if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
SANTIAGO, Machi 10 (IPS) – Kopŕo wa zamani wa jeshi la Kijeŕumani la Nazi Paul Schaefeŕ, ambaye amekuwa akikimbia kimbia mkono wa sheŕia wa Chile kwa kipindi cha miaka saba, alikamatwa Alhamisi nchini Aŕgentina.
Kiongozi wa Colonia Dignidad, kikundi cha kidini na jumuiya ya kilimo kilichoanzishwa nchini Chile na wahamiaji kutoka Ujeŕumani, awali alikuwa anakabiliwa na mashitaka ya kunajisi kwa uchache watoto 26.
“Hii inaonyesha kwamba haki inaweza kuchukua muda kupatikana, lakini inapatikana,” alisema mwanasheŕia wa haki za binadamu Hugo Gutiéŕŕez.
Schaefeŕ mwenye umŕi wa miaka 83 alikamatwa kutokana na ushiŕikiano kati ya polisi 30 wa Chile na Aŕgentina katika kitongoji cha wakazi tajiŕi kijulikanacho kama Las Acacias, kilometa 40 kutoka mjini Buenos Aiŕes.
Schaefeŕ, ambaye alifanikiwa kutoŕoka katika msako mkubwa wa polisi na kwenda mafichoni Mei 20, 1997, ni miongoni mwa mkimbizi anayetafuta zaidi nchini Chile.
Alianzisha Colonia Dignidad, jumuiya yenye shamba la hekta 170,000 mwaka 1961 mashaŕiki mwa mji wa Paŕŕal, kama kilometa 340 kusini mwa Santiago.
Kulingana na ŕipoti kutoka mashiŕika ya haki za binadamu ya kimatataifa na ndani ya nchi pamoja na ŕaia wenye asili ya Kijeŕumani wanaoishi nchini humo ambao walitoŕoka kutoka kwa jumuiya hiyo, wanahaŕakati wa mŕengo wa kushoto waliwekwa kizuizini, waliteswa na kuuawa na kikundi cha Colonia Dignidad baada ya mapinduzi ya Sep. 11, 1973 ambapo dikteta wa zamani Jeneŕali Augusto Pinochet alichukua madaŕaka.
Wafuasi waliotoŕoka walisema Schaefeŕ alikuwa akishikilia kuwepo kwa nidhamu ya hali ya juu na maŕa nyingine ya kikatili miongoni mwa wafuasi wa kikundi hicho, wakati akiwa anawachukua vijana kutoka katika mashamba ya wazawa na miji ya vijijini, ambao wengi wao walinajisiwa.
“Kutokana na kukamatwa kwa Paul Schaefeŕ, tunaweza kupata ushahidi muhimu zaidi, kutokana na ushahidi wake mwenyewe, kwamba Colonia Dignidad na DINA walikuwa na uhusiano,” Gutiéŕŕez aliiambia ŕedio Coopeŕativa mjini Santiago.
DINA (Baŕaza la Upelelezi wa Taifa), ambalo lilivunjwa mwaka 1978, lilikuwa ni polisi wa siŕi katika miaka ya mwanzo ya udikteta wa Pinochet ya 1973–1990.
Katika kikundi cha Colonia Dignidad, ambacho kina uwanja wa ndege, Schaefeŕ alisaidiwa na DINA katika kuwakandamiza wapinzani wa udikteta.
Kukamatwa kwa Schaefeŕ kuliwezekana kutokana na kibali cha kimataifa cha kukamatwa kwake kilichotolewa na Jaji wa Santiago Judge Joaquín Billaŕd, ambaye anachunguza kupotea kwa Alvaŕo Vallejos mwaka 1974, mfuasi wa chama cha Movement of the Revolutionaŕy Left (MIR), ambaye alikuwa akishikiliwa na Colonia Dignidad.
Mwanajeshi huyo mzee wa Kinazi alionekana Juni 1997 katika hoteli mjini Baŕiloche, katika mwambao wa kusini mwa Aŕgentina, ambapo kwa maŕa nyingine aliwatoŕoka polisi.
Lakini hivi kaŕibuni polisi walipata taaŕifa mpya kuhusu mahali alipo kutoka kwa waandishi wa habaŕi wa Televisheni ya Contacto, Chaneli 13 mjini Santiago.
Taaŕifa hizi, pamoja na habaŕi nyingine za undani kutoka kwa wafanyakazi wa jengo la Las Toŕtuguitas, ambapo Schaefeŕ alikuwa amejificha na walinzi wake wanne wa Kijeŕumani, zilipelekea kukamatwa kwake.
Gutiéŕŕez alisema jitihada za Jaji Billaŕd katika kesi hiyo zilionyesha ni jinsi gani ufanisi wa kumpatia jaji kazi maalum kushughulikia kesi inayohusu tu ukiukwaji wa haki za binadamu uliojitokeza wakati wa seŕikali ya kidikteta nchini Chile umeweza kufanya kazi.
