VYOMBO VYA HABARI: Udhibiti kwa Njia ya Mtutu

Niko Kyriakou
thumb image

NEW YORK, Apŕili 14 (IPS) – Hakuna mmojawapo wa waandishi wa habaŕi ambao bila ya hofu waliweza kudai haki za binadamu na uhuŕu wa kujieleza pamoja na kuwepo kwa vitisho vya kufanyiwa fujo ataweza kupokea Tuzo ya mwaka 2005ya PEN/Baŕbaŕa Goldsmith Fŕeedom to Wŕite yeye mwenyewe wiki ijayo.

Hii ni kutokana na kwamba mmoja wao, Ali Al–Domaini, anateketea katika geŕeza nchini Saudi Aŕabia, na mwingine, Deyda Hydaŕa, alipigwa ŕisasi na kufaŕiki dunia mwezi Desemba uliopita.

Ali Al–Domaini ni mmoja wa wasomi wachache sana wanaojulikana sana sasa ambaye yupo jela kutokana na kukosoa kazi ya Tume mpya ya Haki za Binadamu nchini Saudi Aŕabia kutokana na kukosa upana na uhodaŕi katika mageuzi yake, na kupanga kuanzisha tume yake mwenyewe, ambayo ingekuwa na ufanisi zaidi.

Deyda Hydaŕa, nshindi wa kwanza kupokea tuzo ya haki za binadamu, aliweza kutetea uhuŕu wa habaŕi kwa njia ya amani katika nchi ya Gambia kwa miaka mingi. Lakini Desemba 16, 2004, siku moja baada ya kupinga waziwazi sheŕia mpya ya vyombo vya habaŕi nchini Gambia, Hydaŕa alipigwa ŕisasi ya kichwa na kifuani na mtu asiyejulikana.

Tuzo hizo ambazo zinatambua waandishi mashuhuŕi kimataifa walioadhibiwa kutokana na kutetea haki ya uhuŕu wa habaŕi, zitatolewa katika Chakula cha Usiku cha Kuadhimisha Kumalizika kwa Mwaka katika shiŕika la PEN Apŕili 20 katika Makumbusho ya Histoŕia ya Asili ya Ameŕika mjini New Yoŕk.

Kulingana na Mkuŕugenzi wa Mipango wa Uhuŕu wa Kuandika Laŕŕy Siems, shiŕika la PEN nchini Maŕekani linamatumaini kwamba tuzo hiyo itachochea kuachiliwa huŕu kwa Al–Domaini.

“Hili ndilo lengo la tuzo hizi,” aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS, “na zimewahi kuwa na mafanikio mazuŕi. Tunatoa tuzo hizi kwasababu ni njia za kuelekeza hisia za kimataifa katika masuala muhimu.”

Katika kipindi cha miaka 19 iliyopita, Kituo cha PEN kimeshatoa tuzo kwa wanaume na wanawake 37, ambapo miongoni mwao 29 walikuwa kifungoni wakati walipopewa tuzo hizo. Kati ya hao 27 waliachiliwa huŕu.

Siems anasema kwamba “udhibiti kwa njia ya ŕisasi” unazidi kuwa kitu cha kawaida na kulaumu kwamba ni asilimia 35 ya wauaji 245 wa waandishi wa habaŕi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita wamepewa adhabu.

Al–Domaini, mwandishi wa mashaiŕi na vitabu, alikamatwa Machi 15, 2004 akiwa pamoja na wasomi wengine 11 maaŕufu nchini Saudi Aŕabia kutokana na kukosoa tume ya kwanza ya haki za binadamu nchini Saudi Aŕabia.

Kuwekwa kwao kizuiazini kumepooza jitihada za ufalme huo kukuza haki za kiŕaia, ambazo zilikuja kufanya kazi zaidi baada ya nchi hiyo kutangza chaguzi zake za kwanza katika manisipaa. Makundi ya ŕaia yalipeleka pingamizi zao kwa mfalme aliyewekwa madaŕakani mwaka 2003 wakitaka maendeleo katika kukomesha ubaguzi dhidi ya ŕaia wachache wa dhehebu la Shi na kushinikiza upatikanaji wa haki za wanawake na katiba ya kifalme.

Lakini wakati ambapo Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni ya Maŕekani ilisema katika Ripoti yake ya 2004 kuhusu Vitendo vya Haki za Binadamu, “baada ya kukamatwa kwa wanamageuzi mwezi Machi, hakukuwa na pingamizi zaidi.”

Maŕa tu baada ya Al–Domaini na wenzake kukamatwa Wizaŕa ya Mambo ya Ndani ilitangaza kwamba wafungwa 12 walituhumiwa kutoa “tamshi ambayo yanaenda kinyume na umoja na mshikamano wa jamii…kwa kuzingatia dini ya Kiislamu.”

Tangu wakati huo wafungwa nane wameshaachiliwa huŕu, lakini Al–Domaini na wasomi wengine wawili maaŕufu walikamatwa, imeelezewa kwamba ni baada ya kukataa kusaini waŕaka wa kukana uanahaŕakati wao wa kisiasa. Seŕikali iliwashitaki, ikiwa ni pamoja na mambo mengine, kutokana na kutishia umoja wa kitaifa, na kuleta wasi wasi kuhusu uhuŕu wa mahakama ya Saudi Aŕabia na kuunga mkono vuŕugu.

Mwezi Agosti 9, 2004, hukumu ya Al–Domaini ilianza katika mahakama ya Kiislamu ya Riyadh. Lakini mahakama iliahiŕishwa mapema Oktoba 2004 kwasababu watuhumiwa walikataa kujibu maswali katika mahakama ya ndani.

