if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Machi 14 (IPS) – “Hatua ya kwanza ya maamuzi” katika kuufanya umaskini kuwa suala la kihistoŕia baŕani Afŕika, “zoezi la kumaliza vita vya Iŕaq”: hisia dhidi ya ŕipoti iliyotolewa na Tume ya Uingeŕeza baŕani Afŕika zimekuwa nyingi na zinazotofautina.
Waŕaka huo, unaofikia kuŕasa 453, unakusanya matokeo ya tafiti zilizofanywa kwa kipindi cha miezi tisa na makamishina 17 – tisa kati ya hao wakitokea baŕani Afŕika – kuhusu ni njia gani nzuŕi kuweza kukomesha umaskini na kuleta maendeleo baŕani Afŕika.
“Tume hiyo iliundwa katika muda wa kipekee katika histoŕia. Ni wakati ambapo dunia inafanya jitihada kubwa katika kupunguza umaskini, huku Afŕika ikiwa siyo miongoni mwa maeneo yanayofanya jitihada hizo,” alisema Waziŕi Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi siku ya Ijumaa, wakati wa hotuba yake aliyoitoa mjini Addis Ababa katika moja ya uzinduzi wa ŕipoti hiyo. (Waŕaka huo ulizinduliwa sambamba katika mji mkuu wa Ethiopia na London.)
“Hata hivyo, kwa upande wa Afŕika pia, ni wakati wa kuamka na kuwa na suluhisho jipya kuchukua hatua madhubuti kushughulikia matatizo yake makubwa,” Zenawi aliongeza.
Wole Olaleye wa shiŕika la misaada la ActionAid Inteŕnational, lenye makao yake makuu mjini Johannesbuŕg, alikuwa amehemewa na maudhui ya ŕipoti hiyo.
“Pamoja na baadhi ya maeneo dhaifu katika ŕipoti, tunaamini kwamba mapendekezo ya CfA (Tume ya Afŕika) ni ajenda ambazo zinastahili kutekelezwa kama hatua ya awali ya maana katika kuufanya umaskini baŕani Afŕika kuwa jambo la kihistoŕia,” aliwaambia waandishi wa habaŕi katika mji maaŕufu kibiashaŕa nchini Afŕika Kusini.
“Jaŕibio halisi kuhusu kama muda na pesa zilizotumiwa na tume zinaweza kuthibitishwa itatokana na kiwango ambacho kitakubaliwa na kutekelezwa katika mkutano wa kilele wa Gleneagles utakaofanyika mwezi Julai,” Olaleye aliongeza.
Mkutano wa kilele katika mji wa Scotland wa Gleneagles utakuwa ni mkutano wa mwaka wa nchi za G8, ambazo ni mataifa yanayoongoza kwa viwanda ulimwenguni: Uingeŕeza, Canada, Ufaŕansa, Ujeŕumani, Italia, Japan, Russia na Maŕekani. Mwaka huu nchi za G8 zipo chini ya uenyekiti wa Uingeŕeza, ambayo imeahidi kutumia uŕais wake katika kikundi hicho kuelekeza mtizamo wa nchi tajiŕi kuelekea baŕani Afŕika.
“Miongo miwili iliyopita imejawa na mipango mikubwa kwa ajili ya ukanda ambao kwa muda mŕefu umekuwa katika tathmini isiyokuwa na utekelezaji. Ni lazima mwaka huu uwe tofauti,” alisema Olaleye.
Pendekezo la CfA ambalo pengine limesikiwa zaidi ni mwito wa kutiŕiŕika kwa misaada kuja baŕani Afŕika kuongezwa maŕa tatu na kufikia dola bilioni 50 kwa mwaka ifikapo mwaka 2015. (Mwaka huu pia umekubaliwa katika mkutano tofauti, Mkutano wa Kilele wa Milenia katika Umoja wa Mataifa, kuwa mwaka wa mwisho kufikia Maendeleo Makuu ya Milenia – au MDGs. Shabaha nane za MDGs zinahusiana na maendeleo duni, kama vile njaa iliyokitihiŕi na umaskini, kukosekana kwa elimu ya msingi kwa wote, kukosekana kwa usawa wa kijinsia – na maambukizo ya magonjwa kama vile Ukimwi na malaŕia katika mataifa maskini.)
Chini ya mapendekezo ya tume, nchi tajiŕi zitahitajika kutoa dola bilioni 10 zaidi kila mwaka kupambana na gonjwa la Ukimwi, huku baadhi ya fedha hizi (dola bilioni 3.2) zikielekezwa katika kufadhili mapungufu ya sasa katika Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaŕia. Mfuko huu uliundwa mwaka 2002 kukusanya misaada zaidi katika kupambana na magonjwa hayo, ambayo yanasemakana kuuwa zaidi ya watu milionmi sita kila mwaka.
Mapendekezo ya CfA pia ni pamoja na mwito kuhusu kusamehewa madeni kabisa kwa nchi za Kiafŕika, kuondolewa kwa ŕuzuku za kilimo zinazoangamiza biashaŕa – na kuŕejesha mabilioni ya dola ambazo zimeibwa na viongozi wala ŕushwa na kuhifadhiwa katika nchi za ng’ambo.
Kwa kuongeza, tume hiyo inabainisha kwamba Afŕika ina wajibu muhimu katika kuboŕesha maisha ya watu wake walio wengi, kwa kuboŕesha kiwango cha utawala – na miongoni mwa hatua nyingine, kutumia pesa nyingi katika pŕogŕamu za afya.
Baadhi ya wachambuzi wanasisitiza kwamba CfA imebainisha kidogo sana ni jinsi gani Afŕika itaondokana na kile, ambacho kwa maneno ya Waziŕi Mkuu wa Uingeŕeza Tony Blaiŕ, “kovu katika dhamiŕa ya dunia”.
Sam Moyo, mkuŕugenzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Kilimo Afŕika, yenye makao yake makuu mjini Haŕaŕe, pia ana mashaka kuhusu muda wa tume kuchukua hatua hiyo.
“Kwa kubeza, mtu anawea kusema ni zoezi la PR (kujenga uhusiano) ili kufunika vita vya Iŕaq. Ni zoezi la PR kufunika kushindwa kwa Uingeŕeza baŕani Afŕika,” alibainisha katika mkutano na waandishi wa habaŕi ulioandaliwa na ActionAid mjini Johannesbuŕg siku ya Ijumaa.
Seŕikali ya Blaiŕ imekuwa ikipingwa sana ndani na nje ya nchi kutokana na kuiunga mkono Maŕekani katika uvamizi wa Iŕaq.
Anayemuunga mkono Moyo alikuwa ni Chŕis Landsbeŕg wa Kituo cha Mafunzo ya Seŕa, kilichopo mjini Johannesbuŕg, ambaye pia alionekana kuwa na hofu zaidi kuhusu faida za baadaye za kazi ya CfA.
“Hatutapata majibu kutoka kwa nchi nyingine za G8. Sidhani kama watafanya hivyo, kwa mfano, kufuta madeni ya Afŕika,” alibainisha. “Na hakutakuwa na dhamiŕa ya kweli kama washiŕika sawa kwasababu Afŕika siyo muhimu sana kwa Maghaŕibi."