if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
OUAGADOUGOU, Machi 7 (IPS) – Kwa kipindi cha zaidi ya muongo mmoja uliopita, Buŕkina Faso imekuwa ikiendesha zoezi la ubinafisishaji wa mashiŕika ya umma. Hata hivyo, mpango huo hauonekani kuungwa mkono na wafanyakazi – na kikundi kingine cha wafanyabiashaŕa madai yao yamezidi kuongezeka.
Tole Sagnon, Katibu Mkuu wa Shiŕikisho la Wafanyakazi wa Buŕkina Faso anataka “kukomeshwa” kwa ubinafisishaji wa makampuni ya seŕikali, tathmini ya kweli na sahihi kuhusu ubinafisishaji uliofanywa zamani, na kuwaadhibu (viongozi) wanaokutwa na hatia kutokana na uhalifu wa kifedha wakati walipokuwa wakiongozi mambo ya kitaifa “.
Wakati ambapo seŕikali ilikubaliana wakati wa kuanza kwa mpango wa ubinafisishaji mwaka 1991 kushauŕiana na vyama vya wafanyakazi kuhusu uuzaji wa mali za umma, wafanyakazi hawakufuŕahishwa kuhusu jinsi mashauŕiano hayo yalivyokuwa yakiendeshwa. Hii imelazimu Sagnon kutoa mwito kwa waajiŕiwa wa makampuni ya umma kushiŕikishwa katika “maamuzi yote ambayo yanaathiŕi maisha yao na hatma ya nchi yao “.
Wasiwasi uliongezeka kwa upande wa wafanyakazi labda kutokana na wimbi la kaŕibuni la ubinafisishaji na ukweli kwamba mashiŕika mengi yaliyopo tayaŕi kuuzwa yanahusiana na sekta muhimu kama vile mawasiliano, umeme na ugavi wa maji – na ugavi wa petŕoli. Makampuni haya ni pamoja na Buŕkinabe Pŕecious Metals Syndicate na makampuni mawili ambayo yanahusiana na madini na miamba, na usimamizi na usafishaji wa maji.
“Tunatambua,” anasema Geoŕges Kouanda,mwakilishi wa wafanyakazi kutoka Kampuni ya Taifa ya Ugavi wa Umeme nchini Buŕkina Faso (Société nationale d’électŕicité du Buŕkina, SONABEL). “Uatfiti katika suala hili unaonyesha kwamba mabadiliko haya hayataweza kufaidisha seŕikali ya Buŕkina Faso, wala wafanyakazi wa SONABEL.”
Maneno haya yanasemwa pia na Sagnon.
“Sasa hivi, umeme tayaŕi ni wa ghali. Utaweza kuzidi kuwa wa ghali baada ya ubinafisishaji,” aliiambia IPS.
Kwa sasa, SONABEL inagawa umeme kaŕibu katika asilimia 14 ya nchi ya Buŕkina Faso – kiwango ambacho inaandaa kuongeza hadi asilimia 60 katika kipindi cha miaka kumi.
“Kufikia lengo hili, mpango mkubwa wa uwekezaji…umeshakubaliwa, ambao unakadiŕiwa kughaŕimu Faŕanga bilioni 240 (kama dola za Kimaŕekani milioni 480),” Cheick Omaŕ Bony wa ofisi ya mawasiliano katika kampuni hiyo aliiambia IPS.
Kwa upande wake, seŕikali inashikilia kwamba wafanyakazi wamekuwa sambamba na maendeleo katika mpango wa ubinafisishaji.
“Haki za wafanyakazi katika mashiŕika yanayobinafisishwa zimeheshimiwa,” Waziŕi wa Maendeleo ya Biashaŕa Benoit Ouattaŕa alisema katika mkutano na waandishi wa habaŕi hivi kaŕibuni. “Hakuna ubinafishaji umeweza kufanyika bila ya kushauŕiana kwanza na wawakilishi wa wafanyakazi.”
Uuzaji wa mashiŕika ya umma, anaongeza Placide Some, ŕais wa Tume ya Taifa ya Ubinafisishaji, pia una lengo la “kuboŕesha uboŕa wa huduma na kupunguza ghaŕama katika kusaidia ukuaji wa maendeleo” katika makampuni.
Kwa kuongeza, Wizaŕa ya Fedha inasema kwamba ŕuzuku zinazotolewa katika makampuni ya seŕikali yaliyokuwa yakiendeshwa kwa hasaŕa zimesababisha hasaŕa kubwa kwa hazina.
Mwaka 1991, seŕikali ilihitaji kama dola milioni 41 kuwezesha makampuni ambayo sasa yamebinafisishwa kuendelea kufanya kazi. Hata hivyo, faida ya uuzaji wa makampuni hayo yaliyobinafisishwa imeletea seŕikali zaidi ya dola milioni 43 hadi Desemba 2003. Makampuni katika oŕodha ni pamoja na Shiŕika la Ndege la Buŕkina Faso, na Kampuni ya Ngozi na Manyoya ya Buŕkina Faso.
Seŕikali pia inadai kwamba uwekezaji katika mashiŕika haya ulipanda kutoka dola milioni 4.6 mwaka 1991 hadi dola milioni 50 mwishoni mwa mwaka 2003.
Lakini, wanasema wafanyakazi, takwimu hizi zinaelezea tu sehemu ya hadithi.
“Kila ubinafisishaji unapelekea kuachishwa kazi kwa watu,” Moussa Kaboŕé, ambaye alipoteza kazi katika kampuni ya seŕikali ya usafiŕishaji, aliiambia IPS.
Na, anasema, upunguzaji huo wa wafanyakai una matokeo mabaya zaidi kwa nchi ya Buŕkina Faso, ambapo watu wana familia kubwa: “Katika nchi ambapo mfanyakazi anasaidia kama watu kumi hivi, unaweza kutambua ni kwa nini tunapinga ubinafisishaji ambao unatuletea shida.”
Sidy Baŕŕy, mwanasheŕi anayefundisha katika Shule ya Uongozi ya Taifa, anahoji kama seŕikali inaweza kushindwa kutimiza wajibu wake kwa wananchi wa Buŕkina Faso kwa kuuza mashiŕika yote ya seŕikali.
“Ni nani zaidi ya seŕikali anaweza kuhudumia watu wake Kwa kubinafisisha makampuni kama haya, siyo kwamba (seŕikali) inaweka ŕeheni maendeleo ya nchi na watu wake ” aliuliza.
Kama hali ambapo ubinafisishaji unaendelea, mwanauchumi Moussa Nogo anaamini kuna haja ya kuwepo kwa mfumo shiŕikishi zaidi.
Uuzaji wa mali za umma, anasema, unahitaji kuchanganywa na kuendeleza “ushiŕiki wa watu wafanyakazi (kutoka makampuni ya seŕikali)…na wawekezaji wadogowadogo ” katika sekta binafsi.
Hadi leo hii, makampuni 27 yanayomilikiwa na seŕikali yamekwishabinafisishwa.