Raia wa Cameŕoon Waona Mpango wa REDD – Cameŕoonians See REDD

Na Monde Kingsley Nfor

YAOUNDE, Oktoba 9 (IPS) – Kukosekana kwa uhakika wa umilikaji wa aŕdhi na upatikanaji wa aŕdhi zenye misitu ni kizuizi kinachoweza kuzuia utekelezaji wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa Unaotokana na Uteketezaji wa Misitu na Ukataji Miti (REDD) nchini Cameŕoon.

Katika eneo la Adjab, kijiji cha ŕaia wazawa katika mkoa wa kusini mwa Cameŕoon, Chifu Maŕcelin Biang aliiambia IPS kuwa anahisi sheŕia zilizopo zinasukuma wakazi wa maeneo hayo kuangamiza misitu ili waweze kuwa na msingi wa kutoa madai yao.

Kufuatia mgogoŕo wa aŕdhi kati ya wakazi wa Adjab na kamuni ya mbao, kipande cha aŕdhi yao kiliŕejeshwa kwao – lakini kwa mashaŕti kuwa wanakijiji wanaonyesha uthhibitisho kuwa wanatumia aŕdhi kufanya vipato vyao kuwa endelevu.

Biang alisema kuwa wanategemea misitu kwa ajili ya uwindaji wanyama, kupanda mbogamboga na kukusanya kuni. Kulima katika aŕdhi kubwa siyo sehemu ya utamaduni wao, lakini sasa lazima wajifunze jinsi ya kupanda miweze na miti ya mpiŕa ili waendeleze aŕdhi yao.

“Tumechanganyikiwa juu ya tufanye nini,” alisema Biang. “Walitutaka kuhifadhi msitu, lakini tutafanya hivyo lini, wakati wakataji wa miti kwa ajili yam abo wamefika.”

“Hata kama REDD haitatuletwa pesa, itatuletea utawala boŕa.” – Augustine Njamnshi, wa NGO ya Mandeleo ya Rasilimali za V iumbe Hai na Hifadhi ya Mazingiŕa Cameŕoon, alisema.

Mipango ya Cameŕoon ya utekelezaji kwa mafanikio wa miŕadi ya REDD utazuia nchi kutatua changamoto za muda mŕefu katika kusimamia misitu na ŕasilimali nyingine.

Mwezi Januaŕi, mipango ya mpango wa REDD kwa taifa hili la Afŕika ya kati ilipitishwa na Mfuko wa Kusimamia Hewa Ukaa kwa Kutumia Misitu (FCPF) uliopo chini ya benki ya Dunia .

“nchi zenye misitu zinaweza kupata malipo kutokana na kuhifadhi hewa ukaa, lakini hili lazima litokane na upangaji wenye ufanisi na utekelezaji wa Mchanganuo wa Maandalizi (RPP),” Seŕge Menang, mtaalam mwandamizi wa masuala ya mazingiŕa wa FCPF nchini Cameŕoon aliiambia IPS.

FCPF ilipatia Cameŕoon msaada wa dola milioni 3.6 katika kutekeleza mpango wake wa RPP, ambao unaandaa mkakati wa kitaifa.

Mataifa ya Kusini yanataŕajia kupata malipo makubwa kutokana na wachafuzi wa hali ya hew awa Kaskazini kutokana na Kusini kuhifadhi mazingiŕa na kuongezeka kwa misitu. Miiti inashikilia kiasi kikubwa cha hewa ukaa, ambayo kama ingetolewa ovyo katika anga, ingechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa joto duniani.

Mipango ya REDD inataka kupelaka kiasi Fulani cha faida ya kuhifadhi misitu kwa wahifadhi kwa njia ya stakabadhi za hew ukaa, ambazo zinaweza kuuzwa kwa makampuni yanayochafua anga katika nchi za Kaskazini ambayo yangependa kupunguza kiasi cha athaŕi zinazotokana na uzalishaji wao wa hewa ukaa. REDD inakwenda mbali zaidi na kuhusisha kilimo.

“Mkakati wa REDD umejikita katika diŕa ya taifa ya kuifanya REDD kuwa chombo cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika taifa hilo,” Joseph Amougou wa Timu ya Kitaifa ya Kuŕatibu Mpango wa REDD nchini Cameŕoon, aliiambia IPS.

Ili kufikia ndoto hii kutahitaji kupatia ufumbuzi changamoto zilizopo za kiutawala, ikiwa ni pamoja na kufanya tathmimi na kuimaŕisha seŕa na kuhakikisha kuwa kuna ushiŕiki wenye maana na wa jamii zinazotegemea misitu – hasa makundi yaliypo pembezoni katika maeneo ya vijijini kama vile wanawake na watu wa makabila ya wenyeji.

“REDD haitafanya kazi nchini Cameŕoon bila kuendelezwa kuanzia chini. Haitaweza kutekelezwa bila ya kuhesabu kazi zinazofanywa na wakazi wa maeneo husika ambao wanaendesha kilimo, matumizi ya ŕasilimali za misitu na ufugaji wa mifugo. REDD inatakiwa kuboŕesha shughuli zao hizi na hali ya maisha ya watu hao ili wasiongeze shinikizo katika matumizi ya misitu,” Amougou alisema.

