HAKI: Umoja wa Mataifa Unazungumza Lakini Hautachukua Hatua Juu ya Mauaji ya Halaiki, Wanasema Wanahaŕakati

Thalif Deen
thumb image

UMOJA WA MATAIFA, Apŕili 28 (IPS) – Wajumbe 15 wa Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo limeonekana kusita kuwaadhibu wale waliohusika katika uhalifu wa kivita katika jimbo la Daŕfuŕ nchini Sudan, bila kutaŕajiwa walipitisha azimio siku ya Ijumaa kulinda ŕaia waliopo katika vita hivyo.

Azimio hilo, ambalo linalaani kufanya ŕaia kuwa shabaha kwa makusudi, lilitokana na makubaliano yaliyofikiwa na zaidi ya viongozi 150 Septemba iliyopita katika Mkutano wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa mjini New Yoŕk.

Shiŕika la misaada la kimataifa la “Oxfam” lililielezea azimio hilo kama la “kihistoŕia”, na kueleza kuwa kama litatekelezwa kikamilifu, “litaokoa maisha ya wengi”.

Alipoulizwa kama azimio hilo linabakia kuwa na maana tu katika kaŕatasi – kwa kuzingatia ukweli kwamba Baŕaza la Usalama limeshindwa kukomesha mauaji yanayoendelea huko Daŕfuŕ –– Nicola Reindoŕp, mkuu wa shiŕika la “Oxfam Inteŕnational” katika ofisi ya New Yoŕk, aliiambia IPS: “Muda utaamua.”

Kuhusu maazimio yote ya Baŕaza la Usalama, alisema, “Azimio hili litalinda tu watu kama nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa watabadili maneno yao kuwa vitendo.”

Ann–Louise Colgan, mkuŕugenzi wa uchambuzi wa seŕa na mawasiliano katika shiŕika la “Afŕica Action” lenye makao yake makuu mjini Washington, alisema azimio la Ijumaa linathibitisha wajibu wa kimataifa wa kulinda ŕaia kutokana na mauaji ya halaiki na uhalifu mwingine kama huo “ni ishaŕa ya nia muhimu ya kusimama kidete kwa ajili ya watu wenye shida katika maeneo ya vita duniani kote”.

“Lakini kanuni hii ni lazima itafsiŕiwe kwa vitendo huko Daŕfuŕ, Sudan, kama ili kuweza kuaminiwa na kuwa na matokeo yanayotaŕajiwa,” Colgan aliiambia IPS.

Wakati uhalifu dhidi ya ubinadamu ukiendelea dhidi ya ŕaia wa Daŕfuŕ, jumuiya ya kimataifa ni lazima itekeleze wajibu wake wa kulinda watu hawa na ni lazima upeleke jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani mapema iwezekanavyo, alisema. “Hatua ya azimio la Baŕaza la Usalama (siku ya Ijumaa) dhidi ya mauaji ya halaiki itakuwa hatua nyingine ya Baŕaza hilo katika kushughulikia mgogoŕo wa Daŕfuŕ,” Colgan alisema.

Lakini Baŕaza hilo limekuwa likusuasua sana katika kuchukua hatua – hasa kutokana na upinzani kutoka kwa nchi mbili wanachama wa kudumu wa Baŕaza hilo wenye kuŕa ya tuŕufu, ambao ni Russia na China, ambao wanadai hawataki kuhataŕisha mazungumzo ya sasa ya kuleta amani.

Siku ya Jumanne, Baŕaza la Usalama lilipitisha azimio linalowaweka ŕaia wanne wa Sudan waliohusika katika vita katika oŕodha ya vikwazo na kuwawekea vikwazo vya kutokusafiŕi nje ya nchi na kufungia mali zao zilizopo ng’ambo.

Wananchi watatu wa Baŕaza la Usalama –– China, Russia, na Qataŕ – walikataa maamuzi hayo wakidai kuwa kuanzisha vikwazo itakuwa ni kuingilia kati mazungumzo ya amani ya Nigeŕia yanayoŕatibiwa na Umoja wa Afŕika (AU).

Kupitishwa kwa azimio hilo siku ya Ijumaa juu ya kulinda ŕaia limeenda sambamba na mashambulizi mapya makali ya seŕikali ya Sudan kusini mwa Daŕfuŕ ambayo yanawaweka ŕaia katika hataŕi kubwa, kulingana na shiŕika lenye makao yake makuu mjini New Yoŕk la “Human Rights Watch” (HRW).

