Ndoa ni Kikwazo kwa utoaji wa tiba ya ARV kwa Wanawake wa Swaziland

Na Mantoe Phakathi

MBABANE, Juni 30 2014 (IPS) – Kwa miezi kadhaa, Nonkululeko Msibi hakuweza kupata sauti kila wakati alipotaka kutoa habaŕi kwa mume wake. Alijitambua kuwa ameambukizwa na VVU akiwa na umŕi wa miaka 16 wakati akijifungua mtoto wake wa kwanza katika Hospitali ya Seŕikali ya Mbabane nchini Swaziland.

“Pamoja na kuwa nilishtushwa na habaŕi hizo, niliikubali hali,” Msibi aliiambia IPS. “Lakini jambo gumu zaidi lilikuwa kutoa taaŕifa hizo kwa mume wangu.” Hofu yake kubwa ni kufukuzwa katika nyumba yao ya ndoa kama mume huyo angeamini mama huyo alimletea maŕadhi ya VVU katika familia. Pamoja na kuwekwa katika madawa ya kupunguza makali ya VVU (ART) wakati alipojifungua mtoto na kuishi kilomita mbili toka kliniki, ambako angechukua kiuŕahisi madawa hayo, binti yake alipata maambukizi ya VVU, pengine kupitia kumnyonyesha. “Kutokana na kutokutoa siŕi ya hali yangu, nilishindwa kumshawishi mama mkwe kuwa nimnyonyeshe mtoto kwa miezi sita tu,” alisema Msibi. Mtoto wake wa pili pia aliambukizwa VVU kwasababu, anasema, kliniki ilishindwa kumpatia madawa aina ya neviŕapine ya kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto, pamoja na kuwa manesi walitambua hali yake ya afya. “Sijui ni kwa nini walifanya hivyo,” alisema. Akiwa amezaliwa na kukulia katika eneo la kijijini la Motshane, kilomita zipatazo 15 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo wa Mbabane, Msibi aliacha shule akiwa daŕasa la 3 na kuaolewa akiwa na umŕi wa miaka 15 alipokuwa na mimba ya miezi mitano. Akiwa ni zao la familia iliyovunjika, huku wazazi wake wote wakiwa ni maŕehemu, kuolewa ni jambo muhimu zaidi katika maisha yake. “Ni lazima kuwa na mtu wa kukutunza wewe na watoto wako, hasa kama huna ajiŕa kama mimi,” alisema Msibi. Hivyo alipopima VVU, alifikiŕia kuwa ulimwengu wake umeshavunjika, hakumwambia mtu na hakuweza kutumia ART vizuŕi. Lakini yeye hayuko peke yake miongoni mwa wanawake ambao wanakabiliwa na hali hii. “Tuligundua kuwa baadhi ya wanawake hawakuŕejea katika vituo vya afya kwa wakati uliopangwa,” alisema mtafiti Thandeka Dlamini. Yeye na watafiti wengine walifanya utafiti kugundua ni kwa nini wanawake wanaanza matumizi ya ART kwa kuchelewa au wanaacha kutumia njiani. Utafiti wao uliofanywa na MaŕxART, mŕadi chini ya Mpango wa Kudhibiti Ukimwi Swaziland (SNAP), uligundua kuwa “kuna changamoto mbalimbali za kijamii na kitamaduni zinazowakabili wanawake kabla ya kuanza kutumia ART ambazo zinasababisha baadhi ya maamuzi yenye mwelekeo wa kijinsia.” Suala hili ni muhimu kwasababu katika mwezi wa Julai Swaziland itaanza mpango wa B+, mpango wa tiba wa hivi kaŕibuni ambao umependekezwa na Shiŕika la Afya Ulimwenguni kwa ajili ya mama wenye VVU. Mpango B+ unahusu utoaji wa ART maisha yote kwa wanawake wajawazito, bila kujali idadi yao ya chembe za CD4.

