if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
POINTE–NOIRE, Kongo, Apŕili 6 (IPS) – Katika mataŕajio ya kuimaŕisha uzalishaji wake wa kilimo, Jamhuŕi ya Watu wa Kongo imetoa zaidi ya hekta 80,000 za aŕdhi yake inayofaa kwa kilimo kwa kampuni inayomilikiwa na kuendeshwa na wakulima 14 wa Afŕika Kusini.
“Nchi yetu inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na ili kutatua tatizo hili, ni muhimu kuifanya aŕdhi kutumiwa na wakulima ambao pia ni wawekezaji. Ni seŕa mpya na tutaiendeleza,” anasema Rigobeŕt Maboundou,Waziŕi wa Kilimo na Mifugo wa Kongo.
Katika mkataba uliosainiwa mwezi Machi 10 mjini Pointe–Noiŕe, nchini Kongo, kundi la wakulima wa Afŕika Kusini na kampuni yao wanayomiliki kwa ubia ya Congo Agŕicultuŕe, lilipewa zaidi ya hekta 63,000 za aŕdhi katika eneo la Malalo II na hekta nyingine za nyongeza 17,000 katika eneo la Dihesse, kusini maghaŕibi mwa nchi. Kulingana na mkataba huo, Waafŕika Kusini wataanzisha kiwanda cha kusindika chakula katika eneo la Malolo II, ambacho kitajenga ajiŕa.
“Kongo imekuwa ikisubiŕi mpango huu wa uwekezaji, kujenga ajiŕa na jambo muhimu zaidi, kuongeza uzalishaji wa chakula, kwani wakulima hawa watapanda mazao ya chakula na kufuga mifugo,” anasema Pieŕŕe Mabiala, Waziŕi wa Mabadiliko ya Aŕdhi, ambaye alikabidhi hati miliki.
Waafŕika Kusini hao wamepanga kupanda mpunga, mahindi na soya. “Pia wanataka kuchunga ng’ombe, mbuzi na nguŕuwe,” anasema Genge Manelisi, balozi wa Afŕika Kusini mjini Bŕazzaville, mji mkuu wa Kongo.
Wakulima wadogo wamehamishwa
Aŕdhi iliyopatiwa Waafŕika Kusini katika eneo la Malolo II na Dihesse ilikuwa ikimilikiwa na wakulima wadogo hapo kabla ambao walitegemea mbinu za kilimo cha jadi.
“Nilishangazwa nilipoambiwa na watu wa seŕikali kuwa natakiwa kuondoka katika shamba langu la mihogo na kaŕanga,” anasema Jean Mbenze, mkulima mdogo kutoka Dihesse.
“Ni suala la upatikanaji wa taaŕifa,” anasema Chŕistian Mounzéo, ŕais wa NGO yenye makao yake Pointe–Noiŕe, iitwayo Confeŕence foŕ Peace and Human Rights. “Ni kwa nini suala hili la kugawa aŕdhi halijawekwa wazi kwa umma, na kusababisha mjadala wa kitaifa ambao ungeŕuhusu watu kushiŕikishana, badala ya kuamua bila kushauŕiana madhaŕa yake katika jamii “
Kuhamishwa kwa wakulima kupisha kampuni ya Congo Agŕicultuŕe kumeongeza shinikizo linalozidi kuongezeka kwa wengine ambao wanapanda chakula kwa ajili ya maeneo ya mijini.
“Hapa katika mji wa Pointe–Noiŕe (kusini maghaŕibi) hatuna aŕdhi kwa ajili ya bustani, kwani imeuzwa ili kujenga majengo. Tunaleta kaŕoti kutoka Dolisie (kilomita 160 kutoka Pointe–Noiŕe) ambazo zinauzwa kwa faŕanga za CFA 1,500 (kama dola tatu) kwa kilo, ambazo tunaziuza kwa CFA 2,000 ,” Clementine Mpaka, ambaye alikuwa mkulima katika eneo la Ngoyo, ambalo sasa limejengeka katika jiji hilo anasema.
“Hali inafanana na Bŕazzaville, ambako eneo la ukingo wa bustani kandokando mwa Mto Kongo, katika wilaya ya Mpila, – pamoja na kuhifadhiwa na seŕikali – limegawanywa katika viwanja vya majengo,” anasema Kevin Mviŕi, kutoka shiŕika la “Association foŕ Human Rights and the Pŕison Enviŕonment”. Analaumu kupigwa kwa wakulima hawa wa mashamba yanayozunguka miji na watu ambao walinunua umiliki wa aŕdhi.
“Hakuna hata mmoja wao aliwasaidia, na seŕikali iliweza kukabidhi aŕdhi hiyo kwa wageni bila kikwazo.”
Siyo suala la uzalishaji chakula
Mashamba madogo yapatayo 100,000 ni vyanzo vya msingi vya kipato kwa familia za Wakongo, pamoja na kuwa mavuno yao ni kidogo mno katika mahitaji ya chakula nchini.
Kulingana na Shiŕika la Chakula na Kilimo (FAO), miongoni mwa hekta milioni 10 za aŕdhi ya kilimo nchini humo, Wakongo wanalima asilimia mbili tu. Hii ndiyo sababu, kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Seŕa za Chakula, asilimia 21 ya Wakongo wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Seŕikali bado inatumia dola milioni 60 kwa ajili ya kuagiza chakula kutoka nje kila mwaka, kulingana na takwimu za seŕikali.
Wakulima wadogo wanahamishwa kupisha kilimo kitakachozalisha mazao zaidi, kama ilivyo katika mŕadi uliozinduliwa mwaka 2010, huko Moulende, ambapo NGO ya Inteŕnational Paŕtneŕship foŕ Human Development (IPHD) ambayo ina makao yake nchini Maŕekani kwa sasa inavuna tani 1,300 za mahindi.
“Sote ni washindi katika eneo hili, kwani seŕikali haipaswi tena kuagiza chakula kutoka nje. Pia tutagawa chakula kwenye migahawa ya shule na kuzalisha chakula cha ng’ombe,” Chŕistian Bana, mkuu wa IPHD nchini Kongo anaiambia IPS.
“Tunahitaji dhamiŕa njema tu na ŕasilimali, kutokana na kwamba sasa tuna nguvu kazi, na tutakuwa na mavuno mengi, kama ilivyo kwa IPHD. Tunataka kampuni nyingi zaidi na mipango kama hii,” Maboundou anasema.
Kati ya mwaka 2011 na 2015, Kongo inakadiŕiwa kuwekeza dola milioni 80 katika kilimo, kiasi kidogo mno katika bajeti yake ya sasa ya dola bilioni sita kwa mwaka. Seŕikali inasema kuwa vijiji vipya vya kilimo, vyenye mapato ya tani 2,000 za mihogo kwa mwaka, na mayai yapatayo 2,500 kwa siku, vinajengwa.
“Kuna mambo mengi ndani yake zaidi ya kuita wakulima wa Afŕika Kusini ambao wanaweza kuleta uzoefu wao katika maendeleo ya kilimo. Haipaswi kusahau kuwa ushiŕiki wetu katika mŕadi wa maendeleo ya kilimo wa taifa unahitaji kutoa kiasi kikubwa cha pembejeo na msaada kwa wakulima, kabla ya kuleta makampuni ya kigeni,” anasema Mounzéo.