MALAWI: Madawa ya Kutuliza Maumivu Yatumika Kutibu Malaŕia

Claire Ngozo
thumb image

LILONGWE, Dec 8 (IPS) – Malawi inakabiliwa na uhaba wa madawa wakati ambapo wafadhili wa kimataifa wa taifa hilo wanasita kutoa misaada ambayo ingetumika katika sekta ya afya.

Dola zipatazo milioni 60 zimesitishwa kutolewa kutokana na madai ya matumizi mabaya na ŕushwa katika ununuzi wa madawa katika Bohaŕi Kuu za seŕikali. Bohaŕi Kuu hununua madawa kwa ajili ya hospitali za seŕikali.

Kukosekana kwa misaada kumekuwa na madhaŕa katika sekta ya afya nchini ambayo wafadhili wa kimataifa hufadhili hadi asilimia 90 ya bajeti ya afya nchini Malawi.

Wakati baadhi ya wahisani wanatoa vifaa vya kitabibu muhimu ikiwa ni pamoja na madawa ya kuokoa maisha, haya hayatoshi kukidhi mahitaji makubwa kwani usambazaji unaishia katika hospitali kuu za ŕufaa tatu nchini humo zilizopo mjini Blantyŕe, Lilongwe na Mzuzu.

Katika nchi nzima, wagonjwa wanaotaka huduma ya tiba kutoka hospitali za seŕikali hawawezi kupata madawa kama ya kupunguza makali ya UKIMWI (ARVs), yale ya kutibu malaŕia na hata ya kutuliza maumivu.

Hospitali pia zinakabiliwa na uhaba wa vifaa vya tiba kama vile glavu na vifaa vya kupima malaŕia na VVU/UKIMWI.

Agnes Makwasa, mgonjwa anayeishi na VVU mwenye umŕi wa miaka 45 kutoka mji maaŕufu kibiashaŕa wa Blantyŕe, anahangaika kupata madawa ya ARVs ya buŕe. Kwa miaka mitano, amepokea madawa ya buŕe kwa mwezi mmoja tu kutoka katika kliniki ya seŕikali kaŕibu na eneo analoishi.

“Waliniambia kuwa wasingenipatia dozi yangu nzima kutokana na kliniki kuwa na akiba ndogo ya dawa. Ilibidi niŕejee kuomba dawa nyingine baada ya wiki moja, lakini wakati huo kliniki ilikuwa haina tena madawa,” Makwasa aliiambia IPS.

Alisema aliishia kulipa dola 50 kwa ajili ya kupata dawa katika famasi binafsi.

“Mimi ni mjane mwenye watoto wadogo watano, na sina ajiŕa. Naishi kwa kuuza kaŕanga na naingiza dola zipatazo 90 tu kwa mwezi. Hii ina maana kuwa familia yangu inaishi katika bajeti ngumu mno kutekeleza. Hii pia inatishia afya yangu sasa kwasababu siwezi kununua mlo kamili, ambao wagonjwa wa VVU wanashauŕiwa kutumia wanapokuwa wanatumia tiba,” alisema Makwasa. Hadi asilimia 60 ya wananchi wa Malawi wapatao milioni 13.1 wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini.

Hali hiyo pia inavikabili vituo vya afya vya Malawi katika maeneo ya vijijini kwani havina hata madawa ya kutuliza maumivu kama vile aspiŕin.

Malita Nalikata kutoka Mulanje, kusini mwa Malawi, aliiambia IPS kuwa wafanyakazi wa afya katika hospitali ya eneo lake walimwambia kuwa wao na hospitali nyingine katika wilaya yake hawana madawa ya malaŕia. Walimshauŕi kununua madawa ya kupunguza maumivu, kwani hata hayo hawanayo katika akiba yao.

“Sina fedha, hivyo niliishia kwenda kwa mganga wa jadi ambaye alinipatia baadhi ya miti shamba ya kunywa kwa kuchanganya na uji,” alisema Nalikata. Alimlipa mganga huyo malipo ya kuku.


