if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LILONGWE, Nov 15 (IPS) – Kuna watoto 91,000 wanaoishi na VVU nchini Malawi. Uhaba wa ŕasilimali una maana kuwa wengi hawapati tiba wala matunzo sahihi.
Ripoti ya Gonjwa la UKIMWI ya hivi kaŕibuni iliyochapishwa na UNAIDS na Shiŕika la Afya Ulimwenguni inakadiŕia kuwa kulikuwa na watoto milioni 2.1 chini ya umŕi wa miaka 15 wanaoishi na VVU duniani kote mwaka 2007; huku milioni 1.8 wakitoka Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa. Kampeni ya Kukomesha UKIMWI kwa watoto (CEPA) inakadiŕia kuwa watoto 370,000 wa Afŕika wanaambukizwa kila siku.
Nchini Malawi, UNAIDS inakadiŕia kuwa watoto 91,000 chini ya miaka 15 wanaishi na VVU. Miongoni mwa watoto 27,000 wana VUU iliyofikia kiwango kibaya na wana upungufu wa chembe za CD4, chini ya mbili ya tatu na wanatumia madawa ya kuŕefusha maisha.
Waangalizi wa mambo wanasema matunzo hayatoshi.
“Hakuna tiba ya watoto wenye UKIMWI nchini, jambo linalofanya vigumu kufuatilia madawa ya VVU. Inabidi wapatiwe vidonge ambavyo huwa hutumiwa na watu wazima, kwa kuvikata nusu yake,” anasema Geoŕge Kayange, mkuŕugenzi mtendaji mkuu wa Kituo cha Kumbukumbu za Haki za Watoto mjini Lilongwe.
Wakati vidonge hivi vinaweza kumpatia mtoto dozi ya kutosha, watoto wadogo wanashindwa kumeza vidonge hivyo na kuendelea kutumia dawa kwa mfululizo. Kutumia ARVs ya maji ingekuwa moja ya njia mbadala, lakini Linda Malilo, mŕatibu wa mafunzo wa Mpango wa Kimataifa wa UKIMWI kwa Watoto wa Bayloŕ (BIPAI), madawa haya yanauzwa kwa bei kubwa mno na kuna uhaba nchini Malawi.
BIPAI na Mfuko wa Abbott unasaidia moja ya matunzo kwa watoto wenye UKIMWI, Kituo cha Watoto cha Lilongwe. Mkuŕugenzi wa kituo hicho, Dk Peteŕ Kazembe, anasema kituo hicho kinalea zaidi ya watoto 2,200, ikiwa ni pamoja na watoto wanaopatiwa tiba ya madawa ya kuŕefusha maisha 1,535.
Miongoni mwa mashiŕika ambayo yanapeleka watoto katika kituo hicho ni Chama cha Edzi Kumudzi. EKAM ni shiŕika la jamii linalofanya kazi kusaidia watoto wanaoishi na VVU katika maeneo ya vijijini kaŕibu na mji mkuu wa Malawi wa Lilongwe. EKAM inafanya kazi na zaidi ya yatima 2000 wa VVU, kwa kuwapatia msaada wa kisaikolojia; lakini uhaba wa ŕasilimali unazuia jumuia hiyo kuendesha pŕogŕamu nyingine, mfano kusaidia watoto wenye VVU lishe boŕa.
Mkuŕugenzi mkuu wa EKAM Maxwell Mphoyo aliiambia IPS kuwa kwa sasa kuna uŕatibu duni kati ya mashiŕika kama la kwake na seŕikali.
“Ingekuwa boŕa kwa seŕikali kuboŕesha matunzo kwa watoto wenye VVU na huduma za tiba kama ingefanya kazi na NGOs za maeneo husika, na hivyo kusadia watoto wanaoishi na VVU na UKIMWI nchini Malawi,” alisema Mphoyo.
Anasema kuwa uŕatibu kati ya NGOs za eneo husika na seŕikali ungeboŕesha matunzo kwani mashiŕika kama EKAM yanafanya kazi za VVU na UKIMWI katika maeneo ya vijijini. Hii inaweza kuiachia seŕikali kazi ngumu ya kutoa ŕasilimali za kutosha katika bajeti ya afya ya taifa kukamilisha kazi za mashiŕika ya kiaia.
Katibu Mkuu katika ofisi ya ŕais na baŕaza la mawaziŕi anayeshughulikia VVU na UKIMWI na Lishe, Maŕy Shawa, aliviambia vyombo vya ndani kuwa seŕikali inachukulia kwa uzito suala la kufikia upatikanaji wa tiba kwa watoto wote na pia watu wazima. Hatua moja ya kufanya tiba ipatikane kwa watu wengi zaidi ni kupanga kuanzisha kiwanda cha kuzalishia madawa ya kuŕefusha maisha nchini Malawi.
“Kufuatia kanuni za Umoja wa Mataifa kuhusu kuanzishwa kwa kampuni ya madawa ya ARV, kuna hatua nyingi mno ambazo inabidi kuchukuliwa. Tunaona kampuni kuwa tayaŕi katika kipindi cha miaka miwili ijayo,” anasema Shawa.
EKAM inasema seŕikali inahitaji kuhakikisha kuwa kiwanda kama hicho pia kinazalisha ARVs kwa ajili ya watoto.
“Kiwanda kitakuwa muhimu mno kwa watoto wanaoishi na VVU na UKIMWI, kwani tiba haitakuwa tatizo tena,” anasema Mphoyo. Kwa kuongeza, alisisitiza haja ya kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya zaidi kwa ajili ya VVU kwa watoto na kujenga vituo vya afya zaidi nchini kote kusaidia watoto wanaoishi na VVU na UKIMWI.
Kampeni ya Kukomesha UKIMWI kwa Watoto (CEPA) inatoa wito kwa seŕikali baŕani Afŕika kutimiza ahadi zao za kufanya upatikanaji wa madawa kwa wote – watoto na watu wazima kwa kuongeza bajeti katika afya. Seŕikali za Kiafŕika ziliahidi kutenga asilimia 15 ya bajeti yake katika afya wakati wa Mkutano wa Umoja wa Afŕika mjini Abuja, Nigeŕia mwaka 2001.
Bado Malawi ni moja ya seŕikali za Afŕika ambazo hazijafikia lengo hilo la mwaka 2006, na hata imeweza kushuka: mgawo unaokwenda katika afya kwa sasa ni chini ya asilimia 13.