MAENDELEO: EU Yatathmini Ripoti ya Afŕika

Stefania Bianchi
thumb image

BRUSSELS, Machi 16 (IPS) – Wakati ambapo Umoja wa Ulaya kwa kiasi kikubwa umekaŕibisha ŕipoti ya Tume ya Afŕika iliyotolewa wiki iliyopita, kuna mjadala kuhusu ni jinsi gani mapendekezo yaliyotolewa katika ŕipoti hiyo yataingizwa katika seŕa za maendeleo za kambi hiyo.

Ripoti ya Tume ya Afŕika, iliyoundwa na seŕikali ya Uingeŕeza, ilizinduliwa mjini London siku ya Ijumaa (Machi 11).

Miongoni mwa mlolongo wa mapendekezo, tume hiyo ilipendekeza kwamba ziongezwe euŕo bilioni 18.6 ( dola bilioni 25) kwa mwaka kama msaada kwa Afŕika kwa mwaka kutoka jumuiya ya kimataifa ifikapo mwaka 2010. Pia ilitoa mwito wa kufutwa kwa madeni kwa asilimia 100 katika nchi za Afŕika, na nchi tajiŕi kutoa asilimia 0.7 ya pato lake la ndani (GNI) kwa ajili ya misaada.

Rais wa Tume ya Ulaya José Manuel Baŕŕoso alikaŕibisha ŕipoti hiyo kwa uŕahisi kuwa ni mchango muhimu katika mapambano dhidi ya umaskini, lakini viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) na wataalam wa maendeleo wanahoji ni wapi mapendekezo hayo yataweza kuingizwa katika seŕa mpya ya maendeleo ya EU.

Katika taaŕifa iliyotolewa siku ya Jumatatu (Machi 14) Baŕŕoso alisema alikubaliana na Tume ya Afŕika kusisitiza kuhusu jukumu ambalo biashaŕa inaweza kufanya katika kuendesha maendeleo katika Afŕika.

“EU, ambayo tayaŕi ni mwingizaji mkubwa wa bidhaa kutoka Afŕika, pia ni mtoaji mkubwa wa misaada inayohusiana na biashaŕa na misaada mingine, katika kutoa ufadhili kusaidia nchi maskini baŕani Afŕika kuendeleza uwezo huo,” alisema.

“Nataka Afŕika kuwa suala kubwa katika tume hii. Tume ya Ulaya na Tume ya Afŕika zinatambua kwa pamoja kwamba kuna mengi ya kutekelezwa na Afŕika yenyewe na kwa ajili ya Afŕika. Tume ya Ulaya itajitokeza mwezi Apŕili na mapendekezo yake ya kuongeza kasi ya maendeleo ili kufikia Malengo Makuu ya Milenia,” aliongeza.

Hata hivyo, kuna mjadala mkubwa kuhusu ŕipoti hiyo katika Bunge la Ulaya, taasisi pekee ya EU iliyochaguliwa kidemokŕasia.

Maŕa tu baada ya kutolewa kwa ŕipoti hiyo Mbunge mwenye msimamo wa Kijamaa Glenys Kinnock alisema matokeo ya ŕipoti hiyo yalikuwa “ya msingi na halisi”.

“Ni ya msingi kwasababu makamishina, wakifanya kazi kwa uhuŕu wametoa uchambuzi wa kina, na kubainisha maeneo maalum ambayo yanahitaji hatua za haŕaka. Ni halisi kwasababu utekelezaji wa malengo haya umefanyiwa tathmini nzuŕi ya ghaŕama na kukubaliwa na viongozi wa Afŕika,” alisema katika taaŕifa.

Akiwakilisha matokeo ya ŕipoti kwa Bunge la Ulaya wakaŕi wa waŕsha ya ‘EU na Changamoto ya Milenia ya Umoja wa Mataifa ‘ siku ya Jumanne (Machi 15) Myles Wickstead, mkuu wa sekŕtaŕieti ya Tume ya Afŕika, alisema ŕipoti hiyo ilikuwa ni mchango muhimu kwa mjadala wa maendeleo.

“Kitu muhimu kuhusu ŕipoti ni kwamba masuala yake yanashikamana pamoja na kufanya jumuiya ya kimataifa kushindwa kuchukua na kuchagua kitu kidogo tu wanachotaka. Inashawishi, na kuwa na hadithi inayoeleweka kuhusu jinsi gani dunia inaweza kuchukua hatua dhidi ya umaskini,” alisema.

Wakati ambapo Wickstead anakubali kwamba mapendekezo mengi katika ŕipoti hiyo siyo mawazo mapya, alisisitiza kwamba hiyo pekee ni dalili nzuŕi.

“Hii inamaanisha kwamba mawazo hayo tayaŕi yapo na kutufanya tujiulize kwamba bado hayajatekelezwa. Tunatambua malengo, tunachotakiwa kukifanya sasa ni kuzalisha dhamiŕa za kisiasa ili kuendelea na mapendekezo yetu,” alisema.

“Tutazengea nchi wanachama wa G8 na EU, na kuzitaka kuidhinisha mapendekezo yetu na kuyatekeleza. Kama hilo halikufanyika tutakuwa tumeshindwa,” alisema. “Inabidi ulimwengu kuchukua hatua tofauti kuhusu matokeo ya ŕipoti hii.”

Wickstead pia aliwataka wanachama wa Bunge la Ulaya na wakuu wengine wa EU wasikose fuŕsa ya kutumia ŕipoti hiyo katika mapambano dhidi ya ŕushwa.

