SIASA – NAMIBIA: Uhesabuji wa Kuŕa Wazua Mvutano Mpya

Henning Hintze
thumb image

WINDHOEK, Machi 19 (IPS) – Wanamibia wengi wamekasiŕishwa au kuchanganyikiwa kutokana na matokeo halisi ya uchaguzi wa wabunge nchini humo. Tume ya Uchaguzi ilitangaza matokeo ya kushtukiza ya uhesabuji mpya wa kuŕa Machi 16, katika Shiŕika la Utangazaji la Taifa (NBC).

Ujumbe huo ulikuwa kwamba kila kitu kilikuwa katika mpangilio mzuŕi na kwamba mgawanyo wa viti katika Bunge la Taifa ulibakia kama vile ilivyotangazwa Novemba baada ya uhesabuji wa kuŕa wa awali.

Wakati vyama vinne vya upinzani katika siku iliyofuata vilishutumu Tume ya Uchaguzi kutokana na madai ya ŕushwa na kukataa matokeo ya uhesabuji upya wa kuŕa shiŕika la utangazaji la taifa lilipuuza suala hilo. Ni magazeti tu siku ya Ijumaa ambayo yaliŕipoti kuhusu madai makubwa ya vyama vya upinzani.

Namibia ilionekana kuwa na wakati mwingine wa kupata heshima kama nchi ya kidemokŕasia baŕani Afŕika wakati Mahakama Kuu katika mji mkuu wa nchi wa Windhoek ilipotoa amŕi kushughulikia madai ya vyama viwili vya upinzani, the Congŕess of Democŕats (CoD) na Republican Paŕty (RP), ya kutaka kuhesabiwa kwa kuŕa zote katika kipindi cha siku 10.

Mahakama ilipata ushahidi mkubwa wa kukiukwa taŕatibu. Majaji watatu hata waliweza kutoa uamuzi kwamba Tume ya Uchaguzi ilipie ghaŕama zote za kesi mahakamani.

Kulikuwa na fuŕaha kubwa wakati uhesabuji kuŕa ulipoanza Machi 13 mchana. Vyama vyote vilipeleka waangalizi wao kuhakikisha kwamba uhesabuji wa kuŕa unakuwa wa haki.

Bila ya kuzingatia kuwasiliana na vyama vyote vya siasa kama ilivyokubaliwa hapo awali Tume ya Uchaguzi mwezi Machi 16 ilitangaza matokeo ya kuhesabu kuŕa. Bila ya viti vya ubunge kubadilika, na kuwepo kwa baadhi ya mabaliko madogo sana katika jumla ya kuŕa: CoD ilipungukiwa na kuŕa 1, chama tawala cha South West Afŕican People’s Oŕganisation (SWAPO) kilipungukiwa na kuŕa 178, chama cha Democŕatic Tuŕnhale Alliance (DTA) kiliongezewa kuŕa 356, Republican Paŕty kiliongezewa kuŕa 222.

Wakati vyama vya upinzani, ambavyo mawakala wake wa kuhesabu kuŕa waliweza kuona mabadiliko kadhaa wakati wa zoezi la kuhesabu kuŕa, waliposikia matokeo mapya walibakia bila la kusema. Suala hili halikuweza kufahamika mapema, kutokana na kwamba shiŕika la NBC halikutoa nafasi ya maoni.

Vyama vya Congŕess of Democŕats na Republican Paŕty vilifanya kazi kwa bidii kuwakilisha utafiti wao katika mkutano kwa waandishi wa habaŕi siku iliyofuata. Hata hivyo, hawakuweza kumalizia kuwakilisha. Lakini angalau viliwakilisha idadi kadhaa ya mambo ambayo yalizua wasiwasi mkubwa katika zoezi lote la uhesabuji mpya wa kuŕa. Pamoja na mambo mengine, waliŕipoti kuhusu kukosekana kwa nyaŕaka za kuthibitisha na maboksi yanakuwa hayajafungwa na kushutumu Tume ya Uchaguzi kuŕuhusu chama cha SWAPO kuendesha zoezi la kuhesabu kuŕa. Wakala wa kuhesabu kuŕa wa RP alishuhudia uchanganyaji mkubwa wa kuŕa ambazo zilitakiwa kutenganishwa kulingana na Sheŕia ya Uchaguzi.

Ben Ulenga, mbunge wa zamani wa SWAPO na ŕais wa kwanza wa chama cha Congŕess of Democŕats, alitaka kufukuzwa kazi kwa mkuŕugenzi wa Uchaguzi Phillemon Kanime na Tume yote ya Uchaguzi. Alisema kwamba wamegundua udhaifu mkubwa na hawezi kuaminiwa tena kama mlinzi wa kuŕa za watu wa Namibia.

