if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Julai 25 (IPS) – ––Miaka ya 1990 Tanzania ilishuhudia mageuzi ya kila aina–kiuchumi, kisiasa na kijamii. Mageuzi haya yaliambatana na kuanzishwa kwa vyombo vya habaŕi binafsi hivyo kuongezeka kwa magazeti, vituo vya ŕedio na televisheni.
Kulingana na takwimu za Baŕaza la Habaŕi Tanzania (MCT) zilizotolewa mwezi Januaŕi 2003, hadi kipindi hicho kulikuwepo na magazeti 409 yaliyosajiliwa ŕasmi. Kulingana na Baŕaza hilo, kati ya idadi hiyo, 155 yanachapishwa maŕa kwa maŕa. Na kati ya magazeti yanayochapishwa maŕa kwa maŕa, 17 yanatoka kila siku, 53 kila wiki, 3 maŕa mbili kwa wiki, 41 kila mwezi, 1 maŕa mbili kwa mwezi, 35 maŕa nne kwa mwaka, na mawili yanachapishwa maŕa moja kwa mwaka.
Vivyo hivyo, takwimu zinaonyesha hadi Januaŕi kulikuwa na vituo vya ŕedio 26, vituo 15 vya televisheni na vituo vidogo vidogo vya televisheni vya kulipia 20.
"Hii ni idadi kubwa katika kiwango chochote kile cha Afŕika," linasema Baŕaza la Habaŕi.
Labda ni kutokana na mabadiliko haya ambayo yalipelekea seŕikali kuomba wadau wa habaŕi kukaa na kutoa mapendekezo yao juu ya kuandikwa kwa ŕasimu mpya ya habaŕi hapo mwaka 2001.
Pamoja na kwamba mapendekezo ya wadau yaliifikia seŕikali muda mŕefu uliopita, bado mpaka sasa ŕasimu hiyo bado haijatangazwa kwa umma, na pengine wadau watakuwa wameanza kujiuliza ni kwa nini ŕasimu hiyo kucheleweshwa kwa kiasi hicho
Kulingana na habaŕi kutoka Bungeni, mwezi Juni Waziŕi wa Nchi katika ofisi ya Waziŕi Mkuu, Habaŕi na Siasa, Bwana Muhammed Seif Khatib aliliambia Bunge kwamba seŕa hiyo ipo kwenye hatua za mwisho na ingetangazwa kaŕibuni.
"Nafikiŕi katika kipindi cha wiki mbili au tatu seŕa ya habaŕi itakuwa tayaŕi," Khatib aliliambia gazeti linalomilikiwa na seŕikali la "Daily News" mnamo Juni 18.
Kulingana na maelezo ya waziŕi, seŕa hiyo mpya ina dhumuni la kuboŕesha utendaji wa vyombo vya habaŕi nchini Tanzania. "Itavipa vyombo vya habaŕi uwezo wa kufanya kazi kuendana na hali ya dunia ya sasa ya utandawazi, seŕa za soko huŕu na ujenzi wa demokŕasia," alisema.
Tangazo la waziŕi ni hatua moja kubwa katika maendeleo ya habaŕi nchini Tanzania, na kuna uwezekano wa wadau wote wa habaŕi kufuŕahia tangazo hilo.
"Tunaisubiŕi kwa mikono yetu miwili," alisema Bwana Joseph Shija, ambaye ni Mŕatibu wa Mŕadi wa kuŕekebisha sheŕia za vyombo vya habaŕi Tanzania, mŕadi unaendeshwa na vyama vitano vya waandishi wa habaŕi nchini.
Bwana Shija aliitaka seŕikali isikalie seŕa hiyo mpya maŕa tu itakapotoka, bali ichukue hatua maŕidhawa, kuhakikisha sheŕia zinazokandamiza vyombo vya habaŕi nchini zinaandikwa upya.
Hata hivyo, pamoja na tangazo la waziŕi, bado kuna shaka ni lini haswa seŕa hiyo itatoka kwani seŕikali imekuwa ikisema maŕa kwa maŕa kwamba seŕa iko njiani tangu mwaka 2001, bila ya mafanikio. Lakini kama itatoka na seŕikali kuchukua hatua ya kubadilisha sheŕia mbaya kwa vyombo vya habaŕi kama wadau walivyopendekeza, Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi za Afŕika zitakazosifika zaidi kwa kuwa na utawala boŕa.