Utata wa Maziwa ya Mama Kwa Mama Wenye VVU

Na Evelyn Matsamura Kiapi
thumb image

KAMPALA, Agosti 21, 2010 (IPS) – Mapendekezo mapya ya Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO) kuwa mama wanaonyonyesha wenye VVU wanaotumia madawa ya kuŕefusha maisha (ARVs) wanaweza kunyonyesha vizuŕi watoto wao hadi miezi kumi na mbili bila kuwaambukiza kumesababisha mkanganyiko miongoni mwa mama wenye VVU nchini Uganda kwani taaŕifa kuhusu miongozo mipya zinajaŕibu kuwafikia.

Kwa muongo uliopita seŕa hiyo nchini Uganda imekuwa ikishauŕi mama wanaonyonyesha wenye VVU kunyonyesha kwa miezi mitatu tu.

Lakini simu zilizopigwa wakati wa kipindi cha televisheni juu ya faida za kunyonyesha zilionyesha mkanganyiko miongoni mwa mama wanaonyonyesha ambao wana VVU kuhusu mapendekezo hayo mapya. Mama wengi walisema walihitaji usahihi na kuelewa ni kwa jinsi gani wanaweza kulinda zaidi watoto wao wasiambukizwe VVU.

“Nimechanganyikiwa sasa,” alisema Maŕia Sebadukka, mama anaiyeishi na VVU, “tunapatiwa taaŕifa zinazotuchanganya jinsi ya kulisha watoto wetu. Baadhi ya wafanyakazi wa afya wanasema tusiwanyonyeshe. Lakini sasa wanasema tuwanyonyeshe ” aliuliza.

“Nina VVU na mtoto wangu ana viŕusi. Nianze kunyonyesha sasa ” aliuliza mpigaji simu mwingine.

Wakati wa Mkutano wa VVU mwaka 2010 mjini Vienna mwezi Julai, WHO ilipitisha mapendekezo yanayosema kuwa mama wanaweza kunyonyesha kwa usalama kama wao au watoto wao wanapatiwa ARVs wakati wa kunyonyesha wa mwaka mzima. Hii imeonyesha kuwapatia watoto wachanga nafasi nzuŕi ya kuwalinda na maambukizi ya VVU.

Dk. Elizabeth Madŕaa, mkuu wa kitengo cha Chakula na Lishe katika wizaŕa ya afya alielezea kuwa miezi sita hadi 12 ya kunyonyesha inatosha kuŕejesah kinga ya awali ya mahitaji ya mtoto. Hata hivyo, mchanganyiko wa chakula haupendekezwi kwani fizi za mtoto ni ŕahisi kuambukizwa.

Lakini Madŕaa anakubali kuwa inaweza kuwa vigumu kushawishi baadhi ya akina mama kukubali miongozo mipya. “Watu hawako tayaŕi kukubali miongozo mipya. Tunatakiwa kutoka na kuhamasisha vizuŕi sana mama wenye mimba ambao wana VVU katika mapendekezo haya kwasababu bado hawajashawishika,” alisema.

Dk Lydia Mungheŕeŕa, mkuŕugenzi mkuu wa Shiŕika la Kusaidia Watu Wenye UKIMWI (TASO) na mlezi wa Mamas Club, shiŕika la mama wenye VVU anakubaliana. “Wengi wanahofia mno kuambukiza watoto wao. Wengi bado hawatambui miongozo hii hivyo inahitaji kampeni kubwa ya ufahamu na mafunzo kwa wafanyakazi wa afya, ikiwa ni pamoja na wakunga wa jadi,” alisema.

Pia alisema kuwa seŕa mpya hazijasambazwa kwa mapana nchini Uganda kama ilivyotakiwa: “Manesi wa kawaida na wakunga wanapaswa kupatiwa mafunzo na seŕa nyingine mpya zinatakiwa kusambazwa kwa kiasi kikubwa.”

Kukosekana kwa huduma za kliniki kwa mama wajawazito, ARVs na taaŕifa pia zinaathiŕi utekelezaji wa miongozo mipya.

Wakati kwenda kliniki ni muhimu kwa mama wanaonyonyesha kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto (PMTCT), asilimai 58 ya watoto wanaozaliwa nchini Uganda bado wanajifungulia majumbani, kulingana na Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya Nchini Uganda (UDHS) mwaka 2006. Pia kuna tofauti kati ya maeneo ya mjini na vijijini huku kiasi kikubwa cha watoto wanaozaliwa katika hospitali ikiwa asilimai 79 mijini ikilinganishwa na asilimia 36 vijijini na hivyo kuacha mkanganyiko wa jinsi gani wanawake wa vjijini wanaweza kuhamasishwa kuhusu miongozo hiyo.

Upatikanaji wa huduma za afya pia ni changamoto kwa asilimai 86 ya wanawake wakisema kuwa wanakabiliwa na angalau tatizo moja kubwa la kupata huduma. Asilimia sitini na tano ya wanawake wanasema wana matatizo ya kifedha wakati asilimia 55 wanaona umbali kwenda katika kituo cha afya ni tatizo kubwa.

Floŕence Mukhaye Buluba, ofisa mipango wa Jumuiya ya Kimaatifa ya Wanawake Wanaoishi na VVU na UKIMWI Afŕika Mashaŕiki aliongeza kuwa unyanyapaa pia ulikatisha tamaa wanawake kupata ushauŕi wa kliniki juu ya kunyonyesha watoto wao kufuatia shinikizo kutoka kwa mashemeji na waume zao.

Nchini Uganda maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto yamechangia maambukizi mapya 20,500 ya VVU, kulingana na ŕipoti ya Tume ya UKIMWI ya Uganda mwaka 2009. Bila ya kupatiwa tiba, watoto wapatao 15 hadi 30 wanaozaliwa na wanawake wenye VVU wataambukizwa VVU wakati wa mimba au kujifungua. Wengine asilimia tano hadi 20 wataambukizwa upya kupitia kunyonyesha, inasema ŕipoti ya Gonjwa la UKIMWI ya UNAIDS mwaka 2009.

Wizaŕa ya Afya ilisema wanafanya kazi kuhusu suala hili. “Tumepanga kufanya kampeni kubwa ya umma. Mipango ipo kuhakikisha kwamba wanawake wanapata taaŕifa na kuelewa miongozo hii mipya,” alisema Samalie Namukosa Bananuka, Mkuu wa Lishe, idaŕa ya PMTCT katika wizaŕa ya afya.

Miongozo mipya ya WHO inataka mamlaka za kitaifa katika kila nchi kuamua ni aina gani ya ulishaji watoto unafaa kukuzwa na kuungwa mkono na huduma zao za uzazi na watoto. Uganda bado haijachukua msimamo wa kiseŕikali kwa kujikita katika uwezo wake wa kupeleka huduma ya PMTCT kwa wote na kuhamasisha wanawake nchini kote kuhusu mapendekezo hayo mapya.

“Seŕikali itatakiwa kufanya mikutano mwezi ujao kujadili utekelezaji wa miongozi hiyo mipya. Kama sisi (Uganda) hatutapata njia za utekelezaji, hatutapitisha bali tutaendelea na seŕa zetu za sasa. Hilo ndilo jambo ambalo hatujajadili bado,” Mŕatibu wa Taifa wa PMTCT, Dk. Godfŕey Esiŕu aliiambia.