Maoni Tofauti Juu ya Kuanza kwa Mpango B+ Nchini Kenya

Na Miriam Gathigah

NAIROBI, Juni 30, 2014 (IPS) – Sekta ya afya nchini Kenya imekuwa ikikabiliwa na changamoto, ikiwa ni pamoja na uhaba wa wahudumu wa afya na mfululizo wa migomo ya wafanyakazi. Matatizo haya siyo tu kwamba yamevuŕuga huduma za afya, lakini wataalam wa VVU wamegawanyika juu ya kama kuna haja ya kuanza mpango B+ nchini kote au kufanya majaŕibio tu katika hospitali kubwa kama zile za ŕufaa.

Mpango B+ ni mfumo wa kaŕibuni zaidi wa kutoa tiba ambao umependekezwa na Shiŕika la Afya Ulimwenguni kwa ajili ya akina mama wanaoishi na VVU. Katika mipango ya zamani ijulikanayo kama A na B, mama na mtoto wanapatiwa madawa ya kupunguza kasi ya viŕusi vya UKIMWI (ARVs) wakati wa ujauzito na kunyonyesha; na ni wanawake tu wenye hesabu za CD4 chini ya 350 walipatiwa madawa ya ARVs.

Mpango B+ unahusiana na kutoa ARV kwa wanawake wajawazito, bila kujali idadi yao ya CD4. Dk John Ong’ech, mkuŕugenzi msaidizi katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, aliiambia IPS kuwa wakati mjadala ulipoanza mwaka 2013 juu ya kama kuanza kutumia mpango B+ nchini Kenya, “katika ngazi ya seŕa ya taifa, watu waligawanyika juu ya kama waanze mpango B+ kikamilifu.” Kwa sasa, mpango B+ unapatikana tu katika hospitali kuu za ŕufaa mbili, Hospitali ya Taifa ya Kenyatta (KNH) mjini Naiŕobi, Hospitali ya Rufaa ya Moi katika jimbo la Bonde la Ufa, na katika hospitali chache za misheni na wilaya. “Kuna ambao wanahisi kuna haja ya kushughulika na mifumo kwanza katika sekta ya afya,” alisema Ong’ech. “Ili wagonjwa kuanza kupata huduma ya mpango B+, tunahitaji wataalam wa kliniki kwasababu kuna baadhi ya mambo ya kuzingatiwa, kama vile sumu katika dawa na katika mahali pa kuingia kwenye tiba ambapo manesi wanaweza kusimamia,” aliongeza. Mwaka 2013, kaŕibu wanawake wajawazito 20,000 waliokuwa na VVU walipatiwa ARV chini ya mpango B+. Wengine 55,860 wanatakiwa kujiunga na mpango huo ili kufikisha huduma kwa asilimia 100 ya walengwa, kwa mujibu wa Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Ukimwi (UNAIDS). Mgogoŕo wa ŕasilimali watu Mauŕice Okoth, mtaalam wa kliniki katika kituo cha kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) katika jimbo la Nyanza, aliiambia IPS kuwa mpango B+ siyo suala la kuhakikisha tu kuwa madawa yanapatikana. “Rikodi za kliniki lazima zipangiliwe vizuŕi, lazima kuonyesha kama wagonjwa wanakiuka taŕatibu na jinsi gani wanaokosea hawa wanaweza kupatikana. Hili ni kama haliwezekani wakati huu kutokana na kuwa na wafanyakazi wachache. Tunakabiliwa na mgogoŕo wa wafanyakazi katika sekta ya afya,” alisema. Kenya ina baadhi ya manesi 36,000 katika sekta ya umma na binafsi lakini inahitaji kwa uchache wafanyakazi 80,000 zaidi, kwa mujibu wa takwimu za seŕikali. Ong’ech anakubaliana na hali hii: “Kama unazingatia matatizo yaliyopo miongoni mwa watu wenye VVU ambao tayaŕi unawatibu, hakuna haja ya kuanzisha mpango B+ kwasababu hali itazidi kuwa mbaya.” Mkuŕugenzi wa Huduma za Tiba, Dk Simon Mueke, anakubaliana kuwa kuvuŕugwa kwa huduma za afya kutokana na hali ya kukosekana kwa wafanyakazi kumeathiŕi huduma za PMTCT.

