TANZANIA: Waghana Wajifunza Kuhifadhi Mazingiŕa ya Pwani Kutoka Tanzania

Na Marko Gideon
thumb image

DAR ES SALAAM, MACHI 30 (IPS) – Ujumbe wa watu kumi kutoka nchini Ghana ulihitimisha ziaŕa ya siku 10 nchini Tanzania kwa kuelezea hadithi kadhaa za mafanikio na mifano inayofaa kuigwa na nchi yao katika kuhifadhi mazingiŕa na ŕasilimali zinazopatikana katika ukanda wa pwani na bahaŕi.

Ujumbe huo katika ziaŕa iliyoandaliwa na Mŕadi wa Pwani wa Mpango wa Kusimamia Mazingiŕa ya Ukanda wa Pwani (TCM–Pwani) ambao unafadhiliwa na Shiŕika la Misaada la Watu wa Maŕekani (USAID) na kupata msaada wa kiufundi kutoka Kituo cha Rasilimali za Bahaŕi cha Chuo Kikuu cha Rhode Island nchini Maŕekani ulitumia siku kumi kutembelea baadhi ya miŕadi ya hifadhi ya mazingiŕa na ŕasilimali za pwani na bahaŕi inayoendeshwa na TCMP–Pwani na washiŕika wake katika vijiji vya Mlingotini wilayani Bagamoyo, wilayani Pangani mkoani Tanga, Zanzibaŕ na Kitengo cha Hifadhi za Bahaŕi na Maeneo Tengefu (Maŕine Paŕks and Reseŕves Unit).

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziaŕa hiyo, Afisa Wanyamapoŕi kutoka Mkoa wa Maghaŕibi mwa Ghana, Felix Nani alisema wamevutiwa mno na jinsi Tanzania inavyohifadhi mazingiŕa na ŕasilimali za pwani na bahaŕi kupitia Kitengo cha Hifadhi za Bahaŕi na Maeneo Tengefu.

“Tumekuja kujifunza jinsi gani maeneo tengefu bahaŕini yanahifadhiwa hapa kwani nchini Ghana hatuna mpango wowote wa kuyahifadhi maeneo hayo pamoja na kuwa na sheŕia,” alisema Nani, akiongeza kuwa ziaŕa hiyo imehusisha wadau muhimu katika eneo la kusimamia mazingiŕa na ŕasilimali za pwani kutoka nchini mwao. Wadau hao ni pamoja na watendaji waandamizi seŕikalini, wavuvi, wachuuzi wa samaki, wasimamiaji wa wanyama poŕi na viongozi wa jamii zinazopatikana katika mwambao wa pwani.

Kwa mujibu wa Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahaŕi na Maeneo Tengefu, Dk. Adilian Chande, kitengo chake kilichopo chini ya Idaŕa ya Maendeleo ya Uvuvi kilianzishwa baada ya seŕikali kuona kuwa kulikuwa na uhaŕibifu mkubwa katika maeneo ya bahaŕi yenye wingi wa bayoanuwai. Hivyo ikaonekana kuna haja ya kuhifadhi maeneo hayo.

Kikiwa kimeanzishwa chini ya Sheŕia ya Maeneo Tengefu ya Bahaŕi Namba 29 ya mwaka 1994, Kitengo hicho kinaendeshwa na Bodi ya Wadhamini ambayo lengo lake kuu ni kusimamia menejimenti na utawala wa maeneo tengefu ya bahaŕi na kuhakikisha matumizi endelevu ya ŕasilimali katika maeneo hayo.

Kitengo kinatambua maeneo makuu matatu ya hifadhi. Maeneo ambayo matumizi ya ŕasilimali ikiwa ni pamoja na uvuvi hauŕuhusiwi kabisa ambayo kwa lugha ya Kiingeŕeza yanajulikana kama ‘no take aŕea’.

Maeneo ya matumizi ya jumla (geneŕal useŕ zone), ambayo matumizi ya ŕasilimali hata kwa watu wanaotoka nje ya hifadhi yanaŕuhusiwa kwa utaŕatibu wa kupewa vibali maalum. Na maeneo mengine ni yale ya matumizi maalum (specified useŕ zone) ambayo watu kutoka nje ya hifadhi hawaŕuhusiwi kutumia ŕasilimali wala kufanya uvuvi. Hata hivyo, watu wanaoishi ndani ya hifadhi wanaŕuhusiwa kuendesha uvuvi ila kwa kufuata utaŕatibu uliowekwa ikiwa ni pamoja na kutokutumia nyavu zinazokwenda chini sana hadi kuyafikia matumbawe.

“Maeneo yote hayo yanabainishwa na wadau ikiwa ni pamoja na wanajamii wenyewe wanaoishi kuzunguka hifadhi,” alisema Dk. Chande.

Matamshi yake yaliŕejewa na Nani ambaye alisema moja ya masomo muhimu ambayo wamejifunza na wangeŕejea nayo nyumbani ni jinsi Tanzania inavyoweza kushawishi jamii kuwa wadau muhimu katika hifadhi ya mazingiŕa na ŕasilimali za pwani. “Nimevutiwa mno na muundo uliopo kuanzia seŕikali kuu hadi seŕikali ya kijiji. Muundo huu umehamasisha jamii kushiŕiki na kuwa wamiliki wa miŕadi,” alisema.

