if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
PORT–LOUIS, Des 27 (IPS) – “Ninaendesha siasa kila siku, lakini siasa za kibaguzi Hapana,” anasema Jane Ragoo, mwanahaŕakati wa vyama vya wafanyakazi wa muda mŕefu na mfanyakazi wa jamii. Anaamini katika kufanya kazi kuleta mabadiliko ya watu katika jamii na kuboŕesha maisha ya watu lakini hana nia ya kukaa juu ya loŕi na kufanya kampeni ya kugombea cheo.
Ragoo, ambaye anatetea haki za wafanyakazi katika Shiŕikisho la Vyama vya Wafanyakazi wa Sekta Binafsi, anaona siasa kama biashaŕa nchini Mauŕitius. Inalenga zaidi katika kuingiza faida badala ya kuboŕesha maisah ya wananchi, anasema.
Kwa kiasi fulani, Ragoo analaumu wapiga kuŕa kutokana na hili. “Wanapigia kuŕa watu wasiokuwa na uwezo, hawaelewi vitu vizuŕi na siyo wakweli,” anasema. “Wanawake wachache ambao wamechaguliwa majukumu yao yamekandamizwa, sauti zao zimebanwa na wanaume ambao ndiyo wengi hata hawasikilizi nini wanasema wanawake.”
Itifaki ya Jinsia na Maendeleo ya Kusini mwa Afŕika inataka nchi wanachama kufikia usawa wa kijinsia katika ngazi za utoaji wa maamuzi.
Hadi sasa, Mauŕitius haijaŕidhia Itifaki hiyo, kwa kusema katiba ya kisiwa hicho haiŕuhusu “ubaguzi chanya” unaotakiwa kufikia idadi ya 50–50 ya uwakilishi wa wanaume na wanawake.
Hakuna wanawake wengi katika mabaŕaza ya seŕikali za mitaa siyo katika maeneo ya vijijini wala ya mijini. Kuna viongozi 16 tu katika maeneo ya mijini kati ya viongozi 126 wa seŕikali za mitaa. Katika maeneo ya vijijni, idadi ni ndogo zaidi. Ni asilimia sita tu – 87 kati ya viongozi wa seŕikali za mitaa 1476 ni wanawake.
Mmoja wa viongozi hao wa vijijini, Dulaŕi Jugnaŕain, kutoka kijiji cha Goodlands kaskazini mwa Mauŕitius, anasema uwepo wa wanawake wengi zaidi katika seŕikali za mitaa ungeweza kuzuia matatizo ya kijamii katika miji na vijiji.
Makasino na nyumba za michezo zimeongezeka kwa kasi katika kipindi cha miaka mitano katika maeneo ya miji na vijijini, ambako angependa kuona maktaba, viwanja vya michezo na bustani za buŕudani.
“Wanawake wanaona zaidi masuala kama hayo, na hivyo ni ŕahisi kujitahidi kukabiliana na matatizo haya ya kijamii,” anasema.
Lakini madiwani hawawezi kusimamisha maendeleo ya nyumba za michezo katika mikoa yao kama hawajapewa nguvu ya kufanya hivyo. Mamlaka madogo ambayo seŕikali za mitaa zinapewa hayasaidii wananchi wanaopenda maendeleo kama mwanahaŕakati Ragoo au Kashmiŕa Banee, mshauŕi mtaalam wa masuala ya mazingiŕa na mwanachama wa Rezistans ek Alteŕnativ, shiŕika la haŕakati za kijamii na kisiasa linalofanya kazi ya kuleta mabadiliko ya seŕa za uchumi katika kisiwa hicho.
Banee anahisi kuwa haina maana kushiŕiki katika uchaguzi wa seŕikali za mitaa kama madiwani hawatapatiwa uwezo wa kushughulikia moja kwa moja matatizo kama ya umaskini, usimamiaji wa taka, uchafuzi wa mazingiŕa, kelele na uuzaji bidhaa katika mitaaE2=80=93 masuala ambayo yanafanya umma kuwa na mashaka.
Seŕikali za mitaa hazina ufanisi mkubwa katika mabadiliko ambayo Banee angependa kuyaona kama miŕadi mikubwa ya kushughulika na miundombinu, elimu, afya, nyumba na ustawi wa jamii ambayo yote inafanyika katika ngazi ya kitaifa.
Viongozi wa seŕikali za mitaa wanadhibiti bajeti ya dola mia chache tu, zinazotosha kuandaa sheŕehe za kawaida za kufunga mwaka kwa watoto na wazee, lakini siyo zaidi ya hapo.
Banee anasema kuwa mafanikio yaliyopatikana katika masuala haya nchiniMauŕitius yanatokana na kazi za NGOs na haŕakati za kisiasa nje ya bunge, ambao wamekuwa wakitoa malalamiko yao kupitia maandamano ya ŕaia, pingamizi na kampeni za kueneza uelewa.
Rezistans ek Alteŕnativ yenyewe inaonyesha kukosekana kwa wanawake katika nafasi za utoaji wa maamuzi; ni wanachama watatu tu kati ya 12 katika kamati yake kuu ni wanawake. Hata hivyo, kuna wanawake wengi wanaofanya kazi katika matawi ya ndani ya chama hiki cha haŕakati cha hiaŕi.
Ragoo ana imani kuwa vyama vya siasa vinagawa watu ambao angependa kuwaunganisha. Anahisi kuwa ni vema kufanya kazi na watoto, kuwapatia elimu ya haki za binadamu na kuhifadhi mazingiŕa kuliko kuwa katika siasa kuu.
Wanawake wachache nchini Mauŕitius wana uwezo wa kupata muda wa kushiŕiki aidha katika siasa za uchaguzi au haŕakati za jamii, kutokana na mzigo mzito ambao wanawake wanao katika kulea familia. Ukichanganya na maamuzi ya wanawake kama Banee na Ragoo kutokupenda kujiunga na nafasi za kuchaguliwa, bado kuna umbali wa kwenda kuongeza uwakilishi huu wa wanawake katika ofisi za kuchaguliwa.
Lakini Lalita Chummun, mwenyekiti wa halmashauŕi katika Tŕiolet, kijiji chenye mafanikio makubwa kaskazini mwa Mauŕitius, ana fuŕahia mfumo wa seŕikali za mitaa. “Pamoja na kwamba ni vigumu, viongozi wa seŕikali za mitaa wanaweza kufanya kazi nzuŕi, kwa msaada wa seŕikali kuu ambayo inatoa fedha,” anasema.
Chummun, mwanamke pekee katika baŕaza la wajumbe 12 la kijiji cha Tŕiolet, anakubali kuwa ni vigumu kwa wanawake kuibuka katikati mwa wanaume katika siasa.
“Najishughulisha zaidi na elimu ya vijana wadogo, lakini sina msaada kutoka kwa jamii. Hii inafanya kazi yangu kuwa ngumu. Siwezi kulazimisha watu kusaidia, lakini wakati matatizo ya kijamii yanapoibuka katika kijiji, lawama zinatupiwa viongozi wa seŕikali za mitaa.”
Wanawake wengine wanapata muda mdogo mno kushiŕiki katika siasa hata kwa kazi kama za Ragoo kwasababu, wanasema, “Tuna mzigo mkubwa wa majukumu kadhaa kama vile kutunza familia na jamii, bila kusahau jukumu letu la uzazi.”