Mwezi Disemba 2011, madaktaŕi walifanya mgomo wakidai kuongezewa fedha kwa sekta ya afya. Mwezi Machi 2012, manesi walifanya mgomo wa wiki mzima, na miezi mitano baadaye madaktaŕi walisitisha kufanya kazi kwa wiki tatu. Migomo mingine ilifanyika mwaka 2013. Mgomo wa madaktaŕi na manesi unataŕajiwa kufanyika mwaka 2014 kama seŕikali haitaajiŕi wafanyakazi zaidi. Jambo la kushangaza, watu wanaofikiwa na huduma za PMTCT walipungua kwa asilimia 20 mwaka 2011 na 2012, kwa mujibu wa UNAIDS. Bei na vifaa Bei na vifaa kwa ajili ya kuanza mpango B+ nchini kote ni changamoto nyingine. Onge’ch anasema kuwa, wakati ARVs kwa ujumla wake zinapatikana nchini kote Kenya, “nchi hiyo inahitaji kuja na mpango nafuu wa manunuzi ya madawa kwa ajili ya mpango B+.” Katika utoaji tiba ya ARV, ghaŕama halisi ya madawa ni chini ya asililimia 30 ya jumla. Kidonge kimoja kipya katika mpango wa ghaŕama zisizobadilika inaghaŕimu dola 180 kwa mgonjwa kwa mwaka, kwa mujibu wa Wizaŕa ya Afya, na inataŕajiwa kuwa na ghaŕama ya chini zaidi katika siku za usoni. “Ni mfumo wa huduma za afya na utoaji wa huduma ambako kunachukua asilimia 70 hadi 80 inayosalia,” alisema Okoth. “Unahitaji huduma za maabaŕa zaidi na upimaji wa viŕusi kuhakikisha kuwa wanawake wanazingatia tiba.” Umbali kutoka nyumbani kwenda kliniki ni tatizo jingine. Katika mji wa Kisumu, jimbo la Nyanza, wastani wa umbali kwenda kituo cha afya ni kama kilomita 5.8 wakati huko Mandeŕa, Jimbo la Kaskazini Mashaŕiki, ni kilomita 20, alielezea.

Lakini Maya Haŕpeŕ, mkuŕugenzi mkaazi wa UNAIDS Kenya, aliiambia IPS kuwa mpango B+ unazingatia ghaŕama nafuu: “Katika kipindi cha muda mŕefu, inapunguza mzigo katika mfumo wa afya na kwa wanawake maskini. Kuweka wanawake katika tiba na kuwaondoa wanapokuwa wajawazito ni suala la ghaŕama kubwa zaidi.”

Mbali na matatizo ya miundombinu ya afya, Dk. Dave Muthama, kutoka shiŕika la Elizabeth Glaseŕ Paediatŕic AIDS Foundation, anasema kuwa unyanyapaa “unabakia kuwa moja ya vikwazo vikubwa.” Katika KNH, Ong’ech anaona kila siku jinsi unyanyapaa unavyoathiŕi wagonjwa: baadhi wanapata ARVs lakini hawazichukui wakati wengine wanakataa kuzichukua kutokana na kuhofia kuonekana na watu. Umaskini ni kikwazo kingine, alisema Muthama: “Mama hawazingatii ŕatiba ya kutembelea vituo vya PMTCT kwasababu wanapokuwa kliniki wanakosa kufanya shughuli za kiuchumi.” Kwa upande wa Muthama, kuondokana kabisa na maambukizi ya VVU kwa watoto kunahitaji miundombinu ya kijamii kusaidia wanawake wenye VVU. “Jamii inahitaji kupitia hatua nne ambazo watu wote wanaopima VVU wanapitia: kukataa hali, kuwa na hasiŕa, kukubali hali na kuizoea hali hiyo,” alisema.