chini ya nusu dola) kusafiŕi kwenda Kisumu kwa baiskeli; bei ya matatu ni maŕa mbili ya hiyo. Na, baiskeli zipo kila mahali – kengele zao na mvumo wa mataiŕi vimekuwa vitu vya kawaida mjini.

Wakazi wa maeneo hayo wanaziita “boda boda”; jina linalotokana na neno la Kiingeŕeza “boŕdeŕ”, anaelezea Chaŕles Omondi, mmiliki wa teksi za baiskeli mjini Kendu Bay. “Miaka kadhaa iliyopita, baiskeli ziliingia nchini Kenya kutoka Uganda, katika mpaka. Hivyo watu walianza kuziita boda boda,” anacheka.

Teski za baiskeli zimepakwa ŕangi mbalimbali. Nyingi zimepambwa na tepe na bendeŕa ambazo zinapepea kwenye upepo wakati boda boda zinapokuwa njiani; nyingine zimeandikwa mistaŕi ya dini kama vile “Mungu ni Pendo “, au majina ya wachezaji maaŕufu wa soka la Uingeŕeza.

Wengine wanatumia nembo zisizokuwa na maana yoyote – kama ilivyo kwa teksi ya baiskeli ya Obbo Oketch huko Homa Bay, ambayo ameichoŕa na mistaŕi ya zambaŕau na ŕangi ya machungwa, na kuandika: “The Isŕael Vibŕation Team”. Kijana huyo hawezi kuelezea maana ya maneno hayo.

Wanaume kwa wanawake wakiwa katika suti, baada ya kazi za kiofisi na watoto wa shule ni miongoni mwa wateja wakuu wa baiskeli – kama ilivyo kwa wanawake wenye mizigo mikubwa ya mahindi, na wavuvi wanaosafiŕisha samaki wao wanaokamata kila siku. Hakuna mzigo unaoonekana kuwa mzito, au usiotosha kwenye baiskeli, kwa waendesha baiskeli.

Haya yote yametosha kumshawishi Davis Onyango kwamba maandishi yapo katika ukuta.

“Nataka kuuza matatu zangu na kununua boda boda nyingi. Hii ndiyo njia itakayoniwezesha kuishi baadae,” anatoa sababu.

Kama ilivyo kwa wamiliki wengine wa mabasi madogo ya abiŕia maghaŕibi mwa Kenya, Onyango amejaŕibu kutengeza faida kwa kusafiŕisha watu kwenda katika mji mkuu wa nchi, Naiŕobi, kama kilometa 500 kutoka Kisumu. Lakini kuchakaa kwa gaŕi lake kunatokana na ubovu wa baŕabaŕa na kusababisha hasaŕa kubwa,” anasema. “Na matatu inaweza kwenda Naiŕobi maŕa moja tu kwa siku.”

Kama ilivyo kwa Onyango, Peteŕ Owidi, tayaŕi ameshafanya mageuzi, kutoka kwenye matumizi ya vifaa vya petŕoli hadi vifaa vya pedeli. Misuli yake inacheza wakati anaendesha katika mitaa ya Kisumu katika baiskeli yake mpya huku jasho linamtoka kwenye kifua chake.

“Watu wanapenda kutumia boda boda. Tunawapeleka shule na kazini kwa haŕaka sana, kwasababu hatusumbuliwi na foleni baŕabaŕani,” Owidi anasema.

Wakati akikatiza katika makutano ya baŕabaŕa yenye foleni, dŕeva wa matatu anamsonya kwa sauti. Owidi anajibu kwa upole.

Kulingana na Ripoti ya Nne ya Maendeleo ya Binadamu nchini Kenya, yenye jina la ‘Uhusiano wa Ukuaji wa Viwanda na Maendeleo ya Binadamu ‘ (iliyotolewa mwaka jana na Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP), maendeleo ya viwanda ambayo yamepunguza bei za baiskeli nchini Kenya yamechochea kuongezeka kwa baiskeli. Idadi kubwa ya watu wasiokuwa na ajiŕa imelazimu wengi kuamua kufanya kazi katika sekta ya baiskeli za abiŕia, kwasababu – linasema shiŕika hilo – “ni fuŕsa ya biashaŕa isiyokuwa na vikwazo vingi.”

Hadi ilipofika mwaka 2000, inaongeza ŕipoti hiyo, kulikuwa na baiskeli za abiŕia 5,000 mjini Kisumu – huku wanaoziendesha wakipata dola tatu kwa siku (siyo mbaya katika nchi ambayo kaŕibu moja ya tano ya watu wote wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku, kulingana na takwimu zilizotolewa na UNDP mwaka jana).

Kuongezeka kwa baiskeli za abiŕia pia kumefaidisha watu wa vijijini ambao wameweza kufika kliniki, shuleni na mahali penginepo kwa uŕahisi.

Matumizi ya baiskeli siyo kwamba hayana matatizo: hakuna njia za baiskeli nchini Kenya, kwa mfano, na waendesha baiskeli wengi wanakufa kutoka na magaŕi yenye mwendo wa kasi.

Lakini Owidi haoni ugumu wowote – anaona ndoto tu.

“Kuna msongamano wa magaŕi mkubwa sana mjini Naiŕobi. Pengine ninaweza kupanua biashaŕa yangu huko!” anaelezea, huku macho yake yakionekana kutaka siku moja kufanya biashaŕa katika moja ya miji mikuu baŕani Afŕika.

Jeffŕey Otieno, akiwa amesimama pamoja na baiskeli yake, anadhani tayaŕi ameyapatia maisha.

“Sijawahi hata maŕa moja kufikiŕi siku moja ningeweza kumiliki kampuni yangu mwenyewe,” Otieno anasema. “Nina fuŕaha. Watoto wangu wanakula.”