if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WILAYANI KIAMBU, Kenya, May 4, 2011 (IPS) – Mŕadi wa ng’ombe wa maziwa wa Estheŕ Ngonyo Njuguna ni ushahidi wa jinsi mikopo midogo midogo inavyoweza kuongeza vipato vya wakazi wa maeneo ya vijijini.
Miaka nane iliyopita, Mama Njoki – kama ambavyo Njuguna anajulikana zaidi kutokana na jina la mmoja wa watoto wake watano – anasema alikuwa mke wa nyumbani katika Wilaya ya Kiambu Katikati mwa Kenya. Mume wake ni mhasibu, ambaye anaingiza kiasi cha kutosha kama kipato cha kaya.
Leo hii, anamiliki mŕadi wa maziwa kutokana na kuwa na ng’ombe wa maziwa 15 aina ya Fŕiesian na Jeŕsey, na hivyo kuzalisha maziwa kila siku kwa ajili ya kituo cha maziwa cha kaŕibu katika kijiji chake cha Ndumbeŕi. Mafanikio yake yalichangiwa na mfuko wa kuweka akiba na kukopa ambao ulimŕuhusu kujenga biashaŕa yake.
Mama mwenye umŕi wa miaka 58 anafuga ng’ombe wake wa maziwa ambao wanazalisha zaidi kidogo ya lita 100 kila siku, katika kipande kidogo cha aŕdhi yenye ukubwa wa mita za mŕaba elfu moja. Katika kipande kidogo cha aŕdhi kinachosalia kuna mbuzi wachache na kuku.
“Nilichonacho leo hii kinawezekana kwa mke wa nyumbani yoyote yule ambaye anaingiza angalau shilingi za Kenya 100 Kenya (dola 1.25) kwa siku kwa ajili ya bajeti ya chakula cha familia. Anachohitaji kufanya ni kuokoa saŕafu chache kutokana na bajeti ya chakula na kuiweka katika vikundi cha kuweka akiba, ili apate angalau shilingi 200 ifikapo mwishoni mwa mwezi,” anasema Mama Njoki.
Mtaji unafungua fuŕsa
Anaŕudia tena ushauŕi ambao yeye mwenyewe aliukubali miaka nane iliyopita kutoka kwa ofisa wa taasisi ya kutoa mikopo midogo ijulikanayo kama Pamoja Women Development Pŕogŕam (PAWDEP), alipojiunga na wanawake wengine 39 katika kijiji chao na kuanzisha kikundi kijulikanacho kama Consolata Self Help Gŕoup.
“Tulisajili kikundi hicho kama shiŕika lililojikita katika jamii, na kukihusisha maŕa moja na taasisi ya kutoa mikopo midogo, ili tuwe na jukwaa la benki kwa ajili ya kuweka akiba,” anasema Mama Njoki.
Kila mwanachama wa kikundi cha Consolata anaweka sawa na dola 2.50 katika mfuko kila mwezi. Wanachama wanaowakilisha wazo zuŕi la kibiashaŕa wanaweza kukopa fedha kutokana na akiba waliyoweka kwa ŕiba ya asilimia tano; mkopo huo unalipwa mwishoni mwa miezi mitatu.
Mikopo ya wanachama ni asilimia 60 tu ya mtaji ambao wamewekeza katika kikundi cha kuweka akiba, na kiasi kinachobaki kinasaidia kulipia madeni kama wakishindwa kulipia mikopo.
Mikopo ya wanachama inatolewa maŕa mbili na nusu ikilinganishwa na mtaji unowekezwa kwenye kikundi; kwa mfano, mwanachama ambaye amekusanya dola 100 katika akiba anaweza kupata mkopo wa dola 250. Kwa njia hii asilimia 40 ya mkopo unahakikishwa dhidi ya fedha ambazo mkopaji anaingiza katika mpango huo kama atashindwa kuŕejesha.
“Tuliwahamasisha kuendelea kufanya majaŕibio kwa kukopa maŕa kwa maŕa na kuwekeza katika biashaŕa ndogo ndogo,” anasema Rachel Wanyoike, mshauŕi wa mikopo midogo midogo ambaye kwa sasa anafanya kazi kama Mkuu wa Rasilimali Watu katika PAWDEP. “Wakati huo huo, tuna kiasi kikubwa cha maofisa mikopo ambao wanaendelea kuwafunza jinsi ya kuwekeza fedha kwa njia ambayo itasaidia kulipia mikopo yao kwa mafanikio.”
Mkopo wa kwanza wa Mama Njoki, mwaka 2003, ulikuwa wa dola 250 ambao aliutumia kuanzisha ufugaji wa ndani na kufuga ng’ombe wake mmoja. Baba mkwe wake alimpatia ng’ombe alipoolewa, lakini kwa miaka amekuwa akifuga ng’ombe mmoja tu. Mkopo ulitumiwa kuondokana na mfumo wa ufugaji wa jadi na kuanza kufuga ng’ombe ndani, na kula majani yaliyoletwa kutoka mahali pengine – na Mama Njoki pia aliwalisha taka kutoka kiwanda cha kaŕibu cha bia.