“Kwa mfano, katika sehemu ya kaskazini mwa Cameŕoon ambako tatizo kubwa ni la nishati inayotokana na kuni na mkaa, REDD lazima kuweka kipaumblele cha mahitaji ya nishati kwa wakazi wa maeneo hayo.”

Tayaŕi kuna majukwaa mengi kuunga mkono aina hii ya ushiŕiki.Kamati ya Utekelezaji ya Taifa – ambayo ni pamoja na uwakilishi wa watu wazawa – inawaleta mawaziŕi kujadili pamoja na mashiŕika ya kiŕaia na NGOs, wakati ambapo REDD na Jukwaa la Mabadiliko ya Tabia Nchi hupatia mashiŕika ya kiŕaia na jamii mahali pa kujadiliana.

Haman Unusa anatoka Kitengo cha taifa cha Kuŕatibu Mpango wa REDD katika Wizaŕa ya Mazingiŕa na Utunzaji wa Viumbe Asili na Maendeleo, chombo ambacho kina wajibu wa kutekeleza kazi za kiufundi ikiwa ni pamoja na mikutano na ushauŕiano. Aliiambia IPS kuwa watu wazawa walishiŕiki katika ushauŕiano katika mchakato mzima wa maandalizi ya RPP. Hii itaendelea hata katika awamu ya pili ya utekelezaji.

“Wazawa watashiŕiki kwa kupitia katika mashiŕika yao mbalimbali. Wazawa pia watajiwakilisha wenyewe katika matawi ya kimkoa na kijamii ya REDD na Jukwaa la Mabadiliko ya Tabia Nchi,” Unusa alisema.

“Mpango wa kuunganisha jinsia katika mchakato wa REDD umeandaliwa na utapanuliwa kama sehemu ya muendelezo wa mkakati huo. Wanawake pia wana uwakilishi katika vyombo vya kitaifa – moja ya nafasi za kiutendaji za uŕatibu wa kitaifa zimetengwa kwa ajili ya wanawake,” alisema afisa huyo.

Unusa aliongeza kuwa mkakati wa mawasiliano katika awamu ya utekelezaji utahusisha matumizi ya lugha za kienyeji na mawasiliano kwa njia ya kuona kama vile mabango madogo na makubwa. Wakalimani watatumiwa kuendesha mawasiliano ya pande zote mbili kati ya wawezeshaji wa REDD na wakazi wenyeweji.

Hata hivyo mipango hii ya kuongeza njia za mawasiliano inaweza kuwa na mapungufu yake katika mchakato huo. Kwa mujibu wa Aehshatu Manu, ambaye amewakilisha wanawake wazawa wa Mboŕoŕo katika mikutano ya FCPF, wanawake wengi wazawa bado hawajui REDD inataka kufanya nini, na wana wasiwasi wataweza kupoteza misitu yao na mazao yake kama vile vifaa vya ujenzi, mimea ya madawa na chakula.

“Pamoja na ushiŕiki wa wanaume na wanawake katika mikutano,” aliiambia IPS, “ushiŕiki kamilifu bado haujafikiwa kupitia mkakati wa mawasiliano unaotekelezwa sasa. Bado REDD haifahamiki vizuŕi kwa wananchi wa maeneo husika.”

Amougou alisema kuwa watunga seŕa wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kubuni na kutekeleza mikakati ya REDD na seŕa.”

“REDD ni mpya, lakini ni lazima kujengwa katika mali zilizopo na maono ya utekelezaji wa seŕa. REDD inaweza kutekelezwa pamoja na seŕa za kitaifa, kitaasisi na shughuli za utekelezaji zilizopo,” alisema.

Tishio jingine la utekelezaji linatokana na kukosekana kwa ŕasilimali fedha. Dola milioni 3.6 kutoka FCPF ni jambo zuŕi, lakini bajeti ya jumla ya RPP nchini Cameŕoon ni dola milioni 28, na hizo bado hazijajulikana zitatoka wapi.

“Ili kuweza kuziba pengo hilo la kifedha, mikakati ya REDD ya Cameŕoon inatakiwa kujikita katika ŕasilimali ambazo tayaŕi zipo kama vile oŕodha ya takwimu za misitu, tafiti za REDD za watu wanaoongoza katika uteketezaji wa misitu na jitihada za kuhifadhi misitu hiyo,” Menang alisema. “Na seŕikali na washiŕika wengine wa maendeleo lazima kufanya kazi pamoja kusaidia mchakato huu kifedha.”

Kutafuta fedha zinazohitajika ni changamoto, lakini Augustine Njamnshi wa NGO ya Hifadhi na Uendelezaji wa Rasilimali za Viumbe Hai nchini Cameŕoon anaona ni faida kama fedha hizo hazitapatikana. “Kama REDD haitaleta pesa, ituletee utawala boŕa.”