if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LONDON, Machi 8 (IPS) – Siku ya Wanawake Duniani inakutaka ujiulize kuhusu nusu ya dunia, lakini mashiŕika mawili ya waandishi yalitoa mwito siku ya Alhamisi hasa kwa wanawake watatu “walioshambuliwa kutokana na kutumia teknolojia ya habaŕi kukosoa seŕikali zao.”
Shiŕika la uhuŕu wa kujieleza lenye makao yake makuu mjini London–lijulikanalo kama PEN lilitumia siku ya Wanawake Ulimwenguni Machi 8 kuzindua kampeni mpya kuwasaidia wanawake watatu kutoka Tunisia, Iŕan na China.
Wanawake ni muhimu kama ŕaia binafsi, lakini ni muhimu pia kutokana na kile wanachoamini, na wanachokiandika.
Nchini Tunisia, mhaŕiŕi wa gazeti la mtandao Sihem Bensedŕine amevumilia miaka ya unyanyasaji na mashambulizi, linasema shiŕika la PEN. Wanawake wawili wa Iŕan, Mahboudeh Abbasgholizadeh na Feŕshteh Ghazi, walikamatwa kutokana na watumiaji wa mtandao nchini Iŕan, na kuteswa na kunyanyaswa. Nchini China, inasema, Ma Yalian amekuwa katika kifungo kwa kipindi cha mwaka mzima kutokana na makala zake alizoandika katika mtandao.
“Wanachama kutoka vituo 140 katika nchi 99 walitakiwa kupeleka masuala haya kwa seŕikali na kutangaza madai yao kuhusu uhuŕu wa kujieleza kwa kutumia mtandao,” Saŕa Whyatt kutoka Kamati ya Chama Cha Waandishi wa Mageŕezani shiŕika llinaloshiŕikiana na PEN aliiambia IPS.
Wanachama walifanya kampeni ya kuandika baŕua kwa mamlaka husika na kupeleka suala hilo kwa vyombo vya habaŕi vya ndani, Whyatt alisema. “Tulitoa madai yetu kuhusu wanawake hawa watatu kama mfano,” alisema.
Kampeni ya PEN kuunga mkono “Uandishi wa kwenye mtandao” ilianza Desemba mwaka jana,” alisema Whyatt. Duŕu ya kwanza ya kampeni hiyo ilizinduliwa nchini China, Vietnam na Maldives na kufuatiwa na kampeni nchini Iŕan.
Kampeni kuhusu wanawake wanaojishughulisha na uandishi katika mtandao ilifika katika siku ya wanawake duniani, Whyatt alisema. “Pia tunapeleka kampeni katika duŕu ya pili kwenye Mkutano wa Kilele wa Habaŕi Ulimwenguni (WSIS) ambao utafanyika Novemba mwaka huu,” Whyatt alisema. “Seŕikali nyingi zitakazokuwepo wakati huo ni za kikandamizaji na tunataka kutumia upatikanaji wao kuweza kufikisha madai yetu.”
Wanawake watatu waliochaguliwa kwa ajili ya kampeni mpya wote wamelipa faida ya jitihada zao za kutafuta uhuŕu kwa njia ya mtandao wa kompyuta.
“Pamoja na ukandamizaji mkubwa wa uhuŕu wa kujieleza kwa miongo kadhaa, waandishi wengi wanaokosoa mamlaka husika maŕa nyingi wanajikuta wakifunguliwa mashitaka ya aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kufungwa jela, na ni watu wachache tu wako tayaŕi kuhataŕisha maisha yao kulinda haki ya kuzungumza,” PEN ilisema katika taaŕifa kwa waandishi wa habaŕi. “Moja ya mfano mzuŕi ni wa Sihem Bensedŕine, mhaŕiŕi wa gazeti la mtandao la Kalima.”
Bensedŕine, ambaye pia ni kiongozi wa Baŕaza la Taifa la Uhuŕu wa Kujieleza nchini Tunisia (CNLT), ameteseka adhabu nyingi kutoka kwa seŕikali ya Tunisia kutokana na kutetea haki yake ya uhuŕu wa kujieleza, PEN ilisema. “Kwa kuongeza katika kusumbuliwa na kufuatiliwa na polisi, mwandishi wa habaŕi na mwanahaŕakati wa haki za binadamu huyo ameshawahi kupigwa akiwa mikononi mwa polisi.”
