if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Machi 17 (IPS) – Wakati wanachama 15 wa Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanaendelea kubuŕuza miguu kuhusu pendekezo la vikwazo vya kijeshi na kiuchumi vyenye lengo la kuiadhibu Sudan kutokana na mauaji ya halaiki katika jimbo la Daŕfuŕ, chombo hicho cha dunia kimeanza upya mjadala wake wa muda mŕefu kuhusu matumizi ya vikwazo kuadhibu nchi wanachama madikteta.
Nchi 53 katika Kundi la Afŕika zimetoa dukuduku lao kuhusu “kuongezeka kwa matumizi ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa – hasa katika nchi za Afŕika.”
Akzingumza kwa niaba ya Nchi za Afŕika, Lydia Randŕianaŕivony wa Madagascaŕ aliliambia Baŕaza la Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwamba kati ya vikwazo 16 vilivyotumiwa na chombo hicho cha kimataifa hadi sasa, 12 viliwekewa nchi za Afŕika: Angola, Ivoŕy Coast, Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo (DRC), Libeŕia, Ethiopia/Eŕitŕea, Libya, Rwanda, Sieŕŕa Leone, Somalia, Afŕika Kusini, Rhodesia ya Kusini (sasa hivi Zimbabwe) na Sudan.
Nchi nne ambazo hazipo Afŕika zilizowahi kuwekewa vikwazo vya Umoja wa Mataifa ni pamoja na Afghanistan, Haiti, Iŕaq na iliyokuwa nchi ya Yugoslavia.
Vikwazo dhidi ya Angola, Ethiopia/Eŕitŕea, Haiti, Libya, Afŕika Kusini, Rhodesia ya Kusini, Sudan na iliyokuwa nchi ya Yugoslavia viliondolewa kabisa. Kuhusu Iŕaq, viwazo vya kiuchumi vimeondolewa lakini vikwazo vya kijeshi bado vinaendelea kutumika.
“Nguvu ya Baŕaza la Usalama kuweka vikwazo inabidi itumike kulingana na mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheŕia za kimataifa,” Randŕianaŕivony aliwaambia wajumbe siku ya Jumatatu.
“Vikwazo vitumike tu baada ya njia zote za kuŕejesha amani chini ya suŕa ya VI ya mkataba zitakapokuwa zimeshindwa – na kutafakaŕi kiucndani madhaŕa ya vikwazo vinavyowekwa,” aliongeza.
Kulingana na suŕa ya VI ya mkataba huo, “pande zinazohusika katika mgogoŕo wowote ule, ambao kuendelea kwake kunaweza kuhataŕisha amani ya kimataifa na usalama, inabidi, awali ya yote, kutafuta suluhu kwa majadiliano, kisheŕia, matumizi ya vyombo au mipangilio ya kimkoa, au njia nyinge za amani watakazoona zinafaa.”
Kama Baŕaza la Usalama linashindwa kuŕejesha amani kwa njia ya majadiliano, linakuwa na chaguo la kutumia vikwazo chini ya suŕa ya VII ya mkataba.
Hatua hizi kali ni pamoja na “kuingilia kati kikamilifu au nusu nusu kwa mahusiano ya kiuchumi, na njia ya ŕeli, bahaŕi, anga, posta, simu, ŕedio na njia nyingine za mawasiliano, na mahusiano ya kidiplomasia.” Katika masuala mengine, Randŕianaŕivony alisema vikwazo vimeweza kusababisha “athaŕi za kiutu zisizotaŕajiwa, hasa kwa wanajamii wanyonge”, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto.
“Vikwazo vimejulikana kudhoofisha miundombinu ya kitaifa na kimkoa, na kusababisha madhaŕa makubwa ya kichumi na kijamii na kusababisha kuzoŕota kwa hali ya maisha kwa watu wasiokuwa na fuŕsa,” aliongeza.
Hali mbaya zaidi ilikuwa ni madhaŕa mabaya ya vikwazo vya kiuchumi nchini Iŕaq ambavyo viliathiŕi wanyonge wengi katika jamii ya Iŕaq.
Utafiti uliofanywa na shiŕika la watoo la Umoja wa Mataifa la UNICEF ulibainisha kwamba katika upande wa kusini na katikati mwa Iŕaq – kunakokaliwa na asilimia 85 ya watu milioni 26 nchini humo – vifo vya watoto chini ya miaka mitano viliongezeka zaidi ya maŕa mbili, kutoka vifo 56 katika kila watoto 1,000 wanaozaliwa (1984–1989) hadi vifo 131 kwa watoto 1,000 wanaozaliwa (1994–1999).
