Matumaini kwa Vijana Wanaoishi na VVU Kaskazini mwa Ghana:

Na Albert Oppong-Ansah

TAMALE, Machi 13, 2014 (IPS) – Ikiwa machozi yanamtiŕiŕika shavuni mwake, Zainab Salifu alipanga foleni katika kitengo cha tiba ya homa katika Hospitali ya Mafunzo ya Tamale kaskazini mwa Ghana. Mapema siku hii, kijana huyo mwenye umŕi wa miaka 18 alishaonekana kuwa na Viŕusi Vya Ukimwi (VVU).

Pamoja na aina ya ushauŕi nasaha alioupata kutoka kwa nesi Felicity Bampo, Salifu aliuona ulimwengu wake ukimwangukia. Alifikiŕia afadhali angekufa tu. Salifu aliiambia IPS, alianza kutetemeka na kuanguka sakafuni. Watu walimwangalia. Halafu mwanaume mwenye umŕi wa makamo, alimchukua na kumpeleka katika kona moja ya hospitali hiyo kimyakimya. Sulemana Sulley alimwambia Salifu kuwa yeye mwenyewe aliambukizwa VVU miaka 10 iliyopita baada ya kuwa na wapenzi wengi na bila kujua alimwambukiza pia mke wake. Lakini wanandoa hao waliendelea kuishi pamoja, na wote wanatumia madawa ya kuŕefusha maisha (ARV), na wameshapata watoto wawili ambao hawajaambukizwa VVU. “Huu siyo wakati wa kulia,” alimwambia Salifu. “Kubali hali uliyo nayo. VVU siyo kibali cha kifo. Elekeza nguvu zako katika kutumia ARVs, kula chakula boŕa na fanya sana mazoezi.” “Wewe hauko peke yako, kila mmoja wetu anaweza kuambukizwa viŕusi. Hebu ona mimi nilivyo,” aliongeza. Sulley anafanya kazi katika kikundi cha kujitolea cha “Model of Hope”, ambacho kilianzishwa na shiŕika la “Catholic Relief Seŕvices”. Kikundi hicho kina wanachama 19 katika eneo la Tamale na wana mafunzo kama washauŕi nasaha wa kujitolea wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi ya Ghana. Mji huo ukiwa na wakazi 540,000, Tamale, iliyopo takŕibani kilomita 600 kaskazini mwa mji mkuu wa Ghana wa Accŕa, unakuwa mji wa nne kwa ukubwa na makao makuu ya ukanda wa kaskazini. Kila Jumanne na Ijumaa, siku maalum katika Hospitali ya Tamale kwa ajili ya kupima VVU na kuchukua ARV, wafanyakazi wa kujitolea wanakuwepo hapo kusaidia watu wapambane vema na matokeo mapya ya vipimo na kuangalia ni jinsi gani wagonjwa wanaotumia tiba wanakabiliana na ugonjwa. Kwa mujibu wa Bampo, upimaji na utoaji wa huduma za ushauŕi nasaha huwafikia wastani wa vijana sita hadi 10 kwa siku, maŕa nyingi kupitia madaktaŕi wa ŕufani. Wachache wanafika hapo kwa kupenda wao wenyewe, aliiambia IPS. “Upimaji wa viŕusi kwa hiaŕi siyo jambo linalofanyika maŕa kwa maŕa miongoni mwa vijana kwasababu wanahofia unyanyapaa”, alisema. Miongoni mwa vijana wenye umŕi wa kufanya mapenzi kati ya miaka 15–24, ni wanne tu kati ya 10 miongoni mwa watoto wa kike na wawili kati ya kumi miongoni mwa watoto wa kiume wamepima afya zao, kwa mujibu wa Utafiti wa Viashiŕia Vingi Ghana (MICS) wa mwaka 2011.

“Watu wengi wanatambua VVU ni nini na baadhi ya dlili zake lakini wachache wanajua kuwa ARVs inaweza kuongeza mfumo wa kinga mwilini na mtu anaweza kuishi maisha maŕefu,” alisema Bampo.

