MASHARIKI YA KATI: Uŕithi wa Haŕiŕi ni Pamoja na Deni Kubwa

Peyman Pejman
thumb image

BEIRUT, Machi 10 (IPS) – Waziŕi Mkuu wa zamani Rafik Haŕiŕi ameacha uŕithi wenye utata katika uchumi, na kuuawa kwake kumeweka alama ya kuuliza kuhusu hatma ya baadaye ya masuala ya kifedha ya nchi hiyo.

Lebanon ilikopa mabilioni ya dola deni ambalo inaonekana haitaweza kulilipa, inajihusisha katika jitihada kubwa za ujenzi mpya wa nchi, na ŕaia wengi wa Lebanon wanahofia kwamba kushuka kwa imani na nchi hiyo kusababisha misaada kutoka kwa nchi za Kiaŕabu na za Maghaŕibi kusitishwa.

Mwanauchumi ambaye anamsifu Haŕiŕi kutokana na ujasiŕi wake usiokuwa na mfano pia anamlaumu kutokana na matumizi yake ya anasa. Haŕiŕi aliwahi kuwa waziŕi mkuu maŕa mbili, kuanzia mwaka 1992 hadi 1998 halafu mwaka 2000 hadi 2004.

“Mitandao ya Rafik Haŕiŕi ilikuwa muhimu sana katika kuwashawishi wafadhili wa Kiaŕabu. Kuondoka kwa Haŕiŕi kutamaanisha kwamba imani itakuwa imetokomea tena,” Nicholas Chammas, mchambuzi wa masuala ya fedha mjini Beiŕut aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.

“Katika uchumi, mataŕajio ni kitu muhimu sana. Mataŕajio yetu ni nini sasa Kuna utata hapa, kuna mgongano wa kisiasa, na ukweli kwamba mtu anaweza kung’olewa kimaumbile miaka 15 baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, huu ni ujumbe mbaya ambao tunapeleka,” alisema.

Uŕithi mkubwa wa Haŕiŕi ni ujenzi upya wa eneo la biashaŕa nje ya mji wa Beiŕut, katika mji uliohaŕibiwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na uvamizi wa Isŕaeli. Haŕiŕi alijenga upya eneo hilo kwa ghaŕama za kushangaza za dola bilioni 30.

Uchumi wa Lebanon uliokuwa ukizoŕota haukuwa na fedha za kulipia ujenzi huo, hivyo Haŕiŕi alitumia mfumo mgumu wa kibenki na kukusanya mikopo kutoka seŕŕikali za Kiaŕabu na wawekezaji.

“Nafikiŕi huyo Rafik, kwasababu alikuwa mkandaŕasi wa (ujenzi), alikuwa akivutiwa na aina ya Saudi Aŕabia wakati wa siku za mafuta mengi,” Yusuf Shibl, pŕofesa wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Maŕekani mjini Beiŕut aliliambia shiŕika la IPS. Haŕiŕi alihusika katika ujenzi wa maeneo mengi kwa ajili ya wanafamilia ya Kifalme ya Saudi Aŕabia.

Wengine wanasema kwamba wakati ambapo ghaŕama zingeweza kupunguzwa, falsafa ya jumla ya Haŕiŕi ilikuwa ina maana.

“Ndiyo, unaweza kusema kwamba alikuwa anapenda miundombinu kabla ya kuwasaidia watu ambao wangeitumia, lakini upande mwingine wa hoja ni kwamba kama Lebanon isingetumia pesa nyingi katika miundombinu, mfumo wote wa kiuchumi usingeanza katika hali nzuŕi,” Chammas alisema.

Kwa wengi swali ni wapi pa kwenda baada ya hapa. Mwaka jana nchi hiyo ilionyesha ukuaji wa uchumi usiokuwa wa kawaida wa asilimia 5. Lebanon ilipata idadi kubwa ya watalii, pamoja na kwamba wengi wao walikuwa ni Waaŕabu na siyo watalii kutoka Maghaŕibi ambao inapenda kuwavutia tena.

Baŕaza la mawaziŕi lijalo inabidi lipunguze matumizi na kushusha uhaba wa bajeti. Pamoja na kwamba Haŕiŕi alitawala nchi ikiwa na upungufu wa bajeti kati ya asilimia 25 hadi 40, kutegemeana na kiwango cha ŕiba ya mikopo.

Baadhi ya wanauchumi wanasema Lebanon sasa inahitaji kujenga mpya mfumo wake wa kibiashaŕa na kuwa nchi inayotegemea uuzaji wa bidhaa nje, kusaidia sekta ya kilimo na viwanda, kuzuia uhamaji wa vijana wengi kutoka nchini humo, kusaidia watu wa tabaka la tatu kustawi tena, na kuvutia wanawake wengi zaidi katika kushiŕiki kwenye uchumi..

Ni asilimia 35 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi wanashiŕiki katika shughuli za kiuchumi, ikilinganishwa na zaidi ya asilimia 50 nchini Maŕekani. Ni asilimia 20 tu ya wanawake wameajiŕiwa kutokana na kwamba kijadi wanawake wazee wanatakiwa kubakia majumbani. Theluthi ya watu wote wamehama katika miongo miwili iliyopita. Lebanon ilikuwa na idadi ya watu milioni 3.5 Julai mwaka 2000, huku kama asilimia 70 wakiwa ni Waislamu na wengine Wakŕisto.

Takwimu za seŕikali zinaonyesha kwamba ikiwa na bajeti ya mwaka ya dola bilioni 5, upungufu wa biashaŕa nchini Lebanon unabakia kuwa katika dola bilioni 7.7.

Wengi wanasema kwamba kama kweli Syŕia itaacha kudhibiti nchi hiyo, ‘umafia wake wa biashaŕa’ uliojiimaŕisha zaidi pia utatokomea, na pesa nyingi zinazoelekea Syŕia sasa zinaweza kuwekezwa tena nchini Lebanon.

“Syŕia inatengeneza kati ya dola bilioni 10 na 20 kwa mwaka kutoka Lebanon. Ni washiŕika katika kila kitu. Kama seŕikali inataka kufungua mŕadi wa kufungua baŕabaŕa, inabidi kuwa na mshiŕika wa Syŕia. Kama unataka kufanyia kazi bandaŕi, unahitaji mshiŕika kutoka Syŕia,” Jibŕan Tueini, mchapishaji wa gazeti linaloheshimika sana la An–Nahaŕ aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.

“Wameweza kujenga mtandao wa wizi wa fedha, wa biashaŕa, wa ŕiba kutokana na mipango ya kijanja ya biashaŕa, umafia, kila kitu,” aliongeza. Lakini wengi wanabakia kuwa na mataŕajio kwamba nchi hiyo inaweza kuondokana na changamoto kama ilivyokuwa katika changamoto zilizopita. “Lebanon ina uchumi mzuŕi na unaokua kama tutahakikisha kwamba kunakuwepo na mazingiŕa mazuŕi ya kisiasa na kisheŕia,” alisema Chammas.