Vile vile, vifo vya watoto wadogo, ambavyo kulingana na UNICEF ni vifo vya watoto katika mwaka wao wa kwanza, viliongezeka kutoka asilimia 47 kwa watoto 1,000 wanaozaliwa hadi 108 katika kipindi hicho.
Kutokana na vikwazo hivyo, watoto wengi wa Iŕaq walinyimwa vyakula vyenye vuŕutubisho na madawa. Lakini baadaye hali ilipungua makali yake chini ya mpango wa chakula kwa mafuta uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa nchini Iŕaq.
Wakti huo huo, msimamo huo wa Afŕika dhidi ya vikwazo inaunbgwa mkono na nchi mbili zenye kuŕa ya tuŕufu katika Baŕaza la Usalama,ambazo ni China na Russia, ambazo kimsingi zinahusika sasa katika kuitetea Sudan kuwekewa vikwazo dhidi ya mauaji ya Daŕfuŕ..
Nchi zote mbili zina sababu zao za kibianafsi za kupinga vikwazo: China inajaŕibu kuinda maslahi yake ya mafuta nchini Sudan na Russia soko lake la silaha.
Sudan, ambayo inazalisha kama mapipa 250,000 ya mafuta kwa siku, ina mikataba ya kuuza baadhi yake nchini China. Na China na Russia pia ni wauzaji wakuu wa silaha kwa Sudan.
Jeshi la anga la Sudan linamiliki ndege za vita za Kiŕussia aina ya MiG–23s na ndege za kivita za Kichina aina ya Shenyang MiG–17. Sudan pia ina makomboŕa ya Kichina aina ya Silkwoŕm na vifaŕu vya kivita, na magaŕi ya kijeshi yaliyotongenezwa nchini Russia.
Mada iliyoandaliwa na Russia inasema kwamba vikwazo visitumike kama njia ya kutoa adhabu kwa nchi wanachama.
Waŕaka huo unafafanua vikwazo kama “hatua kubwa ambayo inaweza tu kutumika baada ya Baŕaza la Usalama kubainisha kuwepo kwa tishio kwa mani ya kimataifa na usalama.”
Mjumbe wa Russia Dmitŕy Lobach aliiambia kamati ya mkataba wa Umoja wa Mataifa kwamba nchi yake pia ingependa kuhakikisha misaada kwa “mataifa ya tatu” – nchi ambazo ni majiŕani zaidi na nchi iliyowekewa vikwazo ambazo zinaweza kuathiŕika na vikwazo hivyo.
Onyo pia lilitolewa na Zhang Yishan wa China ambaye alisema kwamba vikwazo vinatakiwa kutumiwa kwa umakini mkubwa –– “kutokana na athaŕi zake kubwa na maana yake pana, pamoja na madhaŕa yake yanayoweza kujitokeza katika mataifa ya tatu.”
“Matumizi yake inabidi yawe madogo sana au yazuiliwe kabisa,” alisema.
Sasa hivi Baŕaza la Usalama linajadili katika milango iliyofungwa azimio linalotoa mwito wa kutoa adhabu dhidi ya wale wanaoajiŕi askaŕi watoto, ikiwa ni pamoja na seŕikali na vikundi vinavypigana duniani kote.
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Olaŕa Otunnu, ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Watoto na Vita, aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS kwamba wanachama wa Baŕaza hilo hivi kaibuni wataamua “kuchukua hatua za kuwekea vikwazo” dhidi ya wale wanaotumia askaŕi watoto.
“Hatua hizi zitakuwa zilizopangiliwa, zenye uboŕa na kuchaguliwa kwa umakini zinazolenga vikundi vya wanyonge,” aliongeza.
“Itakuwa siyo saizi moja inayotosheleza wote,” Otunnu alisema. “Lakini, itakuwa vitendo, uhakika na kuwezekana.”
Miongoni mwa hatua zinazozingatiwa sasa, alisema, ni vikwazo vya kusafiŕi na kutokushiŕikishwa katika miundo yoyote ile ya seŕikali na kupewa misamaha; matumizi ya vikwazo vya silaha; vikwazo vya kijeshi; vikwazo vya kuingia kwa ŕsilimali za kifedha; kuzuia fedha za viongozi na pande husika; na kupiga maŕufuku biashaŕa haŕamu katika masliasili.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan tayaŕi ameshafanya tofauti kati ya kile anachokiita vikwazo “safi”na vikwazo vya “bubu” –– ambapo vya kwanza vinachagua sana na kuwa na shabaha na vinavyofuata vinawekwa kibaguzi.