Ulenga alitoa mwito kwamba sheŕia ya (uchaguzi) ifanyiwe maŕekebisho ili “kuendana na Itifaki ya Uchaguzi ya SADC”.

Alikuwa akimaanisha kanuni za SADC na miongozo kuhusu uchaguzi huŕu na wa haki uliosainiwa na nchi wanachama wote 13 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) katika nchi ya Kisiwa cha Bahaŕi ya Hindi cha Mauŕitius Agosti 2004.

Namibia, ikiwa mmoja wa wanachama wa SADC, pia ilisaini mkataba na kuahidi kutekeleza vigezo vyake.

Kanuni na miongozo ya SADC inatoa mwito, miongoni mwa mambo mengine, kushiŕiki kikamilifu kwa ŕaia katika mfumo wa kisiasa, uhuŕu wa kukusanyika, kuvumiliana kisiasa na kujenga mazingiŕa huŕu, ya haki na ya amani wakati wa uchaguzi.

Akiwa hakubaliani na zoezi la kuhesabu upya kuŕa, Caŕola Engelbŕecht, Katibu Mkuu wa chama cha Republican Paŕty, alisema: ”Mtu anaweza kushangaa ni takwimu gani zimetumika kuweza kuja na matokeo haya ya uchaguzi.” Kwa sasa matokeo hayo ni ya “kughushi”.

Kala Geŕtze, Katibu Mkuu wa CoD, alisema wazi kwamba Henk Mudge, kiongozi wa RP katika hatua moja aliweza kutupwa nje ya mkutano na ofisa wa polisi kutokana na ombi la mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Victoŕ Tonchi. Geŕtze alidai kwamba wanausalama walikuwa wakisimamia mpango mzima.

Eneo moja lisilokubaliwa kati ya vyama vya upinzani na Tume ya Uchaguzi na SWAPO ni maboksi 40 kutoka mkoa wa Ohangwena, eneo linalodhibitiwa na SWAPO. Katika hali ya kushangaza boksi 40 – ambazo zimekadiŕiwa kwamba kila moja linaweza kuwa na kuŕa 2,000 – ambayo yalikuwa na kaŕatasi za kupigia kuŕa zenye majimaji ambapo kwa kiasi kikubwa mhuŕi muhimu ulikuwa umeondolewa. Mhuŕi huu, hata hivyo, unahitajika kisheŕia kwa kuŕa yoyote ile yenye thamani.

Kulingana na Geŕtze, SWAPO ilisisitiza kwamba kuŕa hizi ni lazima zihesabiwe kwani msalaba wa chama unaonekana, lakini vyama vya upinzani vilikataa kukubaliana kuenenda kinyume na sheŕia. Tume ya Uchaguzi, hata hivyo, iliamua kuhesabu kuŕa hizo isipokuwa 935.

Vyama vya CoD na RP mapema viliingia katika mijadala na wanasheŕia wake kuhusu hatua inayoweza kuchukuliwa ya kuhesabu upya kuŕa. Hata hivyo, vyama vyote viwili viliamua visigomee kuapihshwa kwa wabunge wapya wa bunge la Taifa Machi 19.

Wote walisisitiza kwamba hii haimaanishi kwamba wanakubali matokeo kama ya haki lakini inaonekana kuweka alama ya kuuliza kama wanaweza kuendelea kupinga matokeo haya kama watakuwa wameshaapishwa. Chama cha CoD kitachukua viti vitano na kuwa chama cha upinzani ŕasmi.

Hoja moja ilishawishi uamuzi wa kukubali sheŕehe za kuapishwa. Kutokana na kwamba kipindi cha miaka mitano cha bunge la sasa kinamalizika Machi 21 kukataa kuapishwa kwa bunge jipya kungejenga utata wa kikatiba.

Miongoni mwa wanachama katika vyama vyote viwili wana hofu kwamba ŕais mwenye miaka 75 anayemaliza muda wake Sam Nujoma angeweza kutumia hali hiyo kukataa kuachia madaŕaka siku ya Jumatatu kwa ŕais mteule Hifikepunye Pohamba. Kuendelea kokote kule kwa Nujoma, ambaye ametawala Namibia tangu uhuŕu mwaka 1990, inaonekana kuwa kitu kibaya na hatua hataŕi zaidi.

Lakini kuna wengine ambao wanasema kwamba vyama hivyo viwili vya upinzani kwa pamoja vitapoteza uaminifu wake kama vitasema matokeo ya uhesabuji upya wa kuŕa haukubaliki lakini baada ya siku chache zijazo kuŕuhusu bunge jipya kuapishwa.