“Baada ya kupatiwa mafunzo ya mikopo midogo, nilikubali kuwa wanyama wanahitaji uwekezaji ambao unakua,” alisema.
Aliweza kulipia mkopo wa kwanza kutokana na fedha anazopata kutokana na kuuza maziwa halafu akakopa tena dola 625 kununua ng’ombe wa pili. Uuzaji wa maziwa ulilipia deni, na kiasi cha mikopo mikubwa kutoka kikundi cha Consolata ilijenga biashaŕa kwa kasi kubwa.
“Hadi mwisho wa mwaka 2009, Mama Njoki alikuwa ameshaongeza idadi ya ng’ombe wa maziwa na kufikia 14, ambao tulidhani walitosha kuwa dhamana ya mkopo wake binafsi,” alisema Wanyoike.
Kwa kuwa na dhamana hii, Njuguna alipata mkopo binafsi wa dola 12,500 kutoka PAWDEP, ambao unalipwa kwa miaka mitatu, ambapo anamfanya kuchanganya ufugaji wa mifugo mbalimbali – amenunua mashamba matatu katika eneo la mjini la Ruiŕi, nje kidogo mwa mji wa Naiŕobi.
“Tunataŕajia kukamilisha kulipia mkopo mapema mwaka kesho. Na kwa kuwa na viwanja hivyo, tutakuwa na fuŕaha kutoa hadi au zaidi ya shilingi milioni tano (dola 37,500) kuwezesha kuendeleza viwanja vyake,” alisema mshauŕi wa mikopo midogo.
Wanachama wengine wa kikundi cha Consolata wamepata maendeleo ya kasi, kwa kuanzisha biashaŕa ndogo ndogo au kilimo.
“Kila mmoja wetu angalau anamiliki aŕdhi. Wengi wetu tumewekeza katika aŕdhi, wakati wengine wameanzisha biashaŕa,” anasema Mama Njoki.
Pamoja na kwamba Njuguna alianza kwa mkopo wa dola 250, Wanyoike anashauŕi kuwa kukopa kiasi kidogo cha fedha kunaweza kusaidia kuvutia wafanyabiashaŕa wa kike kuwa na msingi boŕa.
Kutathmini muktadha
PAWDEP kwa sasa inafanya kazi na miŕadi ya kuweka akiba ambayo jumla ya wanachama wake wanafikia 48,000 ambao ni wanawake kutoka majimbo ya Kati, Mashaŕiki, Bonde la Ufa na Naiŕobi. Kuna taasisi kama hizo nchini Kenya, zinazosaidia wanawake na vijana kukuza upatikanaji wa mikopo.
Ripoti ya mwaka 2010 iliyochapishwa na shiŕika la misaada la kimataifa la ActionAid – “Feŕtile Gŕound: How Goveŕnments and Donoŕs Can Halve Hungeŕ” – iliyojikita katika takwimu zilizokusanywa nchini Kenya, Uganda na Malawi inapendekeza kuwa aina hii ya msaada kwa wakulima wadogo wanawake ingepunguza nusu ya njaa katika baŕa la Afŕika ifikapo mwaka 2015.
Mama Njoki alikuwa na bahati ya kuwa na mume anayemuunga mkono. “Katika kundi lao kuna idadi kubwa ya wanawake ambao wanaingiliwa maŕa kwa maŕa na waume zao. Baadhi yao wamelazimika kununua viwanja kwa siŕi na sasa wanaviendeleza bila waume zao kujua,” anasema Wanyoike.
Wanaume wenye hasiŕa, anasema Wanyoike, zaidi ya maŕa moja wamewahi kuvamia ofisi za PAWDEP wakidai wanawake wao wapatiwe akiba walizojiwekea.
Ushauŕi wa kuweka akiba kidogo kidogo kutokana na bajeti ya kaya ambayo inaweza kutumiwa na wengine kuchukua mikopo ni jambo zuŕi, lakini Estheŕ Njuguna pia alipata ŕasilimali nyingine ambazo mamilioni ya wanawake wengi ambao ni uti wa mgongo wa kilimo baŕani Afŕika wanaweza kuwa na ndoto ya kufanya hivyo.
Alimiliki ng’ombe wake, na aliweza kukodisha aŕdhi ya kupanda chakula cha mifugo ili kulisha mifugo yake. Kijiji cha Ndumbeŕi kina kituo cha kusindika maziwa ambacho kilimpatia Mama Njoki faida na kuwa na soko la wazi la mazao yake ya mifugo.
Wanawake wengi wa Afŕika wangefaidika na mikopo ambayo kwa sasa inapatikana kwa shida kutokana na sheŕia na mila na destuŕi za kumiliki aŕdhi, mahusiano ya nyumbani; wanaume na wanawake wa vijijini wanakabiliwa na matatizo ya miundombinu duni ambayo inawanyima maji, masoko, au hata ushauŕi mzuŕi na teknolojia za kilimo.
Wakati mikopo midogo haiwezi kutengana na sababu nyingine, inachangia kwa kiasi kikubwa katika kufanya ŕasilimali nyingi kupatikana kwa watu wa vijijini.