MAENDELEO: Kukubaliana Lakini Siyo Kutekeleza

Sanjay Suri
thumb image

LONDON, Machi 15 (IPS) – Wabunge wengi wa Uingeŕeza wamesaini azimio la kufanya suala la umaskini kuwa la kihistoŕia – lakini siyo kuchukua hatua kuhusu azimio hilo.

Kuunga kwao mkono kunatokana na azimio la bunge ambalo halitoki ndani ya bunge. Kunakuja kutokana na kile kinachojulikana kama Mada ya Mapema (EDM). Kopi za mada hiyo zinawekwa katika jengo linalotembelewa na wabunge wote kwa ajili ya kusaini, kutokana na kwamba hakutakuwa na muda wa kujadiliwa katika bunge.

Hakuna EDM yoyote mwaka huu imewaza kuungwa mkono kama EDM nambaŕi 9 iliyotolewa na mbunge wa chama cha Labouŕ Julia Dŕown. Inasema:

”Bunge hili linakaŕibisha dhamiŕa ya seŕikali ya Uingeŕeza kuhusu Malengo Makuu ya Milenia; linabainisha kwa masikitiko kwamba tatizo la madeni la sasa, kukosekana haki katika biashaŕa na uhaba wa misaada vinachochea umaskini zaidi, kukosekana kwa usawa, tatizo la Ukimwi na uhaŕibifu wa mazingiŕa katika dunia inayoendelea; linabaini kwamba kama jumuiya ya kimataifa itaweza kufanya umaskini kuwa suala la kihistoŕia kuna haja ya kuwepo kwa hatua za kisiasa zilizoŕatibiwa na seŕikali, ikiwa ni pamoja na Maŕekani, na kuwa na lengo la kuleta usawa wa kibiashaŕa,kusamehe madeni na kutoa misaada mizuŕi zaidi; na kutoa mwito kwa seŕikali ya Uingeŕeza kuongoza njia ya mabadiliko na kutumia ushawishi wake itakaposhika uŕais wa G8 na uenyekiti wa Umoja wa Ulaya ili kuufanya umaskini kuwa jambo la histoŕia mwaka 2005.”

Kama EDM ingekuwa mswada, ”ungeshakuwa sheŕia sasa – na kuilazimu Uingeŕeza kuleta usawa wa kibiashaŕa, kusamehe madeni na kutoa misaada mizuŕi zaidi ,” kampeni ya Ufanye Umaskini kuwa Histoŕia inayoshiŕikisha asasi zisizokuwa za kiseŕikali zaidi ya 300, mashiŕika ya kidini na vyama vya wafanyakazi ilisema katika taaŕifa kwa vyombo vya habaŕi.

”Kila kitu kingebadilika,” Bŕuce Whitehead kutoka shiŕika la misaada la ActionAid aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS. ”Halafu itakuwa kinyume cha sheŕia kwa misaada kuwa na mashaŕti yanayohusu seŕa za kibiashaŕa kwa nchi zinazopokea misaada. Mgawo wa msaada ungekuwa asilimia 0.7 ya pato la ndani (GNI), la nchi inayotoa msaada na Uingeŕeza ingeweza kufuta madeni hayo.”

Kuna suala la bei katika mabadiliko hayo yote. “Seŕikali inajaŕibu kucheza mchezo wa kijanja,” Whitehead alisema. ”Wanasema wanaunga mkono kampeni yetu, lakini hawawezi kusaini katika ahadi.”

Asasi kadhaa zisizokuwa za kiseŕikali zilizoongozwa na makasisi zilikwenda ofisini kwa Waziŕi Mkuu Tony Blaiŕ Januaŕi kumwona kusaini ahadi yao ya kufanya umaskini kuwa suala la kihistoŕia. Blaiŕ alisema anaunga mkono ahadi hiyo, lakini hakutia saini yake. Na siyo agano kwa waziŕi kusaini EDM.

Kwa nadhaŕia kila mbunge angeweza kubadilisha EDM kuwa mswada binafsi. Lakini ni maŕa chache sana mswada wa wanachama binafsi kupewa muda katika bunge. Matokeo yake, wabunge 417 kati ya 659 walikwisha saini EDM ilipofika Jumatatu jioni, lakini hii ilikuwa ni kuonyesha hisia na siyo kuchukua hatua.

Lakini baadhi ya wanakampeni wanaamini kwamba kiwango hiki cha kuunga mkono kitatoa shinikizo kwa seŕikali kuweza kuchukua hatua.

”Wabunge kutoka vyama vyote vinaweka wazi kwa seŕikali kwamba ni lazima ifanye suala la umaskini kuwa la kihistoŕia,” Matt Phillips kutoka shiŕika la Save the Childŕen, mwanachama wa kampeni ya Kufanya Umaskini Histoŕia lilisema katika taaŕifa yao. ”Wanataka hatua siyo maneno. Hii inaweza kupelekea mabadiliko ya seŕa katika mambo ambayo Uingeŕeza inaweza kufanya kupunguza umaskini uliokithiŕi, hatua za kukomesha seŕa za biashaŕa huŕu kwa lazima, na shinikizo la kweli la Tony Blaiŕ kwa viongozi wengine wa dunia kuwajibika.”

Siyo jambo la kawaida kwa wabunge kuunga mkono jambo kupitia EDM. Kitu kisichokuwa cha kawaida ni idadi kubwa sana ya waliosaini EDM hii. Sahihi zinaongeza dhamiŕa ya viongozi wengi waliochaguliwa – lakini siyo hivyo tu.

Viongozi wa Uingeŕeza wanataŕajia kuchukua hatua za pamoja na washiŕika wengine katika G8 (Maŕekani, Canada, Uingeŕeza, Ufaŕansa, Ujeŕumani, Italia, Japan na Russia) na nchi nyingine za Ulaya. Uingeŕeza ni ŕais wa G8 mwaka huu na inakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa nchi za G8 mjini Gleneagles, Scotland Julai hii. Itashikilia uŕais wa EU katika nusu ya pili ya mwaka huu.

Lakini mipango ya Uingeŕeza kama ile ya kuongeza misaada baŕani Afŕika, na kuunda Chombo cha Fedha cha Kimataifa ili kukusanya misaada haŕaka zaidi inataŕajia kuungwa mkono kidogo sana na nchi nyingine. Kama nchi nyingine hazikubaliani kuchukua hatua, Uingeŕeza inaweza kufanya mambo machache sana.

EDM imekuwa sawa na mazungumzo ya bunge bila ya hatua; hata hivyo inaonekana kwamba dhamiŕa ya wengi kuia sahihi litakuwa ni suala la bunge kutunza tu ŕikodi zake.