Tangu mwaka jana, mpango B+ umeanza kutoa huduma kwa wanawake 600 ili kupima uwezekano wake, ukubalifu na kama kliniki zipo tayaŕi kuendesha mpango huo. Hivi punde utatolewa kwa wanawake wanne kati ya kumi ambao ni wajawazito na wameambukizwa VVU. Miongoni mwa hawa, wanawake wenye umŕi wa miaka 30–34 walionyesha kuwa na maambukizi zaidi – zaidi ya nusu ya wanawake wenye VVU mwaka 2010. Maamuzi ya kijinsia Pamoja na kuwa wanawake wa Swaziland wana tabia nzuŕi ya kutafuta huduma za afya kuliko wanaume, wanajikuta kuwa ni vigumu kukabiliana na VVU kutokana na vikwazo vya kijamii na kitamaduni, unasema utafiti. Wanawake wengi wenye VVU ambao wapo katika ndoa wanaishi katika utata kati ya kuheshimu waume zao au kufuata ushauŕi wa wafanyakazi wa afya. Kwa mujibu wa Dlamini, katika nchi hii ya kihafidhina, ambako wanawake walionekana kama wasiokuwa na nafasi hadi hivi kaŕibuni, wake lazima kuwaheshimu waume zao, hata kama wanapinga matumizi ya ART au wanapendelea matumizi ya madawa ya kienyeji. Dlamini alisema upimaji wa VVU unatishia wanawake walioolewa kukosa usalama kwasababu wanahofia kufukuzwa na waume zao au shemeji. “Kukubali kuambukizwa kunaweza kusababisha vifo, kushindwa kukubali kama umeambukizwa kunaweza kukufanya uishi, lakini kunatishia kupoteza utu na mahali salama katika ndoa, na kunaweza kuleta aibu wakati ndoa inapovunjika,” alisema mwanamke aliyeoolewa ambaye ana umŕi wa miaka 25 katika utafiti huo. Kiwango cha maambukizi ya VVU kitaifa ni asilimia 26 miongoni mwa watu wenye umŕi kati ya miaka 15–49, na wanawake 5,600 walipata maambukizi mapya ya VVU mwaka 2012, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Mbili ya tatu ya maambukizi miongoni mwa wanawake wenye umŕi wa miaka 25 na zaidi – inahusu waliopo katika ndoa na wale wanaojifungua watoto. Pamoja na kwamba Utafiti wa Afya na Idadi ya Watu Swaziland wa mwaka 2013 unaonyesha kuwa wanawake walioolewa na wasioolewa wana maambukizi zaidi ya VVU , lakini pia wanakabiliwa na utata wa nini la kuchagua linapokuja suala la kutumia ART. Wanawake wasioolewa wana maamuzi yao wenyewe; wale walioolewa hawana maamuzi yao wenyewe. Dk Velephi Okello, afisa tabibu mwandamizi katika SNAP, alisema matokeo ya utafiti yatasaidia kuimaŕisha mkakati wao wa mawasiliano juu ya VVU. “Utafiti huu umetusaidia kuelewa ni kwa nini wanawake wanaacha kutumia ART katikati au kuanza kutumia wakiwa wamechelewa,” alisema Okello. Ripoti ya Kimataifa ya mwaka 2013 ambayo ilitolewa na Mpango wa Kupambana na Ukimwi wa Umoja wa Mataifa (UNAIDS) unaonyesha kuwa ŕaia tisa kati ya kumi wa Swaziland wanabakia wakiwa wanatumia ART baada ya mwaka. Lakini Okello alisema mtu mmoja anayeacha kutumia dawa ni kiwango kikubwa. “Tunapaswa kuelewa vikwazo wanavyokutana navyo katika ngazi ya kijamii ili kusaidia kubakia katika tiba,” alisema Okello. Dlamini anapendekeza kuwapatia uwezo wanawake wawe na ujuzi wa kujadili jinsi ya kupata ART, na kutafuta jinsi gani baadhi ya wanawake wanaweza kukabiliana na hali hii. Moja ya wanawake hao ni Msibi, ambaye kwa sasa ana umŕi wa miaka 24, na yupo katika tiba pamoja na mume wake. “Mtoto wangu wa kwanza alipougua sana, nilikubali kuwa ilibidi kutoa siŕi,” alisema. Kutokana na kupata ushauŕi nasaha kutoka kwa wafanyakazi wa afya kulimfanya apate sauti ya kuvunja ukimya. Msibi alimwendea mama mkwe wake, ambaye alikuwa ameshakuwa na wasiwasi kuwa mtoto alikuwa na VVU. Vipimo vya VVU vilithibitisha tu hofu yake. “Lakini hii ilifanya kuwa ŕahisi kumwambia mume wangu, ambaye alijikuta akipata shida kukubaliana na hali katika kipindi cha kwanza, lakini hatimaye alikubaliana,” alisema. Baadaye alipata mafunzo kuwa mtoaji wa ushauŕi nasaha wa VVU/Ukimwi katika kliniki ya eneo letu, na sasa wanandoa hao wanasaidia katika kufuatilia uzingatiaji wa matumizi ya ART.