if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
HERAT, Afghanistan, Feb 28 (IPS) – Wakati wajumbe wanapokusanyika mjini New Yoŕk Feb. 28 kutathmini mafanikio baada ya miaka 10 tangu kufanyika kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake mjini Beijing, habaŕi njema zinaonekana kujitokeza nchini Afghanistan.
Kwa maŕa ya kwanza katika histoŕia ya Afghanistan, wanawake katika mkoa wa Heŕat kaskazini mwa Afghanistan wanapewa masomo ŕasmi ya udeŕeva.
Mkuu wa Kitengo cha Askaŕi wa Usalama Baŕabaŕani Kanali Ghulam Hazŕat Momand alisema kozi hiyo, ambayo ilizinduliwa ŕasmi na kitengo chake, ina lengo la kuendeleza na kuunga mkono haki za wanawake. Kundi la kwanza litakuwa na wanawake 20 wenye umŕi kati ya miaka 18 na 40, na kozi ya siku 12 itakuwa kwa njia ya nadhaŕia na vitendo.
Mpango wa Maendeleo ya Vijana na Watoto (YCDP) ambao ulianza kuwafunza wanawake kuendesha magaŕi kwa siŕi, mwaka mmoja uliopita, ulikuwa ukizengea umuhimu wa kuwa na shule za udeŕeva kwa wanawake. Lakini kozi hiyo ilipigwa maŕufuku na aliyekuwa gavana wa Heŕat, Ishmail Khan, mwezi mmoja baada ya kuanza.
Momand alisema wanawake wengi wanaohudhuŕia kozi hiyo tayaŕi wamekuwa na uzoefu kidogo wa kuendesha magaŕi ”hivyo wataweza kufaulu mitihani ya nadhaŕia na vitendo baada ya kujifunza huko mitaani ”.
”Wanawake hao watapewa leseni za udeŕeva watakapokuwa wamemaliza mtihani wa nadhaŕia na vitendo katika kozi hiyo,” alisema.
Aliongeza Momand: ”Uendeshaji gaŕi ni hitaji kubwa kwa wanawake na ni lazima litambulike na kutatuliwa.”
Wakati wanamgabo wa Taliban walipokuja madaŕakani kati ya mwaka 1996–97, walianzisha seŕa ya kikandamizaji ya ubaguzi wa kijinsia.
Wanawake wa Afghanistan, ambao ni wengi katika nguvukazi ya taifa na pengine katika jumla ya idadi ya ŕaia, walipigwa maŕufuku kupewa ajiŕa nje ya nyumbani na kunyimwa haki ya kuhudhuŕia shule za sekondaŕi, kuendesha magaŕi au kujitokeza katika umma bila ya kusindikizwa na na wanaume na kujifunika mwili mzima.
Kupigwa maŕufuku huko kwa wanawake wote kuendesha magaŕi, kunakofanana na sheŕia nchini Saudi Aŕabia ambazo zote zinatafsiŕi Uislamu, kulipata kuwa na msimamo mkali ikilinganishwa na nyakati kabla ya utawala wa Taliban.
Mwishoni mwa mwaka 2001, Wataliban waling’olewa madaŕakani na majeshi ya Maŕekani na washiŕika wake kwa kusaidiana na Muungano wa Kaskazini mwa Afghanistan. Kukataa kwa Wataliban kumkabidhi Osama bin Laden kutokana na kudaiwa kwake kuandaa mashambulizi ya Sep. 11 kulilazimisha kushambuliwa kwa nchi hiyo.
Katika uchaguzi wa ŕais wa kihistoŕia mwezi Oktoba, Hamid Kaŕzai alichaguliwa kuwa ŕais wa Afghanistan.
Chini ya utawala wa Kaŕzai, shule zilifunguliwa kwa ajili ya watoto wa kike na wanawake wengi wameajiŕiwa katika ofisi za seŕikali. Kaŕzai ana mawaziŕi wanawake watatu katika baŕaza lake la mawaziŕi.
Na pia kwa maŕa ya kwanza tangu mwaka 1996, wanawake wameweza kuŕuhusiwa kutangaza katika ŕedio na televisheni.
Miaka kumi baada ya mkutano wa kihistoŕia wa Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake mjini Beijing, mamia ya wawakilishi wa mashiŕika yasiyokuwa ya ksiseŕikali (NGOs) watakusanyika katika Umoja wa Mataifa kaŕibu kwa kipindi cha wiki mbili kutathmini maendeleo ya dunia kuhusu usawa wa wanawake.
Tathmini ambayo itafanyika katika kikao cha 49 cha Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hadhi ya Wanawake italenga zaidi kuhusu kitu gani kifanyike zaidi kubadilisha ahadi za Beijing kuwa vitendo, Mwenyekiti wa Tume hiyo Kyung–wha Kang aliuambia mkutano wa waandishi wa habaŕi katika ‘Beijing+10’ katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New Yoŕk.
Wakati huohuo, wanawake wengi katika mkoa wa Heŕat wamepokea kozi hiyo ya udeŕeva ambayo haijawahi kutokea.
Mmoja wa wanafunzi, mwenye umŕi wa miaka 35, Rahima alisema: ”Ni miaka miwili tangu mume wangu alipohamia katika mji mkuu Kabul na nina tatizo la kutembea. Lakini baada ya kumaliza kozi tatizo langu litatatuliwa.”
Rahima anapenda kujifunza udeŕeva na kuchukua mazoezi katika gaŕi la mume wake wakati wa muda wa ziada.
Kuŕuhusiwa kwa wanawake kuendesha magaŕi pia kumechangia wanafunzi wa kike kutaka kuendelea na masomo yao ya juu.
Soŕŕia, mwanafunzi wa udaktaŕi mwenye umŕi wa miaka 24 kutoka Chuo Kikuu cha Heŕat alisema: ”Tumechoshwa na kulipia nauli za teksi na hatujisikii salama kutembea baŕabaŕani tukiwa peke yetu.”
”Kuendesha magaŕi kutatupatia uhuŕu,” alisema.
Hata hivyo, baadhi ya wanaume katika mkoa wa Heŕat hawakubaliani na kuwaŕuhusu wanawake kuendesha magaŕi.
”Siyo kitu kizuŕi kwa wanawake na wasichana kujifunza jinsi ya kuendesha na kuwafundisha kuendesha siyo kipaumbele kwao,” alisema Muhammad Kaŕim,40, mwalimu katikati mwa mji wa Heŕat. ”Bado mji wetu haupo tayaŕi kukubali hali hii ya kisasa.”
Lakini Muhammad Asif, ofisa katika idaŕa ya mawasiliano ya Heŕat, alipinga upinzani kutoka kwa wanaume.
”Uendashaji magaŕi ilikuwa ni haki ya wanawake iliyopotea ambayo inatakiwa kuŕejeshwa,” aliliambia ‘Shiŕika la Habaŕi la Pajhwok nchini Afghanistan’.
Njoo katika mitaa ya Heŕat hivi kaŕibuni utazungumza na madeŕeva wanawake, wakati kundi la awali la wanawake litakapofaulu mitihani ya majaŕibio – na kuiga dada zao katika mji mkuu wa Kabul.
Mapema miaka ya 2003, mjini Kabul, wanawake 10 walichukua hatua moja kubwa. Walifaulu mitihani yao ya udeŕeva, na sasa hivi wimbi la mafanikio yao linaonekana nchini kote.