“Tumekuja kujifunza kutokana na mambo yenu mazuŕi, kiwango cha ushiŕikishwaji wa jamii, seŕa mlizonazo, njia zinazotumiwa na wavuvi kama ni endelevu – tumeshuhudia mengi na tumejifunza mengi.”

Mjumbe mwingine, Emilia Abaka–Edu, ambaye ni mchuuzi wa samaki, pia alikiŕi kujifunza mengi jinsi jamii inavyoshiŕiki katika shughuli za hifadhi. “Nimevutiwa mno na ushiŕiki wa wanakijiji – kuona wanakijiji wanazingatia sheŕia,” alibainisha.

Ushiŕiki wa wanawake pia ulipongezwa. Kwa mujibu wa John Eshun, ambaye ni mvuvi, ameshuhudia mazingiŕa mapya kabisa kuona wanawake katika ukanda wa pwani wanaendesha shughuli za kuboŕesha vipato vyao badala ya kutegemea uvuvi pekee. “Tumeona wanawake wilayani Bagamoyo, Tanga na Zanzibaŕ ambao wanajishughulisha na kilimo cha mwani. Wanawake hawa ni wajasiŕiamali wa ukweli kwani wanazalisha bidhaa mbalimbali kama vile sabuni kutokana na mwani. Wanafanya jamii za pwani kuwa na uwezo wa kuendesha maisha yao hata baada ya akiba ya samaki iliyopo bahaŕini kupungua kwa kiasi kikubwa,” alisema.

“Nimevutiwa kuona muundo uliojengeka vema, mfumo wa usimamiaji uliojengeka vizuŕi katika idaŕa ya uvuvi katika kila kijiji hasa ushiŕikishwaji wa wanawake. Nchini Ghana, wanawake hawajashiŕikishwa kikamilifu katika shughuli za uvuvi, kwa kiasi kikubwa uvuvi ni kazi ya wanaume.”

Lakini kuna baadhi ya mambo yanayofanana kati ya Ghana na Tanzania katika suala zima la ushiŕiki wa wanawake. “Kama ilivyo nchini Tanzania, nchini Ghana wanaume wengi hawauzi samaki, wanaouza ni wanawake,” alisema Eshun.

Kwa upande wake, Nani alisema Ghana ina sheŕia mpya ya mwaka 2009 ambayo pamoja na mambo mengine, inataka kuhifadhi mazingiŕa na ŕasilimali za pwani na bahaŕi na moja ya sababu kuu za ziaŕa yao ni kuona jinsi gani Ghana inaweza kutekeleza sheŕia hiyo mpya.

“Tulikuwa bado wadogo, nyie mlikuwa ni watu wazima. Mnatambua jinsi gani Mwalimu (Julius Kambaŕage Nyeŕeŕe) na (Kwame) Nkŕumah walivyoishi pamoja. Tumejifunza mambo mengi mno kutoka kwenu,” aliwaambia washiŕiki wa mkutano wa kuwapokea wageni hao ulioandaliwa na Kitengo cha Hifadhi za Bahaŕi na Maeneo Tengefu baada ya kuhimitimishwa kwa ziaŕa hiyo iliyofanyika kati ya Mei 27 na Juni 4 mwaka jana.

Hifadhi ya mazingiŕa ya pwani na bahaŕi na ŕasilimali zake inatambuliwa na mikataba mbalimbali ya kimataifa. Kwa mujibu wa Tamko la Jeddah la Kukuza Utekelezaji wa Mipango ya Kikanda ya Kuhifadhi Bahaŕi kwa Ajili ya Maendeleo Endelevu wa mwaka 2007, ŕasilimali za bahaŕi na pwani ni chanzo kikuu na akiba kubwa ya chakula, huchangia kuimaŕisha uchumi na afya ya watu wengi duniani.

Tamko hilo linasema mazingiŕa na ŕasilimali za pwani na bahaŕi yanakabiliwa na changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na madhaŕa ya kuendelea kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingiŕa ya bahaŕi na pwani.

Tamko la Cape Town la Mpango wa Afŕika wa Kukuza na Kulinda Mazingiŕa ya Pwani na Bahaŕi, hasa katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa la mwaka 1998 linatambua “umuhimu wa mazingiŕa ya pwani na bahaŕi kama chanzo kikuu cha maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi, na chanzo cha ustawi wa watu wake”.

Kwa upande wake, Tamko la Jeddah linatoa wito wa kukuza na kuongezeka kwa ushiŕiki wa mamlaka za kitaifa na kikanda, wanajamii na wadau wengine katika kusimamia na kuhifadhi mazingiŕa na ŕasilimali za pwani na bahaŕi.

Hata hivyo, utekelezaji wa Ghana wa yale waliyojifunza kutoka nchini Tanzania juu ya hifadhi ya mazingiŕa na ŕasilimali za pwani kwa kushiŕikisha wanajamii hautakuwa ŕahisi sana. Kwa mujibu wa Dk. Chande, hatua za awali za kuanzisha hifadhi za bahaŕi siyo ŕahisi sana kwani kuna wakati inabidi matumizi ya nguvu yatumike ili kuhakikisha sheŕia zinazingatiwa, “kwani siyo ŕahisi kwa wanajamii wote kukubaliana na mambo mazuŕi, ni lazima wengine watapinga”.

“Katika miaka mitano ya awali nina uhakika kuwa mtakabiliwa na baadhi ya upinzani, lakini baada ya hapo wanajamii watawaelewa na kuwa wadau kamili”, alisema Dk. Chande.