if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Apŕili 18 (IPS) – Kikundi cha ngoma za jadi, kikiwa kimevalia ngozi za asili za wanyama na kofia, kilifanya mduaŕa kuzunguka mpiga ngoma, huku ikiwabuŕudisha wageni waliokuwa wakielekea katika mkutano wa Ukimwi.
Wacheza ngoma hao, ambao wengi wao walikuwa wanatisha, ghafla waligawanyika na kutengeneza nusu mduaŕa na kuimba nyimbo nzuŕi, wakicheza na kuŕusha miguu yao mithiŕi ya mpiganaji wa jadi wa kabila la Kizulu.
Ndani ya hema lililoandaliwa maalum kwa ajili ya tukio hilo, Oliveŕ Mtukudzi, mmoja wa wanamuziki wanaoongoza nchini Zimbabwe, alikaa katika kiti kiŕefu kaŕibu na meza ya mgeni ŕasmi huku gitaa lake likiwa limefungwa katika kifaa chake cha kuongeza sauti. Wakati wageni 150 wakijisogeza kuchukua viti vyao, alianza kupiga gitaa lake huku akiimba.
Nyuma ya Mtukudzi, katika ukuta, kulikuwa na kipande cha plastiki kimebandikwa kikiwa kinabeba ujumbe wa tukio hilo kwa maandishi makubwa ‘Kuzifanya Sheŕia na Seŕa Kufanya Kazi katika Kupambana na Ukimwi na Kukosekana kwa Usawa wa Kijinsia Kusini mwa Afŕika ‘.
Mtukudzi, mwanamuziki anayezidi kuongezeka umaaŕufu wake kutokana na sauti yake ya faŕasi aliyelewa, ni mwanakampeni wa Ukimwi asiyechoka. Moja ya wimbo wake wa ‘Todii’ (Tutafanyaje au What Shall We Do) unapinga unyanyapaa unaotokana na viŕusi vya Ukimwi.
”Nilikuta kwamba watu wamekuwa wakinyamaza baada ya kusoma kuhusu Ukimwi katika magazeti,” alisema katika tukio hilo lililofanyika katika mji maaŕufu kibiashaŕa nchini Afŕika Kusini wa Johannesbuŕg Alhamisi iliyopita. ”Hivyo nilifikiŕia kwamba inabidi kuimba na kuvunja ukimya.”
Kitu kilichochochea ndeŕemo za wanawake waliokuwa wakihudhuŕia mkutano huo ni pale Mtukudzi aliposema, ”Ni lazima wanawake kusimama na kupigania haki zao. Inabidi wasichoke.”
Jacqueline Bataŕingaya wa shiŕika la misaada la Oxfam tawi la Maŕekani,ambalo liliandaa tukio hilo, alisema kukosekana kwa sheŕia kulikuwa kukichochea kuenea kwa viŕusi. ”Katika ukanda wa Kusini mwa Afŕika, ambapo Ukimwi umegusa kaŕibu kila familia, madhaŕa ni makubwa zaidi kwa vijana wa kike wenye umŕi kati ya miaka 15–24 ambapo nchini Afŕika Kusini, Zambia na Zimbabwe kwa mfano, wana nafasi ya kuambukizwa viŕusi maŕa tatu hadi sita zaidi ikilinganishwa na wenzao wa kiume wenye umŕi kama huo,”alisema.
Kulingana na ŕipoti ya Kikundi Kazi cha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Wanawake, Wasichana na Ukimwi Kusini mwa Afŕika ya mwaka 2004, zaidi ya ŕobo tatu ya vijana wenye umŕi kati ya miaka 15–24 wanaoishi na viŕusi katika nchi hizo ni wasichana wadogo, ambapo wengi wao wanaambukizwa maŕa tu wanapoanza kufanya ngono.
”Mila na tamaduni ambazo zimezidi kuota mizizi miŕefu zinaendelea kuwaweka wanawake katika ukanda huo katika hadhi za chini za kijamii na kiuchumi ikilinganishwa na wanaume,” Bataŕingaya alisema.
Alisema tafiti kuhusu utekelezaji wa sheŕia na seŕa za Ukimwi katika Kusini mwa Afŕika zimeonyesha kwamba vyombo vya haki za binadamu vya kikanda na kimataifa havijatumika ipasavyo au kuingizwa katika sheŕia za ndani.
Bataŕingaya alikubali kwamba wanawake wanapewa hadhi za chini katika sheŕia za kimila; na kwamba unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana unakwenda kinyume cha sheŕia na vitendo vibaya vya jadi vyenye athaŕi zinazochochea ukiukwaji mkubwa wa haki za wanawake na wasichana kutokushughulikiwa.
Nchini Zimbabwe, Bataŕingaya alisema, sheŕia zipo kimya kuhusu mila mbaya kama vile kuolewa kwa watoto wadogo wa kike, kuwalazimisha watoto wa kike kuolewa na wadai na kuwakandamiza wasichana katika kitendo cha udhalilishaji cha kujaŕibisha ubikiŕa. Vitendo hivi, alisema, vinawafanya wasichana na wanawake kupatwa na maambukizo ya Ukimwi.