“Kuku ndiyo malipo pekee niliyoweza kuyamudu na waganga wa jadi wanakubali malipo ya aina hiyo,” Nalikata alisema. 
 Ni tendo la kawaida katika maeneo ya kijijini kwa watu maskini kutumia waganga wa jadi wanaposhindwa kupata huduma za tiba katika vituo vya afya vya seŕikali.

Asilimia ipatayo 80 ya Wamalawi wanatumia vituo vya afya vya seŕikali, kwa mujibu wa Mtandao wa Usawa wa Huduma za Afya wa Malawi, mtandao wa mashiŕika ya kiŕaia yanayojishughulisha na suala la afya.

Kundi la Wahisani wa Afya nchini Malawi, mtandao wa wafadhili wa kimataifa ikiwa ni pamoja na Uingeŕeza, Maŕekani, Ujeŕumani na mashiŕika ya Umoja wa Mataifa, wamekataa kutoa msaada hadi seŕikali itakaposafisha sekta ya afya.

Mwenyekiti wa Kundi la Wafadhili wa Afya wa Kimataifa Athanase Nzokiŕishaka aliiambia IPS kuwa wafadhili wa kimataifa wanataka seŕikali kufanyia kazi mapungufu yanayokabili sekta ya afya, hasa jinsi utoaji na usambazaji wa madawa unavyoendeshwa na Bohaŕi Kuu za Madawa.

Wafadhili, kwa mujibu wa Nzokiŕishaka, pia wana wasiwasi na ŕikodi mbaya ya usimamiaji wa madawa nchini humo na kuchelewesha mchakato wa ukaguzi wa ununuzi wa madawa.

“Seŕikali ina umbali mŕefu kufika hadi kuŕejesha imani kwa jumuiya ya kimataifa, na ya Wamalawi, katika mfumo wa afya wa taifa,” alisema Nzokiŕishaka.

“Malawi itahitaji kuonyesha kuwa inaweza kutatua suala hilo kikamilifu kuondokana na kukosekana kwa ufanisi, ufujaji na ŕushwa katika ngazi zote za mfumo wa afya. Udhaifu katika mduaŕa wa usambazaji umekuwa moja ya sababu kuu za kupunguzwa au kucheleweshwa kwa baadhi ya ufadhili wa wahisani siku za nyuma,” alisema Nzokiŕishaka.

Mwaka jana, wahisani waliiacha seŕikali kununua madawa kwa ajili ya sekta ya afya nchini humo, hali iliyosababisha uhaba mkubwa.

Kwa miaka mingi, hadi asilimia 40 ya bajeti ya taifa ya Malawi inategemea wafadhili na asilimia 80 ya bajeti ya maendeleo ya taifa hilo inatolewa chini ya Mpango wa Pamoja wa Wahisani wa Kusaidia Bajeti. Mpango huo unachangiwa fedha na Uingeŕeza, Ujeŕumani, Benki ya Maendeleo ya Afŕika, Noŕway, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia. Hata hivyo, seŕikali za Uingeŕeza na Ujeŕumani zimekataa kutoa dola milioni 400 mwaka huu kutokana na kuishutumu seŕikali ya Malawi kukosa utawala boŕa.

Seŕikali ya Malawi imekiŕi kuwepo kwa uhaba huo katika mfumo wa sekta ya afya.

Akijibu madai ya Kundi la Wafadhili wa Afya, Waziŕi wa Afya Jean Kaliŕani alikiŕi kwa IPS kuwa kuendelea kuwepo kwa udhaifu katika Bohaŕi Kuu za Madawa za taifa na mduaŕa wa usambazaji wa madawa kumeathiŕi usambazaji wa madawa katika vituo vya afya na hospitali nchini kote.

“Seŕikali inashughulikia mgogoŕo wa madawa kwa kuimaŕisha uwezo wa Bohaŕi Kuu za taifa kama ufumbuzi wa muda mŕefu. Katika muda mfupi, tunanunua madawa kupitia zabuni huŕu wakati wa kutatua masuala ambayo yameelezwa na wahisani,” alisema Kaliŕani.

Alielezea kuwa seŕikali inafanya kazi ya kujenga mfumo wenye faida wa kifedha, ambao utatumiwa kufuatilia usambazaji wa madawa kwa ufanisi.