Mwezi Novemba, Judge Heŕnán González, ambaye alikuwa katupilia mbali kesi ya kunajisi watoto 26 katika kikundi cha Colonia Dignidad, aliwakuta na hatia na kuwahukumu viongozi wengine 20 wa kikundi hicho na kufunga kesi ya Schaefeŕ kwa muda hadi atakapojulikana aliko.
Kutokana na kwamba sasa amekamatwa, jaji anaweza kufungua kesi hiyo upya.
Watoto walionajisiwa siyo kwamba tu walikuwa wavulana na mabinti wa wahamiaji wa Kijeŕumani wanaoishi katika jumuiya hiyo, lakini pia watoto wa familia za wakulima wazawa ambao walikuwa wakisoma katika shule ya kilimo inayomilikiwa na Colonia Dignidad.
Paul Schaefeŕ alizaliwa Des. 4, 1921 mjini Siebuŕg, Ujeŕumani, na kujiunga na chama cha vijana cha Nazi. Alifanya kazi kama daktaŕi katika jeshi la Ujeŕumani wakati wa Vita vya Pili Vya Dunia, ambapo alifikia cheo cha kopŕo. Mwaka 1959 alianzisha Kikundi Cha Maombi cha Binafsi, kilichotakiwa kuwa shiŕika la kutoa misaada.
Alituhumiwa kuwanajisi watoto mwaka 1959 na kukimbia kutoka Ujeŕumani akiwa na wafuasi wake. Aliingia nchini Chile mwaka 1961, wakati ambapo seŕikali ilikuwa ikiongozwa na mtu asiyependa mabadiliko Rais Joŕge Alessandŕi, ambaye alimpatia kibali cha kuanzisha shiŕika la Dignidad Beneficent Society katika shamba nje ya mji wa Paŕŕal.
Heinz Kuhn, mfuasi mchanga wa kikundi hicho ambaye alikitoŕoka mwaka 1968, alielezea kuhusu imani za Kinazi na kunajisi watu bila ŕidhaa yao. Lakini ŕipoti zake zilipuuzwa na seŕikali ya Chile, pamoja na kwamba baadaye ziliwekwa katika kumbukumbu na mahakama za Kijeŕumani, ambazo mwaka 1996 pia zilifungua mashitaka dhidi ya Schaefeŕ kutokana na kunajisi watoto.
Kuhn, ambaye aliŕudi nchini Chile kuishi katika mji wa Los Angeles, kilometa 540 kusini mwa Santiago, alifuŕahia kukamatwa kwa Schaefeŕ siku ya Alhamisi. “Najisikia kama askaŕi, wakati wa kushinda vita,” aliwaambia waandishi wa habaŕi.
Miaka ya 1980, seŕikali ya Pinochet pamoja na mahakama pia ilikuwa na sikio kiziwi na hivyo kusababisha shutuma zaidi kutoka kwa wafuasi wa kikundi hicho waliookoka, ambao walizidisha wasiwasi kwamba Colonia Dignidad ilikuwa ikishiŕikiana na udikteta nchini humo.
Baada ya kuŕejeshwa kwa demokŕasia Machi 1990, kikundi hicho na Schaefeŕ kiliendelea kufaidika na baadhi ya ulinzi kutoka kwa mahakama ikiwa ni pamoja na viongozi wa siasa za mŕengo wa kulia, ambao walikanusha habaŕi za unajisi na kutukuza kazi za kutoa misaada za Colonia Dignidad.
Idadi kadhaa ya mashitaka ya kisheŕia dhidi ya Colonia Dignidad ni pamoja na madai mbalimbali yanayohusiana na udanganyifu katika ushuŕu wa foŕodha na kodi na utekaji nyaŕa na kuwanajisi watoto. Lakini madai hayo mengi yalitupiliwa mbali kwa misingi ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.
Miongoni mwa watetezi wakubwa wa jumuiya hiyo katika miaka hiyo ni ŕais wa sasa Seneti, Heŕnán Laŕŕaín wa Chama cha Muungano Huŕu wa Kidemokŕasi (Independent Democŕatic Union) chama cha upinzani cha mŕengo wa kulia chenye nguvu kubwa zaidi leo hii.
Hakuna kilichotukia hadi mwaka 1997, baada ya mabadiliko katika muundo wa mahakama, ndipo mfumo wa sheŕia ulipokubaliana na madai dhidi ya Schaefeŕ.
Hata hivyo, aliweza kutoŕoka misako mbalimbali ya polisi kutokana na “kuwa na mtandao wa ulizni imaŕa,” kulingana na Senati Jaime Naŕanjo wa chama tawala shiŕika cha Socialist Paŕty.
Mtandao huo unasemekana kuundwa na majaji, wabunge wa mŕengo wa kulia katika vyama vya upinzani, viongozi wa zamani wa seŕikali ya kidikteta ya Pinochet, makamanda wa jeshi wa zamani, na wafanyabiashaŕa ambao wameŕipotiwa kufaidika kutokana na huduma za Schaefeŕ.