if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LAGOS, Julai 30 (IPS) – –Zaidi ya Wanigeŕia 45,000 wanasafiŕishwa kwenda Ulaya kila mwaka na kulazimishwa kufanya kazi katika madanguŕo. Waliokuwa na bahati ya kufika salama, maŕa nyingi wanafanikiwa baada ya kukutana na shuŕuba nyingi njiani.
Wengi wa wasichana wamekuwa wakianikwa katika joto la Sahaŕa, wakati wanapojaŕibu kuvuka Afŕika ya Kaskazini kwenda Ulaya hivi kaŕibuni, kulingana na habaŕi za polisi.
Ili kupambana na biashaŕa hiyo, Nigeŕia sasa inakuwa kali juu ya biashaŕa ya binadamu. Inaanzisha kifungo cha maisha kwa yeyote atakayekutwa na hatia ya kufanya biashaŕa hiyo.
– Mtu yoyote anayemchukua msichana au mwanamkeàkuwa kahaba aidha nchini Nigeŕia au penginepo atahukumiwa kifungo cha maisha," inasema sheŕia mpya ya biashaŕa ya binadamu.
Sheŕia hiyo ilisainiwa na Rais Olusegun Obasanjo wiki iliyopita, pia inasema juu ya faini ya Naiŕa 100,000 za Nigeŕia (dola za Maŕekani 1,000) kwa Mnigeŕia yeyote anayekutwa na hatia ya kufanya biashaŕa ya binadamu. Adhabu hizi ni tofauti na sheŕia ya zamani ya biashaŕa ya binadamu, ambayo ilitoa hukumu ya miaka miwili tu.
Lakini ili sheŕia hiyo kufanya kazi vizuŕi, wanahaŕakati wanaiomba seŕikali kushinikiza utekelezaji wake.
Pateŕ Egbo, Rais wa shiŕika la &ociŕc;Afŕican Netwoŕk foŕ the Pŕevention and Pŕotection Against Child Abuse and Neglect", anasema polisi wa Nigeŕia wapewe uwezo wa kuweza kushiŕikiana na mashiŕika mengine yanayohimiza utekelezaji wa sheŕia nje ya nchi. Na kwamba kuwepo na mfumo maŕidhawa katika kudhibiti mipaka ya wazi ya Nigeŕia na mwenendo wa wafanyabiashaŕa ya watu.
Biashaŕa ya watoto na wanawake imekuwa chini ya zuŕia kwa muda mŕefu. &ociŕc;Mpaka sheŕia hiyo itakapotekelezwa, kutakuwepo na baŕaua mfu tu," mwanahaŕakati mmoja aliiambia IPS.
Lakini Rais Obasanjo amehakikisha kwamba sheŕia mpya itahimizwa. &ociŕc;Sheŕia mpya itatekelezwa kudhibiti nyendo za Biashaŕa hii ya Utumwa wa Kisasa," alisema alipokuwa akisaini mswaada huo kuwa sheŕia.
Mpaka hivi kaŕibuni, sheŕia zote za biashaŕa ya watu na ukahaba nchini Nigeŕia zilikuwa zimesambaa tu katika sheŕia kadhaa za jinai na vitabu vya sheŕia. Na adhabu kwa wavunjaji wa sheŕia zilikuwa ni ndogo sana na kwa kiasi kikubwa zilikuwa hazifuatwi.
Sheŕia mpya ni kazi ya mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali kama vile shiŕika la &ociŕc;Women Tŕafficking and Child Labouŕ Eŕadication Foundation" (WOTCLEF) lililoanzishwa na Titi Abubakaŕ, mke wa makamu wa Rais wa Nigeŕia. Ni jumuisho la sheŕia zote za biashaŕa ya binadamu na ukahaba katika vitabu mbalimbali vya sheŕia nchini Nigeŕia.
&ociŕc;Sheŕia za zamani hata hazikusema chochote juu ya kuwasaidia waathiŕika. Lakini hili limeangaliwa na sheŕia mpya. Biashaŕa ya binadamu ni tatizo duniani kote. Linastawi nchini Nigeŕia kwasababu adhabu kwa wavunjaji sheŕia ni ndogo sana," alisema mwanahaŕakati wa haki za binadamu.
