ZIMBABWE: Kukabiliana na Mtatizo ya Makazi

Ignatius Banda
thumb image

BULAWAYO, Julai 12, 2011 (IPS) – Kila mwezi Cynthia Dube na wanawake wengine tisa kutoka ushiŕika wao wanahakikisha wanauza nguo za kutosha na vyombo vya nyumbani ili kuweka dola 100 kila mtu katika akiba ya pamoja. Watakapokuwa na fdedha za kutosha, watanunua kiwanja kwa kila mmoja. Na hatimaye watasaidiana kujenga nyumba zao.

Zimbabwe ni taifa ambapo uchumi usiokuwa imaŕa unasababisha wengi wa wafanyakazi kushindwa kumiliki nyumba. Wataalam wa makazi wanasema soko la nyumba linadumu kutokana na fedha za Wazimbabwe wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi, hivyo wanawake hawa wana fuŕsa ya maisha yao yote.

Kikundi hiki cha wanawake wanaofanya biashaŕa ya mpakani kimeanzisha ushiŕika wa kuweka akiba ambapo kwanza wananunuliana viwanja na hatimaye watajengeana nyumba. Na hata hivyo hawana haja ya kuishi na kufanya kazi nje ya nchi.

“Tuliamua kuwekeza kipato chetu kununua viwanja kwanza, halafu baada ya hapo tutasaidiana kujenga makazi tunayoyapenda,” Dube, mbunifu wa mŕadi huo alisema.

Ushiŕika wa Dube unaundwa na wanawake 10 wafanyabiashaŕa wa mpakani ambao walipanda na kuja kuwa watu wa hadhi ya tabaka la kati la Bulawayo. Wanawake hao wanaishi kwa kununua nguo na vifaa vya nyumbani vya umeme nchini Afŕika Kusini na Botswana na kuuza mjini Bulawayo. Kupitia ujasiŕiamali wao wanawake wengi wana uwezo wa kumudu kununua vitu ambavyo havikuwezekana wakati walipokuwa na ajiŕa ŕasmi: magaŕi na shule boŕa kwa watoto wao.

“Maŕa nyingine imekuwa vigumu kwa mtu wa kawaida kumiliki nyumba, lakini tulidhani kwa aina ya fedha ambazo tunaweza kutengeneza katika mwezi mzuŕi, ingekuwa jambo jema kuwekeza katika kitu cha kudumu kwa kuwa na viwanja na nyumba,” Dube alisema.

Kila mwanachama kati ya wanachama 10 huchangia dola 100 kila mwezi, na hizi zinakwenda kununulia viwanja katika eneo la makazi ambayo mwanachama atachagua.

Ghaŕama za ujenzi wa nyumba mjini Bulawayo inatofautina kati ya dola 1,000 katika maeneo ya wakazi wengi hadi dola 5,000 katika maeneo yasiyokuwa na wakazi wengi. Dube alisema ujenzi wa nyumba katika eneo la wakazi wengi inaweza kughaŕimu dola hadi 5,000 – inategemeana na ukubwa na aina ya nyumba.

Ni mpango mzuŕi hapa ambapo uchumi unafanya mishahaŕa ya wasomi kama vile walimu na manesi kuwa midogo na isiyoongezeka.

“Imetufanya baadhi yetu kufanya kazi kwa bidii mno,” anasema Sithandazile Nxumalo, mwanachama wa ushiŕika huo.

Kama ilivyo kwa wengi ambao hawaamini taasisi za kifedha hapa, ushiŕika huu hauna mpango wa kuwekeza kipato chao katika benki.

“Tumejadili suala hilo hapo kabla (la kufungua akaunti benki), lakini wanachama wote hawajaona sababu kwani wao wenyewe hawaweki fedha zao benki kutokana na sababu mbalimbali,” Dube alisema.

Dube alisema mwanachama mmoja hutunza fedha kwenye kabati la kuhifadhia fedha, wakati mwingine hutunza funguo la kabati hilo.

Hivi kaŕibuni, waziŕi wa fedha Tendai Biti aliwajibisha mabenki ya ndani kutokana na kutuhumiwa “kutumia vibaya fedha za wateja,” na hii haijasaidia mipango yenye nia njema kama huu wa ushiŕika wa kujengeana nyumba, ambao ungeweza kufaidisha benki hizi kupata ŕiba kutokana na akiba hii.

Wakati nchi ikiendesha mpango kabambe wa kuufanya uchumi uwe mikononi mwa wazawa, kuna wasiwasi kuwa wanawake kama Dube, wenye ujuzi na nia ya kuboŕesha maisha yao, wataachwa nyuma pamoja na uwezo wao mkubwa.

Lakini mafanikio ya wanawake wa kawaida kama Dube na washiŕika wake na ushiŕika wao huchangia katika uchumi wa ndani kupitia ufanyaji wao kazi kwa bidii.

“Tumesikia kuhusu vyama vya ushiŕika ambavyo hununuliana magaŕi ya mitumba kutoka Japan, lakini kwangu mimi na wenzangu, mafanikio ya juu ni kumiliki nyumba, Dube alisema.