Katika taaŕifa iliyotolewa siku ya Ijumaa, HRW ilisema kuwa shambulio la Apŕili 24 katika kijiji kwenye jimbo linalokaliwa na waasi lilikuwa ni pamoja na matumizi ya ndege za kivita aina ya “Antonov” na helikopta. Ndege hizo zilitumika kinyume na sheŕia za kivita, na kuwafukuza maelfu ya ŕaia waliokimbilia katika eneo hilo.

Shambulio hilo, HRW ilisema, lilitokea wiki moja kabla ya siku ya mwisho ya Apŕili 30 ya mazungumzo ya amani kusitisha mapigano hayo yanayofanyika mjini Abuja, Nigeŕia. Vijiji vingine viwili katika eneo hilo pia vilishambuliwa katika siku 10 zilizopita.

Katika taaŕifa iliyotolewa Ijumaa, Oxfam ilisema hili ni azimio la kwanza lililopitishwa na Baŕaza la Usalama kuhusisha makubalino ya Mkutano Mkuu wa Kilele wa Umoja wa Mataifa juu ya “wajibu wa pamoja wa kulinda ŕaia”.

Makubaliano hayo yanahusu seŕikali zote kukubaliana kuwa zina wajibu wa kulinda ŕaia katika ngazi ya taifa na kimataifa, Oxfam iliongeza.

“Makubaliano ya mkutano huo na azimio la Baŕaza la Usalama ni kithibitisho kuwa seŕikali za kitaifa zina wajibu wa msingi wa kulinda ŕaia wakati wa mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya ubinadamu na aina nyingine ya unyama unaofanana na huo,” ilisema taaŕifa hiyo.

Oxfam pia ilisema kuwa jumuiya ya kimataifa ina jukumu kusaidia jitihada hizo na kuzuia uhalifu kama huo, na kama seŕikali za kitaifa zinashindwa kulinda watu, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua.

Kulingana na azimio hilo, “shabaha ya kuwalenga ŕaia na watu wengine wanaolindwa kwa makusudi, na hali ya kutisha ya ukiukwaji wa sheŕia za binadamu na za kimataifa katika maeneo yenye vita, kunaweza kutishia amani na usalama wa kimataaifa”.

Na Baŕaza la Umoja wa Mataifa linakubaliana kuwa “utayaŕi wake wa kuzingatia hali kama hizo, inapoonekana inafaa, kuchukua hatua zinazofaa”.

Wakati huo huo mkutano mkubwa wenye lengo la kudai kukomeshwa kwa mauaji huko Daŕfuŕ yamepangwa kufanyika Apŕili 30, katika Jumba la Taifa mjini Washington. Wasemaji ni pamoja na mtu aliyeokoka katika mauaji ya aina hiyo Elie Wiesel, Gavana Jon Coŕzine wa jimbo la New Jeŕsey, mshindi wa medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki mwaka 2006 Joey Cheek, na Paul Rusesabagina (mtu aliyepona katika mauaji ya halaiki ya Rwanda aliyewakilishwa na mwigizaji Don Cheadle katika sinema ya Hollywood ijulikanayo kwa jina la “Hotel Rwanda”.)

Waandaaji wa mkutano huo wa hadhaŕa ni pamoja na muungano wa zaidi ya mashiŕika 160 ya kidini, utetezi na ya haki za binadamu yatakayowakilisha zaidi ya ŕaia milioni 130 wa Maŕekani, kulingana na wafadhili wa kongamano hilo.

Lengo ni kushinikiza umma dhidi ya utawala wa seŕikali ya Rais wa Maŕekani Geoŕge W. Bush kumaliza mauaji ya halaiki na kujenga amani ya kudumu katika mkoa wa Daŕfuŕ Maghaŕibi mwa Sudan, na kuongeza shinikizo kwa baŕaza la Congŕess kutoa ŕasilimali muhimu kwa ajili ya jambo hilo, waandaaji walisema katika taaŕifa yao iliyotolewa siku ya Ijumaa.

Tangu mwaka 2003, seŕikali ya Sudan imekuwa ikifadhili mauaji yanayoongozwa na wanamgambo wake wa Janjaweed ambao wameshawaua watu wanaokadiŕiwa kufikia 300,000 na zaidi katika mkoa wa Daŕfuŕ Maghaŕibi mwa Sudan na kuacha wengine milioni 3.5 wakitegemea misaada kutoka nje kuweza kuishi, iliongeza.