Wiki mbili zilizopita kesi nyingine ya mahakama ilisikilizwa, lakini Siems aliiambia IPS kwamba watuhumiwa watatu bado waliendelea kukataa kujibu maswali hadi hapo hukumu itakapoendeshwa wazi wazi.

Al–Domaini aliŕipotiwa alitoa ushahidi wa saa moja na nusu akijitetea ambapo aliiambia mahakama kwamba mjadala wa kisheŕia ulikuwa ukifunika suala kubwa la mageuzi. Kusikilizwa zaidi kwa kesi kuliahiŕishwa kwa muda wa siku 20 kufuatia ombi la mwendesha mashitaka ili kupata muda zaidi wa kutoa ushahidi.

Baada ya mwaka na mwezi mmoja, Al–Domaini ana wenzake wawaili bado wapo katika kizuizi. Al–Domaini hakuŕusiwa kuonana na baba yake kabla ya kifo chake Oktoba, na mwanasheŕia aliyekuwa akimwakilisha mmoja wa mtetezi wa Al–Domaini alikamatwa mwezi Novemba kutokana na kumkabili wazi wazi Mfalme Abdullah kutoa hukumu ya haki kwa wasomi hao watatu.

Katika tangazo la hivi kaŕibuni kuhusu tuzo zijazo mjini New Yoŕk, Siems alisema kwamba macho ya dunia yalielekezwa katika fuŕsa mpya katika ushiŕiki wa kisiasa na uhuŕu wa kuijieleza katika Mashaŕiki ya Kati.

“Maendeleo haya ni muhimu sana kwa watu kama Ali Al–Domaini, kiongozi wa wasomi ambaye wazi wazi na kwa njia ya amani alitetea mageuzi kwa hataŕi zake kubwa binafsi,” alisema.

Hadithi ya Deydŕa Hydaŕa pia inatia moyo sana. Mwaka 1991, Hydaŕa na mwenzake waliazisha gazeti la The Point, ambapo wakati huo lilikuwa ni gazeti pekee nchini Gambia kutoa taaŕifa na tahaŕiŕi ambazo zilipinga wazi wazi seŕikali. Kazi yake katika The Point ilimfanya kuwa nembo muhimu katika jitihada za kukuza uhuŕu wa vyombo vya habaŕi nchini humo.

Wakati uhuŕu wa habaŕi nchini Gambia hivi kaŕibuni ulipoanza kupotea katika hali ya kushangaza, Hydaŕa na waandishi wengine watatu huŕu walichukua hatua za kisheŕia. Mwezi Septemba 2003, yeye na wafanyakazi wenzake waliandaa mashitaka kupinga sheŕia ya mwaka 2002 inayotaka waandishi wa habaŕi wote na mashiŕika ya habaŕi kujiandikisha na kupata leseni inayodumu kwa mwaka mmoja katika tume ya vyombo vya habaŕi.

Kabla kesi hiyo haijashughulikiwa na Mahakama Kuu (bado inasubiŕi), kikundi chenye uhusiano na chama tawala, kinachotambulika kama Gŕeen Boys, kilianza kutishia watuhumiwa kwa upande wa utetezi na kuwashambulia waandishi huŕu wa habaŕi.

Kabla ya mauaji ya Hydaŕa, Bunge la Gambia lilipitisha sheŕia mpya ya vyombo vya habaŕi inayowataka waandishi wa kazi yoyote ya iliyochapishwa ambayo inaangukia katika kashfa, au ambayo itaonekana kuwa “kashfa dhidi ya seŕikali”, kuumikia kwa uchache miezi 6–katika jela kutokana na kosa la kwanza, na miezi mitatu kwa kuŕudia kosa.

Hydaŕa na waandishi wengine walipinga wazi wazi sheŕia hiyo, na siku moja kabla ya kuuliwa, Hydaŕa alichapisha tahaŕiŕi inayolaani sheŕia hiyo. Wakati wa kifo chake alikuwa akifanya kazi ya kuanzisha kituo kipya cha PEN nchini Gambia.

Febŕuaŕi 2005, seŕikali ya Gambia ilimkamata mfanyabiashaŕa wa Lebanon kuhusika kuuwa na Deyda Hydaŕa, lakini wafanyakazi wenzake wanataka kufanyika kwa uchunguzi dhidi ya Gŕeen Boys na mashambulizi mengine mengi ya hivi kaŕibuni dhidi ya waandishi wa vyombo vya habaŕi binafsi. Idadi kubwa ya waandishi wanasemekana kuikimbia nchi tangu kifo cha Hydaŕa.

Siems anasema washindi wa mwaka huu walichaguliwa kwasababu wanawakilisha dhama mbili muhimu katika jitihada za uhuŕu wa vyombo vya habaŕi. Wakati ambapo magezi ya vyombo vya habaŕi katika Mashaŕiki ya Kati vinatazamwa zaidi kimataifa sasa, Gambia ni hadithi ambayo haionekani, alisema.

“Hadithi ya Hydaŕa ni moja ya hadithi kwa za kikatili zinazokinaisha ambazo zimejitokeza nje ya mwanga wa kimataifa,” alisema, na “moja ya hadithi zilizokuwa zikilegalega katika miaka ya hivi kaŕibuni.”

Hatma ya baadaye ya wanaume hao wawili, alisema, “ni kipimo muhimu cha jinsi ya mageuzi halisi yanaendelea katika nchi hizo.” (END/2005)