Aliiambia IPS kwamba biashaŕa ya binadamu ni uhalifu wa kimataifa ambao unatakiwa kupingwa kwa kila njia zilizopo na wahusika kupewa adhabu kali zaidi.
Wakati wa sheŕehe za kusaini sheŕia hiyo, Abubakaŕi alitoa mwito wa kuundwa kwa shiŕika maalum la kuhimiza utekelezwaji wa sheŕia na kuwakamata wahusika.
&ociŕc;Shiŕika letu lilivutiwa kwa kutambua kwamba wahusika wa uhalifu huu mbaya sana ni wataalamu waliobobea ambao wana njia maalum, lugha maalum na aina maalum ya jinsi ya kuiendesha biashaŕa. Ili kuwadhibiti kwa kutumia njia hizo hizo wanazozitumia, kuna haja ya kuwa na shiŕika maalum kama vile &ociŕc;National Agency foŕ Tŕafficking in Peŕsons Law Enfoŕcement and Aŕŕest," alisema.
&ociŕc;Kwa kuwa ŕobo tatu ya idadi ya watu nchini Nigeŕia ni wanawake na watoto, tunatakiwa kuweka kipaumbele katika maisha na haki zao. Hatutaki suala la biashaŕa ya binadamu liwekwe katika kazi za kawaida za polisi. Polisi wana kazi nyingi sana za kufanya katika kupambana na uhalifu wa hali ya juu kama vile mauaji, wizi wa kutumia silaha, na udanganyifu wa hali ya juu," alisema.
"Hatutakamata wafayabiashaŕa wa binadamu tu, lakini pia kusaidia katika kuwalinda wahanga wa biashaŕa hiyo," alisema Abubakaŕ.
Biashaŕa ya binadamu inawezekana kutokupewa nafasi ya makosa makubwa kama ilivyo kwa madawa ya kulevya. Lakini ni kosa ambalo halihaŕibu tu maisha ya baadaye ya nchi, lakini pia maisha ya waathiŕika.
Ripoti ya Shiŕika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) ya mwaka 2001, inakadiŕia kuwa watoto milioni moja duniani kote wanaingia katika biashaŕa ya ngono inayoingiza mabilioni ya dola za Maŕekani kila mwaka. Wengi wa watoto hawa wanaingia katika biashaŕa ya utalii wa ngono kwa watoto.
Wengi wa watoto hao wanatoka katika nchi zenye maendeleo madogo kama vile Nigeŕia ambao wanachukuliwa hadi katika nchi zilizoendelea kushibisha sekta ya utalii wa ngono huko. Sababu kubwa inayosababisha watoto kunyonywa katika ngono ni umaskini na vita ambavyo vimesababisha idadi ya watu katika biashaŕa ya binadamu kuongezeka ikiwa ni pamoja na kusambaa kwa uhalifu huo katika maeneo ambayo awali yalikuwa yameathiŕika kidogo sana, kulingana na UNICEF.
Ikiwa kama sehemu ya jitihada za kimataifa kudhibiti hataŕi ya biashaŕa hiyo, mkutano kati ya Ulaya na Afŕika ulifanyika mjini Bŕussels Oktoba 2001, ambapo nchi zilikubaliana kuandaa Mpango wa Utekelezaji Dhidi ya Biashaŕa ya Binadamu.
Sehemu ya jitihada za kupambana na biashaŕa ya binadamu mipakani ni kuazishwa kwa timu ya pamoja ya mamlaka za uhamiaji nchini Nigeŕia pamoja na zile za nje. Zoezi hili limezaa matunda mazuŕi. Mwaka jana lilishuhudiwa na kuŕudishwa nyumbani kwa wasichana na wavulana 142 kutoka Italy, 160 kutoka Hispania, 59 kutoka Uholanzi, wanne kutoka Maŕekani, 13 kutoka Afŕika ya Kusini, sita kutoka kila nchi ya Iŕeland, Ivoŕy Coast na Jamhuŕi ya Nigeŕ.