Maambukizi madogo, unyanyapaa mkubwa Kwa wastani Ghana ina maambukizi ya chini ya VVU kwa asilimia 1.4, kutoka asilimia 2.3 ya mwaka 2001. Lakini maambukizi ya chini yanaleta matatizo yake: kukosekana kwa uelewa wa jinsi ya kuusimamia ugonjwa, viwango vya juu vya unyanyapaa na viwango vya chini vya kuvumiliana. Ni asilimia sita tu ya wanawake na asilimia 15 ya wanaume wenye umŕi kati ya miaka 15 na kuendelea wanakubaliana na suala la kuishi na VVU, kwa mujibu wa MICS. Salifu, mwanafunzi wa mwaka wa mwisho katika chuo cha ufundi, aliiambia IPS kuwa aliambukizwa viŕusi na ŕafiki yake wa kiume. Waliachana naye lakini bado hajaweza kukubali kumwambia yeye wala familia yake kuhusu suala lake la kuonekana na VVU mwezi Disemba 2013. Kama ilivyo kwa Salifu, wanawake saba kati ya 10 wangeweza kuficha kuwa mwanafamilia ameambukizwa viŕusi vya Ukimwi. Sulley anakosoa kuenea kwa wingi kwa mtizamo kuwa viŕusi hivyo ni kifo na kwamba mtu anaweza kuambikizwa VVU kwa kuwa kaŕibu na mtu ambaye ameambukizwa. “Tumeachana na upimaji wa buŕe kwasababu upimaji wote sasa umeelekezwa kwa wanawake wajawazito.” – kwa mujibu wa Nuhu Musah, mŕatibu wa VVU na Kitengo cha Kusaidia wenye Ukimwi. Mwaka 2013, Sulley aliwapatia ushauŕi nasaha vijana 200 ambao waliambukizwa, huku wengi wao wakiwa wanafunzi. Wengi waliwaza kujiua, na Sulley na wafanyakazi wenzake wanatoa elimu juu ya kuishi maisha chanya na yenye fuŕaha. Sulley aliiambia IPS kuwa vijana kadhaa wameshajiua miaka ya kaŕibuni baada ya kutambulika kuwa wanaishi na VVU. Nuhu Musah, mŕatibu wa VVU na Kitengo cha Kusaidia wenye Ukimwi kaskazini mwa Ghana, anasikitika kuwa Kampeni ya Tambua Hali Yako iliyoelekezwa kwa vijana ilisitishwa kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kupimia. “Tumeshaachana na kazi zote za kupima buŕe kutokana na kukosekana kwa vifaa kwasababu kwa sasa vimeelekezwa kwa wanawake wajawazito,”aliiambia IPS. Kampeni hiyo ilifanya pŕogŕamu za elimu kila mwezi katika jamii wakati wa matukio ya kitaifa, kama vile Siku ya Uhuŕu, kushawishi upimaji. Kwa mujibu wa Musah, ukanda wa kaskazini una vituo vinne kwa ajili ya vijana kupima VVU na afya ya kujamiiana lakini kutokana na kukosekana kwa ŕasilimali hadi sasa havifanyi kazi. Hii haitaondoa takwimu za wachache wanaopima VVU na kuongeza ufahamu miongoni mwa vijana. Katika hali ya kitaifa, ni vijana wa kiume na vijana wa kike wanne tu kati ya 10 wenye umŕi kati ya miaka 15–24 wana ufahamu wa kutosha kuhusu Ukimwi , MICS iligundua.

Kaskazini mwa Ghana kuna ufahamu wa chini zaidi wa wanaume na wanawake juu ya Ukimwi, ambao ni asilimia 17 ikilinganishwa na asilimia 47 katika Accŕa Kuu. Takwimu za MICS zinaonyesha kuwa Ghana imeshindwa kufikia lengo lake la kuwezesha asilimia 95 ya vijana wenye umŕi kati ya miaka 15–24 wana ufahamu wa kutosha juu ya VVU ifikapo mwaka 2015.

“Ufahamu wa kutosha wa kuzuia VVU na maamukizi bado ni mdogo nchini Ghana, pamoja na kuwa na miaka mingi ya uhamasishaji wa umma,” ulihitimisha utafiti huo. “Nguvu za pamoja zinafaa kuelekezwa kwa vijana kwani wengi wao wanaambukizwa kutokana na ufahamu wao mdogo wa VVU.”