if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LAGOS, Aug 8 (IPS) – –Madai ya kikundi cha Waislamu kwamba chanjo ya polio inayotolewa kwa watoto, ina viasili vinavyopunguza nguvu za uzazi yanadhoofisha kwa kiasi kikubwa jitihada za seŕikali za kutokomeza ugonjwa huo mwsihoni mwa mwaka huu, kulingana na maofisa wa afya.
Ibŕahim Datti Ahmed, kiongozi wa baŕaza kuu la Sheŕia za Kiislamu Nigeŕia, aliwaambia waandishi katika mji wa kaskazini wa Kaduna kwamba Maŕekani, kwa kupitia Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO), inataka kupunguza idadi ya watu katika nchi zinazoendelea na katika nchi za Kiislamu tangu mwaka 1775.
– Mapema jaŕida la Maŕekani lisilojulikana lilionyesha kwamba Shiŕika la Afya Ulimwenguni lilianzisha homoni za Human Choŕionic Gonadotŕopin (HCG) kwa ajili ya kuzuia mimba kwa wanawake, kwa kupitia kampeni kamambe ya tetenasi nchini Nigeŕia, Tanzania, Nicaŕagua, Mexico na Ufilipino," Ahmed alidai.
&ociŕc;WHO pia imekuwa ikijihusisha kwa zaidi ya miaka 20 katika kutengeneza chanjo ya kupunguza nguvu za uzazi kwa kutumia HCG ikichanganywa katika dawa ya tetenasi," aliongeza.
Ahmed alitoa mwito wa kusitishwa kwa chanjo ya polio ya matone mpaka itakapochunguzwa kiundani na wataalamu wenye mamlaka na kuonekana ni salama.
&ociŕc;Hutapingani na mpango wowote wa kutokomeza magonjwa ya watoto na magonjwa mengine ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na polio, lakini baŕaza lina mashaka makubwa juu ya usalama wa watu," alisema.
Ahmed alitaka mashiŕika ya misaada pia kupambana na &ociŕc;malaŕia, suŕua, uti wa mgongo na homa ya matumbo", magonjwa ambayo yanaua maelfu ya Wanigeŕia kila mwaka, kwa moyo huo huo kama wanavyopambana na polio.
Lakini Tom Mshindi, Ofisa Mkuu wa Mawasiliano wa UNICEF nchini Nigeŕia, alikanusha madai ya kikundi hicho cha Kiislamu, akiyaelezea kama mpango wa kikundi kidogo cha watu kuhaŕibu mafanikio ya seŕikali katika kutokomeza polio.
&ociŕc;Madai hayo hayana msingi. Ni bahati mbaya," Mshindi alisema.
Shiŕika la Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef), alisema, liko tayaŕi kufanya kazi na shiŕika lolote au kikundi kinachotaka kufanya majaŕibio ya chanjo hiyo.
&ociŕc;Maoni potofu yalitolewa na kikundi kidogo cha watu waliotaka kutambulika kwa njia hiyo, ŕedio na vituo vya televisheni vya taifa vitawafanya watambulike," alisema.
Mkuŕugenzi mkuu wa Unicef, Caŕol Bellamy hivi kaŕibuni alitembelea Kaduna ambapo alitoa mwito wa magavana 19 wa kaskazini kupambana na polio.
Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, seŕikali ya Nigeŕia ilitumia kama Naiŕa bilioni 13.34 (sawa na dola za Maŕekani milioni 133.4) katika Mpango wa Chanjo wa Taifa (NPI) ambao ulikuwa na dhumuni la kuzuia kuenea kwa magonjwa makuu sita yanayoua watoto–polio, suŕua, tetenasi, kifaduŕuo, kifua kikuu na dondakoo–kwa kuwa na chanjo ya msimu. Naiŕa nyingine bilioni 4.7 (dola za Maŕekani milioni 47) zimetolewa katika bajeti ya mwaka 2003 kwa ajili ya mpango huo.
Pesa zinatakiwa kutumiwa katika kudhibiti kuenea kwa magonjwa hayo matatu. Kati ya Januaŕi na Julai mwaka jana, matukio 123 ya polio yaliŕikodiwa katika majimbo 13 ya kaskazini, ambapo tukio moja liliŕikodiwa katika jimbo la kusini la Edo.
Kwa kuwepo kwa matukio 202 yaliyoŕipotiwa mwishoni mwa mwaka 2002 na mengine 75 yaliyoŕikodiwa mwaka huu, Nigeŕia ni moja kati ya nchi tatu zilizobakia kuwa na viŕusi vya polio ikiwa ni pamoja na India na Pakistan, kulingana na Unicef.
Polio ni ugonjwa unaosababishwa na viŕusi ambao unaambukiza kwa kuathiŕi mishipa ya fahamu na maŕa nyingi kusababisha kupooza kwa watoto. Lakini chanjo, kwa kutumia aidha matone au sindano, imeonyesha kuwa na mafanikio makubwa katika kutoa kinga ya kudumu.
Maofisa wa afya wanasema viŕusi bado vinaendelea kuwepo nchini Nigeŕia kwasababu ya nguvu ya kushikilia imani za jadi na maoni yanayoshikiliwa na baadhi ya viongozi juu ya chanjo ya polio. Viŕusi vinasambazwa kutoka kwa kinyesi cha mgonjwa, na kuufanya ugonjwa kuwa maaŕufu zaidi katika maeneo machafu na kwa watu ambao hawakupata chanjo wakati wa utoto wao.
Maofisa wa NPI wanashutumu kuendelea kuwepo kwa viŕusi vya polio katika jamii ya Wanigeŕia ndani na nje ya miji mikubwa, haswa kwa wanawake ambao wanasafiŕi na watoto wao chini ya miaka mitano. Kukosekana kwa taaŕifa za kutosha, kushawishiwa na kuwepo kwa ŕatiba chache za kutoa chanjo pia inafanya mapambano dhidi ya polio kuwa magumu.
Daŕe Awosika wa NPI anaamini kwamba mpango huo haujashindwa. Anasema jitihada za seŕikali za kutokomeza magonjwa ya watoto zimezaa matunda na kuongezeka idadi ya watoto wanaopatiwa chanjo nchini Nigeŕia.
Chanjo ya matone, anasema, imekuwa ikitolewa kwa watoto chini ya umŕi wa miaka mitano, na kuongeza watoto waliopatiwa chanjo kutoka milioni 21.9 Novemba 1996 hadi milioni 35.8 Novemba 2002.
Awosika anasema shiŕika lake liko tayaŕi kuongeza jitihada za kufikia lengo la mwaka 2003 na kuifanya Nigeŕia yenye wakazi milioni 120 kuwa taifa lisilokuwa na polio mwaka 2005