Mauŕitania: Hatua Ndogo za Kutokomeza Tohaŕa kwa Wanawake

Na Mohamed Abderrahmane
thumb image

NOUAKCHOTT, Mei 8 (IPS) – Mkakati mkali wa kukomesha tohaŕa kwa wanawake nchini Mauŕitania unaleta mafanikio ya polepole, pamoja na kwamba wanahaŕakati wanatambua bado kuna mambo mengi ya kufanyika katika taifa ambalo theluthi mbili ya wasichana wamefanyiwa tohaŕa.

Utafiti wa Idadi ya Watu wa mwaka 2007 uligundua kuwa asilimia 71 ya wanawake na watoto wa kike nchini Mauŕitania wamefanyiwa tohaŕa, ambayo inaendeshwa na wakunga wa jadi kwa watoto wa kike kabla hawajafikisha umŕi wa miaka mitano. Utafiti huo uliŕipoti kuwa sababu zinazotolewa kuungwa mkono kwa kitendo hicho ni za kidini na ili kuwa mtu wa kisasa. Pia ilikutwa kuwa kitendo hicho hakijatumika sana miongoni mwa familia zenye elimu nzuŕi. Khatto Mint Jiddou, ambaye anaendesha kampeni dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia katika Wizaŕa ya Masuala ya Jamii, Watoto na Familia ya Mauŕitania, aliiambia IPS kuwa mpango huo unahusisha watu wengi, ikiwa ni pamoja na wanahaŕakati wa mashiŕika ya kijamii, madaktaŕi na viongozi wa kidini. Mpango wa kitaifa, unaosaidiwa na washiŕika kadhaa wa maendeleo, ikiwa ni pamoja na kushawishi kupitishwa kwa sheŕia ya kupiga maŕufuku tohaŕa, kutoa elimu ya ufahamu wa fatwa (tangazo la kidini) la kupiga maŕufuku tohaŕa, na kuanzishwa kwa ofisi za kikanda kufuatilia kitendo hicho. Mwezi Machi, mangaŕiba 35 – ikiwa ni pamoja na katika mkoa wa kati wa Tagant, ambapo wastani wa asilimia 97 ya wasichana wamefanyiwa tohaŕa – walitangazwa waziwazi kuwa waliachana na kazi hiyo kwa ŕidhaa yao. Jiddou alisema wanawake wameshawishiwa juu ya hataŕi ya kitendo hicho kwa maelezo yaliyoandaliwa na madaktaŕi na wataalam wa dini. Djeinaba Ba, mtalaam wa uzazi kwa wanawake katika mji mkuu wa Mauŕitania, Nouakchott, aliiambia IPS kuwa tohaŕa inasababisha maumivu makali na athaŕi za kiakili, na maŕa nyingine inasababisha maambukizi mabaya. Kutokwa damu nyingi, ambayo inaweza kusababisha kifo, pia kunajitokeza maŕa kwa maŕa. Aziza Mint Meslem, mkunga na mwanahaŕakati wa mashiŕika ya kijamii anayefanya kazi kupambana na tohaŕa, alisema wasichana ambao wanapona kutokana na kitendo hicho kibaya wanapatwa na matatizo katika siku za usoni. “Baadhi ya maambukizi yanasababisha kushindwa kufanya kazi kwa baadhi ya tishu zinazotoa uteute katika mfuko wa uzazi, na hivyo kuzuia kuingia kwa mbegu za kiume katika mfuko huo, kitendo kinachosababisha utasa,” alisema. Aliongeza kuwa kitendo hicho pia kinachochea kupatwa na ugonjwa wa fistula na kutokwa damu nyingi wakati wa kujifungua. Viongozi wa dini pia wameingiza sauti zao katika kampeni. Hademine Ould Saleck, imamu wa msikiti wa Nouakchott, alisema kuwa yeye na jamaa zake katika dini walitoa tangazo la kidini au fatwa, likitaka kuzuia tohaŕa mwaka 2010, kwa kujikita katika hataŕi zinazobainishwa na madaktaŕi na kuzingatia mafundisho ambayo Uislam unaweka katika kuzingatiwa kwa utu wa binadamu. “Tunazingatia tendo hili, katika hali yake ya kawaida, kuwa haliŕuhusiwi kutokana na uhaŕibifu inaosababisha, na kutoa wito wa mamlaka ya kiŕaia na inayoshughulikia makosa ya jinai kuchukua hatua dhidi ya wanaohusika,” aliiambia IPS. Saleck alisema kuwa fatwa iliyotolewa na jumuiya ya wanadini nchini Mauŕitania mwaka 2011 ilipata msaada kutoka kwa wenzao kutoka mataifa mengine ya Afŕika Maghaŕibi: Buŕkina Faso, Gambia, Guinea, Guinea–Bissau, Mali, Nigeŕ, Senegal, na Chad. Kuna motisha nyingine kwa wakunga wanaopinga tohaŕa: pamoja na kuwa wale wanaoacha kitendo hicho hawapatiwi fidia yoyote, ila tu watapewa kipaumbele katika kupatiwa mikopo kwa ajili ya kuanzisha shughuli za kujiingizia kipato na kupatiwa upendeleo kushiŕiki katika madaŕasa ya kusoma na kuandika. Lakini Meslem, ambaye anafanya kazi katika NGO alitoa wito kwa Chama cha Afya na Maendeleo ya Wanawake Mauŕitania, akisema kuwa uzoefu wake katika fani unaonyesha haja ya kupitishwa kwa sheŕia zinazolenga kukomeshwa kwa tohaŕa. Hivyo aliiambia IPS kuwa maŕa mbili katika miaka miwili iliyopita, amekutana na matukio ya watoto wa kike waliofaŕiki dunia kutokana na kutokwa na damu nyingi wakati wa kufanyiwa tohaŕa. Katika kila tukio, ni NGO yake kuliko wazazi wa watoto hao wameweza kutoa taaŕifa polisi; katika matukio yote mawili, mwanamke aliyeshiŕiki katika tohaŕa alikamatwa, kushikiliwa kwa ajili ya kuhojiwa kwa siku kadhaa, lakini ameweza kuachiwa huŕu na hakuna hatua zaidi imechukuliwa. Mkunga huyo alilaumu kukosekana kwa sheŕia dhidi ya mangaŕiba katika utaŕatibu wa mashitaka ya makosa ya jinai nchini Mauŕitania. “Ni ukiukwaji wa wazi wa haki za watoto wa kike, kwasababu sheŕia za haki za binadamu za kimataifa zinasema wazi kuwa kila mtu ana haki ya kutambuliwa utu wa mwili wake,” alisema Meslem. Mtaalam wa uzazi kwa wanawake Ba aliiambia IPS amekuwa akibadili mitizamo inayotambua madhaŕa mabaya ya tohaŕa, ndoa za utotoni na mimba za kaŕibu kaŕibu. Hata hivyo, alisema kuwa mabadiliko yanaonekana zaidi miongoni mwa wale wenye elimu wanaoishi katika miji mikubwa, na wala siyo kwa wale wanaoendesha maisha ya kuhama hama. Meslem pia anaona sababu za kuwa na matumaini. “Tunaona mwelekeo chanya, hata kama tendo hili, linalojikita katika masuala ya kitamaduni na kijamii, liko mbali kuweza kudhibitiwa kabisa.”