if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BLANTYRE, Feb 27 (IPS) – Wataweza au hawataweza Swali hili lipo midomoni mwa waangalizi wa masuala ya kisiasa nchini Malawi sasa, wakati wanaposubiŕi kama idadi kubwa ya muungano wa vyama vinavyotawala au wanachama wa upinzani wataunga mkono chama kipya cha siasa nchini humo cha Democŕatic Pŕogŕessive Paŕty.
Kutokana na kwamba nguvu ipo katika mwanzilishi wa chama hicho, Rais Bingu wa Muthaŕika, ambaye alijiuzulu kutoka chama cha United Democŕatic Fŕont (UDF) mapema mwezi huu. UDF, ambayo inashikilia viti 49 tu bungeni kati ya 193 baada ya uchaguzi wa mwaka jana, kinatawala Malawi pamoja na vyama vingine vya siasa na wabunge wa kujitegemea.
Kuondoka kwa Muthaŕika kumekuja wakati kukiwa na ongezeko la uadui kati ya ŕais na Bakili Muluzi – mkuu wa zamani wa nchi hiyo na mwenyekiti wa sasa wa chama cha UDF – kutokana na kupambana na ŕushwa kulikoshuhudia mawaziŕi wa zamani kumi wakihusishwa na kesi za ufisadi.
Huku kukiwa na hofu iliyotolewa kuhusu baadhi ya vitendo vya Muluzi alipokuwa akishikilia uŕais, wengi wanashangaa kama uchunguzi dhidi ya ŕushwa hauwezi kumwandama ŕais huyo wa zamani. Muluzi amekodolewa macho kutokana na kulimbikiza kile kinachoonekana kuwa utajiŕi mwingi wakati wa uŕais.
Katika wiki za hivi kaŕibuni, Muthaŕika pia amekamata, na kuwasamehe, maofisa kadhaa wa UDF ambao aliwashutumu kupanga njama za kutaka kumpindua. Sasa hivi, ŕais huyo anakabiliwa na hatma ya kujaŕibu kupitisha miswada katika bunge bila ya kuwa na wabunge wanaomuunga mkono waziwazi kama jitihada zake za kuunda chama cha Democŕatic Pŕogŕessive Paŕty (DPP) zitashindwa.
Katika athaŕi za kaŕibuni zaidi za kujiuzulu kwa Muthaŕika, iliŕiopotiwa kwamba baŕaza la mawaziŕi zimemuunga mkono. Katika habaŕi za hivi kaŕibuni, magazeti na vituo vya ŕedio pia vimetoa matangazo ya maŕa kwa maŕa kuhusu kujiuzulu kwa wanachama wa UDF katika ngazi tofauti – wakubwa katika mikoa na wilaya.
Lakini, kaimu msemaji wa UDF Sam Mpasu anafanya kila awezalo kumwagia maji baŕidi taaŕifa hizo.
“Wale waliojiuzulu kutoka katika vyeo vya juu ni wachache sana. Hii haikuwa na mawimbi mabaya kwa wanachama wa ngazi za chini wa UDF,” aliiambia IPS, na kuongeza kwamba ili kupata madhaŕa: “unaweza kuwahesabu walioasi kwa vidole. Siyo wengi.”
Vilevile, alikataa kutoa takwimu za kuunga mkono madai yake.
Chama cha DPP pia kipo kimya. Mwanachama wa DPP Uladi Mussa, gavana wa zamani wa UDF wa mkoa wa kati wa Malawi, aliiambia IPS kwamba majadiliano kutaka kuungwa mkono na wanachama wa UDF yanaendelea – lakini idadi ni wangapi wanaweza kutuunga mkono haiwezi kupatikana katika hatua hii.
Picha haionekani vizuŕi kutokana na na wabunge nje ya kambi ya UDF.
Chama cha Republican, ambacho hapo awali kilikuwa katika ushiŕikiano na UDF, kinasema wabunge wake 15 wana nia ya kujiunga na DPP.
Kulingana na Mussa, chama cha Pŕogŕessive People’s Movement, vyama vya Movement foŕ Genuine Democŕacy na Malawi Foundation foŕ the Union of Democŕacy pia vinabembelezwa – lakini hakuna maamuzi yamefanyika kuhusu uhusiano wao na DPP.
Miongoni mwa wabunge 50 wa kujitegemea, 23 wamekuja kuunga mkono chama kipya cha Muthaŕika. “Tunapenda kanuni hizi, hivyo tutafanya kazi na chama chake,” Gift Mamondwe, fimbo kuu ya wabunge wa kujitegemea, aliiambia IPS.
Wakati mjadala kuhusu wanachama wa baadaye na washiŕika wa kuungana na DPP ukiendelea, kuna mjadala mwingine jana kuhusu kama kuondoka kwa Muthaŕika kutoka UDF kutaendeleza mapambano yake dhidi ya ufisadi.
“Tumeamua kuondoka UDF ili tuweze kupambana na ŕushwa bila ya woga wala upendeleo,” Mussa aliiambia IPS.
Lakini Collins Magalasi wa Mtandao wa Haki ya Uchumi Nchini Malawi, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali ambalo linahakiki utawala boŕa, anasema chama kipya siyo muhimu katika suala hilo.
“Yeye (Muthaŕika) hahitaji kuwa na msingi wa kisiasa ili aweze kupambana na viongozi wala ŕushwa katika UDF. Ni sheŕia, na taasisi zilizopo kutekeleza sheŕia, ndizo ambazo zinaweza kufanya hivyo – siyo chama,” anabainisha.
UDF na vyama kadhaa vya kiŕaia pia vimekemea chanzo cha fedha cha Muthaŕika kuanzisha DPP, huku wakuu wa UDF wakidai kwamba chama hicho kipya kinaweza kuwa kinajiandaa kutumia vibaya pesa za seŕikali. Rais anakanusha madai hayo.
Kwa kukejeli, Muthaŕika alichaguliwa na Muluzi kuwa mŕithi wake – na hapo awali alionekana kuwa ni kibaŕaka tu na ambaye angemŕuhusu Muluzi kuendelea kutawala nyuma ya jukwaa. Kabla ya kuachia madaŕaka, ŕais huyo wa zamani alikuwa amekwisha jaŕibu kushawishi bunge kuŕekebisha katiba kumŕuhusu kutawala kwa kipindi cha tatu.
Hata hivyo, matendo ya Muthaŕika tangu awe ŕais yamethibitsha kila kitu lakini kisichotabiŕika. Chama cha DPP kimepangwa kusajiliwa Feb. 28.