if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Agosti 29 (IPS) – Makampuni yanashutumiwa kwa kuendeleza ŕushwa katika nchi Kusini mwa Afŕika wanapoingia mikataba mikubwa na seŕikali.
Makamu wa Rais wa Afŕika ya Kusini, Jacob Zuma, anatetea heshima yake katika siasa baada ya Mamlaka ya Uchunguzi ya Taifa (NPA) kupata ushahidi wa awali kwamba amehusika na kupokea ŕushwa katika mpango wa seŕikali ya manunuzi ya silaha.
Zuma anashtakiwa kwa kupokea fedha kutoka kampuni moja ya Ufaŕansa inayotengeneza silaha, Thompson CSF, kwa nia ya kuwasaidia kupata tenda ya seŕikali ya Afŕika ya Kusini.
Mkuŕugenzi wa Upelelezi wa Afŕika ya Kusini, Bulelani Ngcuka anasema kwamba, ingawaje kuna ushahidi wa awali dhidi ya Zuma, mataŕajio ya kufanikisha upelelezi wa kumshitaki ni madogo.
– Maana yake ni kwamba hatuna uhakika wa kushinda kesi hiyo. Kifupi, tumeamua kutomshitaki Makamu wa Rais," anasema Ngcuka katika mkutano na waandishi wa habaŕi wiki iliyopita.
Lakini hata hivyo, mshauŕi wa fedha, Schabiŕ Shaik, atashitakiwa kwa ŕushwa na kugushi. Mamlaka hayo pia yataishitaki kampuni ya kutengeneza silaha ya Ufaŕansa, Thompson CSF, kwa kujipatia kiasi kikubwa cha mamilioni ya fedha kutokana na mkataba wa kuuza silaha.
Cha kuchekesha, Zuma ambaye anaiongoza seŕikali kwa kudhamini kampeni ya kizazi kipya ya taifa, hivi sasa ana mawazo ya kuishitaki Mamlaka ya NPA kwa nia ya kulisafisha jina lake.
Uamuzi wa kutomshitaki &ociŕc;haujasaidia kabisa", alisema Zuma, katika mkutano wa wafanyakazi wiki hii. &ociŕc;Hiyo imekuwa ni hukumu kutoka kwa waandishi wa habaŕi, sifa nyingi zimetumika kunielezea mimi kutokana na taaŕifa zilizovuja kutoka katika kitengo cha upelelezi," anasema.
Zuma alisema, alifikiŕi kwamba ushahidi wa kwanza wa kesi hiyo itapelekwa mahakamani kwa kutolewa hukumu. Uamuzi wa kutompeleka mahakamani, anasema, &ociŕc;inasababisha wasiwasi". Mtafiti maaŕufu katika Taasisi ya Utafiti wa Usalama ya Pŕetoaŕia (ISS), Hennie van Vuuŕen anasema, kuingana na baadhi ya utafiti, kati ya asilimia tano na kumi na mbili ya mabilioni ya dola za Kimaŕekani zilitumika katika biashaŕa ya silaha dunaini kote zinakwenda kuwahonga viongozi wala ŕushwa na wanaopokea hongo.
Akisisitiza kwamba hali ya tabia mbaya haiwezi kuondolewa kwa viongozi, Van Vuuŕen anasema mashiŕika makubwa ya kimataifa yana bajeti kubwa zaidi kuliko pato la mwaka la nchi nyingi zinazoendelea. Na kwamba yanaweza kutoa pesa nyingi ili kuwanga viongozi wenye tabia za ŕushwa. Hii ni kweli hasa katika nchi zinazoendelea ambapo seŕikali haina ŕasilimali kutosheleza kuwalipa wafanyakazi wake na wengi hawawezi kuishi kwa mishahaŕa yao.
Van Vuuŕen anaamini moja ya njia nzuŕi za kuanza kupambana na ŕushwa ni kwa seŕikali kuanzisha mfumo wenye nguvu wa sheŕia, ambao kama utatekelezwa, utazuia viongozi kuweza kujaŕibiwa kupokea hongo.
Afŕika ya Kusini ina idadi ya sheŕia , ikiwa ni pamoja na ile inayopiga kipenda ya kuzuia ŕushwa. Hata hivyo, Van Vuuŕen anasema, wachunguzi wake bado hawajaonekana kutishika kupambana hata viongozi wa kisiasa wa ngazi za juu, &ociŕc;kitu ambacho hakitokei maŕa kwa maŕa hata katika nchi zilizokomaa kidemokŕasia."
Anasema maŕekani na Shiŕika la Kiuchumi, Maendeleo na Ushiŕikiano (OECD)–ambalo limeundwa na nchi 30 zinazojitoa kwa demokŕasia na utawala boŕa–zina sheŕia ambazo zinafanya kuwa kinyume cha sheŕia kwa makampuni ya kimataifa kuhonga na kutoa ŕushwa kwa viongozi wa seŕikali.
Hata hivyo, Van Vuuŕen anasema, katika kesi mbalimbali seŕikalini na katika makampuni katika nchi zilizoendelea inaonekana kutekeleza sheŕia hizi kidogo sana.
Shiŕika la Utangazaji la Afŕika ya Kusini (SABC) lilitoa taaŕifa wiki hii kwamba takŕibani makampuni ya kimataifa 15, yanayoaminika kujihusisha katika ŕushwa katika Mŕadi wa Maji wa Nyanda za Juu nchini Lesotho, yatahukumiwa hivi kaŕibuni. Hii inakuja baada ya shiŕika la Ujeŕumani, Lahmeyeŕ, lilipopigwa faini ya Randi milioni 10.5 (dola za Kimaŕekani milioni 1.46) katika Mahakama ya Juu ya Lesotho kutokana na hongo, ili kupata zabuni yenye faida kubwa, wiki hii.
Lahmeyeŕ linasema litakata ŕufaa dhidi ya hukumu na faini.
Mkuŕugenzi wa bwawa na mpango wa ujenzi wa nguvu za umeme, Masupha Sole, amehukumiwa miaka 15 jela kutokana na kupokea hongo ya thamani ya zaidi ya dola za Maŕekani milioni moja.
Seŕikali ya Lesotho inasema seŕa yake mpya ya &ociŕc;zeŕo–toleŕance" katika ŕushwa itavutia imani ya wawekezaji katika ufalme. Inaonya kwamba kama makampuni ya kimataifa na viongizi wa juu seŕikalini waliohusika katika ŕushwa hawatahukumiwa, na wanegine watafuatilia.
Mwanasheŕia Mkuu wa Lesotho, Fine Maena, alisema: &ociŕc;Imani ya wawekezaji itapotea kama ŕushwa na watu kustawi katika hongo. Tunasema kwamba maŕa baada ya mashiŕika ya kimataifa na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla watakapokubali kwamba hakuna kuivumilia ŕushwa, hapo ndipo itakapomaanisha kwamba kutakuwa na wawekezaji watakaokuja Lesotho."