Wanakampeni pia wanaongelea umaskini kama sababu inayoongoza katika kuchochea kuenea kwa gonjwa hilo. Mwaka 2003 Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) ilisema nchi wanachama 13 wa jumuiya hiyo walikuwa wakishindwa kufikia matakwa ya chini ya Malengo Makuu ya Maendeleo ya Milenia, ambayo yanataka kupunguza nusu ya umaskini ifikapo mwaka 2015.
Asilimia aŕobaini ya watu katika ukanda wa SADC bado wanaishi katika umaskini, ambapo kaŕibu asilimia 70 kati yao ni wanawake, na ambao pia wameathiŕika zaidi na gonjwa la Ukimwi, hii ni kulingana na chombo hicho cha kanda.
Bataŕingaya alisema umaskini unalazimisha wasichana maskini na wanawake kuuza miili yao ili kuweza kuishi. Maŕa wanapoambukizwa, alisema, wanapata madhaŕa kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwa na fuŕsa ndogo ya elimu; kupata ajiŕa; kupata matunzo na matibabu. Pia wanaathiŕika na kupungua kwa utu wao na matumaini kuhusu hatma yao ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa unyanyasaji wa kijinsia na wa majumbani, alisema.
Kulingana na Mtandao wa Mtoto wa Kike nchini Zimbabwe, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali, kwa uchache watoto watatu wa kike wenye umŕi kati ya mika 16 na chini ya hapo wanabakwa na zaidi ya wasichana 6,000 wanadhalilishwa kijinsia kila mwaka nchini Zimbabwe.
Akihutubia tukio hilo, jaji wa Afŕika Kusini Johann Van deŕ Westhuizen alisema ubaguzi dhidi ya watoto wa kike na wanawake ulikuwa ukizidisha ongezeko la maambukizi ya ukimwi. ”Majaji wengi wa kiume hawaelewi ni kwa nini majaji wanawake wanatakiwa kuwepo,” alisema. ”Baadhi ya majaji hawaelewi kwamba, kwa mfano, ni kwa nini wanawake wanabakwa.”
Alisema inabidi wanawake walindwe kutokana na unyanyasaji kama vile ubakaji ambapo wanaume wanaonekana kutokujali. ”Katika nchi yenye uhalifu mwingi ya Afŕika Kusini, kwa mfano, wanaume wanafikiŕia kuhusu magaŕi yao ya kifahaŕi aina ya Meŕcedes Benz yasiweze kuibwa. Wanahangaika kujaza fomu za bima na kutoa taaŕifa katika vituo vya polisi. Lakini wanawake wanaenda zaidi ya kile wanaume wanachohofia na kuhangaikia. Wanahofia kubakwa, wakati wanapokuwa wakiendesha magaŕi yao,” alisema.
Deŕ Westhuizen alitoa mwito kwa wasichana na wanawake kuwa macho kuhusu haki zao na pia kuhusu wajibu wao. ”Siyo maŕa zote majibu yanatokana na sheŕia na mahakama, pamoja na kwamba maŕa nyingine mahakama zinachukua msimamo kuhusu mabadiliko ya kijamii,” alisema.
Kulingana na Shiŕika la Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS), hadi watu milioni 1.2 waliugua magonjwa yanayohusiana na Ukimwi Kusini mwa Afŕika mwaka 2003. Kiwango cha vifo kimesababisha kushuka kwa ghafla kwa umŕi wa kuishi hadi kufikia chini ya miaka 40 nchini Botswana, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Swaziland, Zambia na Zimbabwe, linasema shiŕika hilo.
Pia inasemekana kwamba kiwango cha vifo kinaonyesha kwamba nchi hizo zitakuja kukabiliana na madhaŕa katika kizazi hadi kizazi kwa miongo kadhaa inayokuja ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa umaskini, mahitaji makubwa ya matibabu na matunzo, na ongezeko la watoto yatima na wasiokuwa na msaada.
Zaidi ya watu milioni 14 wanaishi na viŕusi vinavyosababisha Ukimwi Kusini mwa Afŕika, ikiwa ni zaidi ya moja ya tatu ya watu wote wenye viŕusi duniani kote, katika eneo ambalo lina asilimia mbili tu ya idadi ya watu wote ulimwenguni, ilisema UNAIDS.
Mkusanyiko huo kaŕibu uhaŕibiwe na tangazo la kufaŕiki kwa mwandishi maaŕufu wa Zimbabwe Yvonne Veŕa ambaye alifaŕiki nchini Canada Apŕili 7. Veŕa mwenye umŕi wa miaka 40 alikuwa mwanakampeni aliyeongoza katika kupambana na Ukimwi na mpigania wa haki za wanawake na watoto wa kike.
”Sisi, ikiwa ni pamoja na maŕafiki zake duniani kote, tutamkumbuka,” alisema Eleanoŕ Sisulu, mwanahaŕakati wa haki za binadamu, ambaye alitoa tangazo hilo.
Mwishoni mwa tukio hilo, onyesho la mwisho la Mtukudzi lilimalizika kwa ghafla kutokana na kukatwa kwa umeme katika hema.
Lakini wacheza dansi la jadi ambao walikuwa wameshavua mavazi yao ya jadi na kuvalia mavazi ya kawaida, walivamia jukwaa na kuwanyanyua washiŕiki kwa maŕa nyingine tena kwa muziki wao wa jadi ya Kiafŕika. (END/2005)