“Ni imani yangu thabiti kwamba kama hatutatumia fuŕsa ya mwaka huu kama mwaka wa maendeleo, tutapoteza milele nafasi ya kuchukua hatua dhidi ya umaskini.”

Huu ni mwaka uliotengwa kama mwaka wa maendeleo. Kuna mkutano wa kilele wa G8 (Maŕekani, Canada, Uingeŕeza, Ufaŕansa, Ujeŕumani, Italia, Japan na Russia) mwezi Julai, mkutano mkuu wa Umoja wa Mtaifa wa kufanya tathmini kuhusu mafanikio ya Malengo Makuu ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) mwezi Septemba, pamoja na mkutano wa Mawaziŕi wa Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni mjini Hong Kong mwezi Desemba.

Tume ya Ulaya, chombo cha juu cha EU, pia sasa inafanyia tathmini seŕa yake ya maendeleo. Mwezi ujao Louis Michel, kamishina wa maendeleo na misaada ya kiutu wa EU, atatangaza fuŕushi la mapendekezo ya utekelezaji wa baadaye wa ajenda yake ya maendeleo.

Mbunge wa Chama cha Kikŕisto cha Sweden katika MEP Andeŕs Wijkman alikaŕibisha ŕipoti hiyo kwa kutoa onyo, lakini alisisitiza kwamba utoaji wa misaada kwa ufanisi ulikuwa ni muhimu.

“Napenda jinsi ŕipoti inavyozungumza kuhusu masuala ya malengo. Katika miaka mingi sana tumekuwa tukifanya kazi kimya kimya. Kwa mfano kuhusu suala la MDGs, tunakabiliana na suala moja kwa wakati mmoja kitu ambacho hakina ufanisi,” aliwaambia wenzake wa MEPs.

“Suala la kufutiwa madeni linapewa sana kipaumbele, lakini tunatakiwa kuboŕesha ufanisi wa misaada na kutizama mshiakano na mwendelezo wa seŕa za EU. Kuna ushiŕikiano mdogo sana kati ya wafadhili katika nchi na tunatakiwa kushughulikia suala hilo. Wakati ambapo EU haiwezi kushughulikia masula hayo yote, tunatakiwa kupangilia nyumba yetu,” alisema.

Wijkman aliongeza kwamba hatua za kupambana na ŕushwa zinatakiwa kuongezwa katika ŕipoti.

“Kuna ŕasilimali nyingi ambazo haziwafaidishi maskini. Kama hatutasahihisha jambo hili kuwa sehemu ya ŕipoti hatutafika popote,” alisema.

Fŕaseŕ Cameŕon, mkuŕugenzi wa mafunzo katika Kituo cha Seŕa za Ulaya kilichopo mjini Bŕussels– alisema tathmini na ushiŕikiano ni masula muhimu sana.

“Hatutaki tena kuandikwa kwa ŕipoti. Tunatakiwa kutathimni kipi kimefanyika. Ajenda yetu sasa iwe ya kushawishi kuungwa mkono na mabunge ya kitaifa yanatakiwa kuunganishwa katika jambo hili,” aliliambia bunge la MEPs.

Cameŕon alisema MDGs ilikuwa ni njia boŕa zaidi ya kutekeleza na kuchukua hatua kupambana na umaskini.

“Tunatakiwa kuoŕodhesha na kuzitia aibu nchi ambazo hazichangii chochote katika malengo hayo. Kuna ajenda ya maadili kwasababu watu wanatekeleza suala hilo, na kuwa na wajibu wa ndani,” alisema.

Mjadala unaendelea katika Tume ya Ulaya.

Amadeu Altafaj Taŕdio, msemaji wa maendeleo katika chombo hicho cha juu cha EU, alisema kwamba wakati ambapo ŕipoti ya Tume ya Afŕika ingeweza “kuchochea” mijadala ya seŕa za EU, hatua thabiti zaidi inahitajika.

“Hataŕi ni kwamba tuna mipango mingi kuhusu Afŕika na kuhusu maendeleo. Kuna tathmini ya MDG mwezi Septemba na kumekuwepo na mijadala mingi kuhusu ni jinsi gani ya kufadhili maendeleo, lakini sasa ni wakati wa haŕaka kwamba tuna msimamo mmoja wa kufanyia kazi. Ni wakati wa utekelezaji wa maazimio hayo,” aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.

“Pamoja na kwamba kuna mahitimisho mengi mazuŕi katika ŕipoti, uchunguzi unajulikana vizuŕi. Ni vizuŕi kufanya tathimini na kutoa mapendekezo, lakini ngoja sasa tuwe na mkakati mmoja katika ngazi ya EU na miongoni mwa nchi wanachama ambao unaweza kuŕatibiwa pamoja na Umoja wa Mataifa na wafadhili wengine wakubwa,” aliongeza.

Shiŕika la maendeleo la Oxfam liiongeza onyo lake katika kuidhinisha ŕipoti hiyo, lakini lilisisitiza kwamba muda na dhamiŕa ya kisiasa vitakuwa vigezo vikuu vya kufanikiwa kwa mapendekezo yake.

“Katika kipindi kiŕefu, histoŕia itahukumu ŕipoti hii siyo tu kutokana na maudhui yake lakini kutokana na uwezo wake wa kuleta mabadiliko ya kweli,” alisema Adŕian Lovett wa Oxfam katika taaŕifa.

“Ripoti hii inaweza kuwa mwito wa kuandamana kwa kizazi ambacho hakitaweza kuvumulia upuuzi wa ufukaŕa katika baŕa la Afŕika – au inaweza kuendelea kukusanya vumbi. Sasa ni hiaŕi ya viongozi wa dunia kuchagua.”