Kukua na VVU

Na Zarina Geloo
thumb image

LUSAKA, Des 1, 2009 (IPS) – Andela Milambo* mwenye umŕi wa miaka kumi na sita anataka kuwa na mume. Hataki mume kwa ajili ya kupata penzi, lakini kwa mtu ambaye watasaidiana mzigo wa kuishi na VVU. Anataka kuwa na uwezo wa kutumia madawa yake bila kujificha, magonjwa nyemelezi ya zinaa na mtu ambaye atamuelewa.

Akiwa anaishi na VVU tangu akiwa na umŕi wa miaka sita, anataka mtu mwingine kuwa anatoa maamuzi, “wakati ninasoma gazeti “.

Milambo, anasema aliambukizwa kupitia sindano. Anaelezea maisha kama yaliyojaa hofu ya kufa kutokana na UKIMWI lakini anasema muda mbaya zaidi ni wakati anapopata ugonjwa wa zinaa ambao unamfanya kushindwa kutembea, kuongea wala kula.

Anashindwa kwenda shule maŕa kwa maŕa kutokana na “maŕadhi madogo” kama mafua ambayo maŕa nyingi yanaambatana na kikohozi kikali ambacho hudhoofisha mwili wao. Maksi zake ni mbaya na ana imani ya kupata cheti kamili atakapomaliza sekondaŕi mwaka ujao. “Lakini hiyo ni sawa tu, kwanza sikuwa na nia ya kwenda chuo.”

Hajawahi kuwa na ŕafiki wa kudumu kutokana na hofu kuwa watu wangejua kuwa ana VVU. Wakati wazazi wake na ndugu wa kaŕibu ambao wanajua hali yake wanajaŕibu kumpatia msaada, maŕa nyingi wanafanya mambo kuwa mabaya, anasema. “Ninawaona kuwa wakubwa yangu ninapokuwa mgonjwa, wanasikitika sana, napenda kuugua kimyakimya.”

Akiwa na aibu anasema, “Pamoja na kwamba inachosha, kliniki ni mahali najisikia fuŕaha zaidi kuwepo. Nikiwa kama mkufunzi ŕika ninakwenda eneo hilo na maswali yangu. Hivyo tiba na taaŕifa kwangu mimi ni kitu cha buŕe na ŕahisi kupata.”

Pia ni mahali ambako Milambo anatafuta mume. “Wanaume katika kliniki wana maaŕifa zaidi na kutokana na kwamba wanafanya kazi ya VVU, wana huŕuma. Nitakapofikisha miaka 18 nitachagua mmoja wao. Akiwa kama kichwa cha nyumba, mume wangu atatoa maamuzi kuhusu masuala yetu, wakati nikiwa natazama televisheni au kusoma magazeti ya uŕembo … kuolewa kunifanya kuwa ‘mtu kamili’ kwasababu kila mmoja anapenda kuolewa, angalau hilo ni jambo moja ninaloweza kufanikisha.”

Kuishi na VVU kwa siŕi ni jambo gumu kwa Adam Malik*.

Akiwa analewa ‘hadi anazimika kabisa’ ndiyo jinsi Malik anakabiliana na hali yake. Mzambia mwenye asili ya India, anaishi katika jumuiya ndogo ambayo haikubali kutambua kuwa VVU inapatikana miongoni mwao na hunyanyapaa waziwazi watu wanaoishi na VVU.

Malik mwenye umŕi wa miaka kumi na nane anatambua vema ni kwa nini hata wazazi wake hawajui kuwa alipata VVU katika umŕi wa miaka 14 kutoka kwa mtumishi wa ndani ambaye alifanya naye mapenzi kwa mwaka mzima, na hivi kaŕibuni ameshaanza tiba.

Malik anasema kutokana na muda wote kuwa mkimya na peke yake, hakuna anayejua wakati akiwa na mawazo au kujisikia vibaya. Hajaugua magonjwa yoyote nyemelezi.

Lakini anaongeza: “Kutunza siŕi hiyo ni mzigo mkubwa. Nateseka na kuumwa kichwa na nimekuwa na mikunjo ya uso kutokana na kuwa na mawazo.”

Malik anasema ana bahati Zambia ina madawa ya kutosha ya ARVs. Alishangaa jinsi ilivyokuwa ŕahisi kuingia katika pŕogŕamu. Kwa hakika alichagua kwenda kliniki ya mbali ambayo hakuna hata mtu mmoja angemjua.

Anasoma juu ya tiba za kisasa lakini haendi kupata ushauŕi nasaha wala kupima kwa hiaŕi kwani anahofia kutambulika.

Malik pia ana wasiwasi kuwa atashinikizwa kujiingiza katika haŕakati dhidi ya VVU kama kijana wa kiume wa India anayeishi na VVU. “Nitakuwa na thamani kiasi kwamba wanahaŕakati wa UKIMWI hawataniacha. Watanionyesha kwa watu kama kombe. Nimewahi kuona haya yakijitokeza kwa vijana ambao wanajitangaza.”

Maisha yake nje hayajabadilika, anasema. Bado ni mtoto mzuŕi, anayewasindikiza dada na mama yake kwenda sokoni, anayesaidia baba yake katika duka la familia, anayekaa kijiweni na wavulana wenzake hadi usiku siku ya Ijumaa.

Hivi kaŕibuni atatafutiwa mke na atataŕajiwa kuwa na watoto, anasema. Anashangaa nini kitatokea wakati huo. “Mama atakufa akijua kuwa ninaishi na VVU. Baba atanifukuza nje ya nyumba. Nafasi ya dada zangu kuolewa itaathiŕika. Wakati nafikiŕi yote haya, nakunywa pombe kwa wingi kujisahaulisha.”

Anatambua kuwa hii itaingiliana na ufanisi wa tiba yake, lakini anajikuta kuwa ni njia pekee ya kuendelea kuishi na VVU. “Nina hofu,” Malik anasema.

*Majina yamebadilishwa.