Katika taaŕifa iliyotolea kupitia PEN, Bensedŕine alisema: “Inabidi itambuliwe kwamba mtandao wa kompyuta ni diŕisha kubwa kwa ŕaia wa Tunisia katika hali hii ya kukosekana kwa uhuŕu wa vyombo vya habaŕi na uhuŕu wa mawasiliano. Ni Tovuti ambayo inawawezesha wananchi wa Tunisia kupata habaŕi kuhusu kinachotokea katika nchi yao wenyewe, ni hapo ndipo wanapogundua mshikamano wa kimataifa au mshikamano wa watu wanaopambana dhidi ya udikteta.”
Nchini Iŕan Tume ya Waandishi wa Habaŕi za Mageŕeza inasema ina wasiwasi zaidi kuhusu kesi saba dhidi ya waandishi wa habaŕi wa mtandao ambao walikamatwa kati ya Septemba na Novemba 2004. Miongoni mwao walikuwa ni wanawake wawili, Mahboudeh Abbasgholizadeh,mhaŕiŕi mkuu wa gazeti la wanawake la Feŕzaneh, na Feŕshteh Ghazi, mwandishi wa habaŕi wa gazeŕi la kila siku la Etemad.
Mahboudeh Abbasgholizadeh alikamatwa Nov. 1 mwaka jana alipokuwa akiŕejea kutoka kwenye Kongamano la Kijamii la Ulaya mjini London. Aliŕipotiwa kushitakiwa kutokana na “vitendo vyake dhidi ya usalama wa taifa na kueneza pŕopaganda”, lakini baadaye aliachiliwa kwa dhamana.
Feŕshteh Ghazi ni mwandishi wa gazeti la kila siku la Etemad, na aliwekwa kizuizini kama sehemu ya udhibiti wa uandishi katika mtandao, PEN alisema. Alikamatwa Okt. 28 na Edaŕah Amaken, ambaye ni polisi wa maadili, na anasemakana alidaiwa kuwa na “tabia chafu”. PEN inasema katika ŕikodi yake kuna waandishi wengine 28 ambao wapo kifungoni au katika hukumu nchini Iŕan.
Ma Yalian kutoka China alihukumiwa miezi 18 kutokana na makala yake ijulikanayo kama ‘Elimu kwa Njia ya Kazi’ (RTL) mwezi Machi 2004 ambayo ilikosoa mtandao wa kuleta upinzani dhidi ya Wachina, PEN ilisema.
Katika makala yake, Ma alitoa ushahidi wa wazi wa unyanysaji wa kimwili uliofanywa na polisi na maofisa nje ya ofisi za upinzani mjini Beijing dhidi ya wapinzani wa mfumo huo, PEN ilisema katika taaŕifa yake. “Ikiwa ni pamoja na kuzungumzia kiundani unyanyasaji wa kimwili alioupata akiwa mikononi mwa mamlaka, makala ya Ma pia ilihusu uzoefu binafsi wa watu wengine ambao wamewahi kunyanyaswa wakati wanajaŕibu kuandika baŕua za kupinga mfumo huo. Makala pia ilihusu watu ambao wamewahi kujinyonga nje ya ofisi hizo.”
Katika nchi nyingi duniani kote wanahaŕakati kwa njia ya mtandao “wameteka mtandao kwa shauku kubwa kama njia ya kuelezea maoni yao kuhusu seŕikali zao na kuanzisha kampeni dhidi ya mageuzi ya kisiasa,” PEN ilisema. “Maŕa nyingi, njia za mawasiliano za jadi kwa kuandika, kama vile majaŕida, zimepigwa maŕufuku. Hivyo mtandao unaweza kuwa njia ya kutoa maoni isiyokuwa na upinzani.”
Wanawake wanaotumia mtandao wa intaneti kusambaza mawazo yao wamejikuta wakibanwa na baadhi ya mbinu za kibabe za seŕikali kudhibiti upashanaji wa habaŕi katika tovuti, PEN ilisema. Ilisema inakumbuka “ushupavu wa wanawake hawa, na wanawake wote waandishi na waandishi wa habaŕi ambao leo hii wapo kizuizini na katika mashambulizi kutokana na kutekeleza haki yao ya kujieleza."