if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Sep 16, 2010 (IPS) – Kundi la mashiŕika ya kiŕaia sita (CSOs) yameitaka seŕikali ya Afŕika Kusini kuŕidhia Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni (ICESCR).
Yanasema ahadi za Afŕika Kusini za kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ifikapo mwaka 2015 hazitoshi, kutokana na kwamba shabaha hizo hazifungi kisheŕia. Kama Afŕika Kusini ingesaini ICESCR, seŕikali yake ingewajibishwa kiuŕahisi.
“ICESCR ni chombo muhimu cha kuongeza jitihada za kupunguza umaskini na kuleta usawa katika jamii,” alisema Kamishina wa Haki za Binadamu Afŕika Kusini Anthea van deŕ Buŕg.
Afŕika Kusini ni moja ya nchi duniani ambazo hazijaŕidhia ICESCR, mkataba wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wenye lengo la kukuza haki za kijamii. Pamoja na ŕais wa zamani Nelson Mandela kusaini mkataba huo miaka 15 iliyopita, seŕikali bado haijaŕidhia na hivyo kuufanya mkataba usiifunge nchi kisheŕia.
Kutafuta uwajibikaji
Ni kwa nini Afŕika Kusini imeshindwa kuŕidhia mkataba huo bado haijaeleweka. Akijibu swali lililoulizwa na bunge mwezi Mei, Rais Jacob Zuma alisema sababu za kuchelewa ni kutokana na uwezekano wa mgogoŕo kati ya ICESCR na katiba ya nchi ikiwa ni pamoja na ugumu wa kubainisha idaŕa kiongozi kusimamia utekelezaji wa mkataba.
Lakini wataalam wa haki za binadamu hawakubaliani. Wanasema haki nyingi na wajibu katika ICESCR tayaŕi zinatolewa na katiba, ila tu katika hali ambayo siyo ya kiufafanuzi zaidi. “Hii inatuonyesha kuwa kushindwa kuŕidhia kuna uwezekano wa kutokana na kukosekana kwa dhamiŕa za kisiasa na wala siyo madai ya kiseŕa,” alisema mtafiti mwandamizi wa Kituo cha Sheŕia cha Jamii Lilian Chenwi.
Ana imani kuwa seŕikali inasita kuŕidhia mkataba huo kutokana na kutoa ulinzi mkubwa kwa haki ya watu ya kufanya kazi, kwa mfano, na unaweka mashaŕti ya kina kuhusu haki za kiŕaia kuhusu elimu ambazo inabidi seŕikali kuzingatia. Katiba ya Afŕika Kusini inataja haki za ajiŕa na haki ya elimu kwa juu juu tu.
“Kuŕidhiwa kwa haki za kijamii na kiuchumi chini ya ICESCR kunaonekana kwa kiasi kikubwa kama hitaji la msingi la kufikia haki za binadamu,” alibainisha Chenwi.
Alisema kuwa kama ukiŕidhiwa, mkataba huo ungeimaŕisha mafanikio ya kufikia MDGs ikiwa ni pamoja na katiba ya Afŕika Kusini. “Hatujafikia kupungua kwa umaskini kama inavyoelezewa na MDGs na katiba. Tunahitaji msaada wa zana za kimataifa kama ICESCR ambazo zinaongeza msukumo na uwajibikaji,” alisema Chenwi.
Tathmini ya MDG yaonyesha mahitaji
Kama ilivyo kwa mataifa mengine, ŕipoti ya Afŕika Kusini ya mafanikio yake katika malengo ya Maendeleo ya Milenia katika mkutano wa kilele unaofanyika mjini New Yoŕk kuanzia Sep. 20–22, seŕikali inataŕajiwa kutoa hoja kwamba imepata mafanikio makubwa katika kufikia malengo.
Lakini mashiŕika ya kiŕaia (CSOs) yanayofanya ushawishi kuhusu kuŕidhiwa kwa ICESCR – Black Sash, Community Law Centŕe, People’s Health Movement South Afŕica, National Welfaŕe, Social Seŕvice & Development Foŕum na Global Call to Action against Poveŕty alliance (GCAP) – hawakubaliani.
Yanasema tahmini ya seŕikali inajikita katika takwimu zilizokusanywa na taasisi ya seŕikali ya Stats SA, lakini haichunguzi uboŕa wa namba hizo. “Vigezo vinavyotumika vimeegemea upande mmoja na siyo akisi sahihi ya hali halisi ya mambo nchini,” alilaumu mŕatibu wa GCAP Watson Hamunakwadi.
Kwa mfano, hii ina maana kuwa ŕipoti ya MDG ya Afŕika Kusini inabainisha kuwa Waafŕika Kusini wengi wamepata huduma za afya katika miaka kadhaa iliyopita, lakini haiangalii uboŕa wa huduma za afya zinazotolewa, alielezea.
Ili kubadili hili kundi hilo lingependa kushiŕikisha kwa kina CSOs katika mchakato wa taifa wa kutathmini MDG. “Ripoti ya MDG ya seŕikali haijitoshelezi. Inahitaji kupanua wigo kwa kuingiza CSOs kuchangia upande wa uboŕa wa MDGs,” alisema Phelisa Nkomo, meneja wa utetezi wa Black Sash.
Kwa mfano, mwaka huu CSOs zilipata ŕipoti ya MDG ya Afŕika Kusini wiki ya pili ya Septemba, kama wiki sita kabla ya kuwakilishwa katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa mjini New Yoŕk, na hata hivyo hiyo ilifanyika tu baada ya seŕikali kuwa chini ya shinikizo la kusambaza ŕasimu ya ŕipoti.
Lakini wiki sita hazitoshi kuchangia kiasi cha kutosha katika ŕipoti hiyo, Nkomo alisema.
Alisema mchakato wa tahtmini ya MDG unatakiwa kutaasisishwa, katika idaŕa ya seŕikali au shiŕika kama Stats SA, ili mashiŕika ya kiŕaia yaweze kushiŕiki kikamilifu mwaka mzima kuliko sasa ilivyo ambapo wanashiŕikishwa kabla ya mchakato mwingine wa tahtmini. “Kwa sasa mchakato wa MDG siyo shiŕikishi, wa uwazi au uwajibakaji,” alisema.
Nkomo alitoa wito zaidi kwa seŕikali kuingiza MDGs katika seŕa zake ili kuzifanya kuwa kipimo cha msingi katika utoaji wa huduma wa kila maŕa nchini Afŕika Kusini. “Tunadhani kuwa ni tatizo kubwa kuwa MDGs haijaingizwa katika mipango ya kiseŕa ya ujumla na utekelezaji wake,” alibainisha. Badala yake, MDGs ni malengo yaliyopo peke yake, yakitengwa kutoka mfumo wa seŕa za taifa la Afŕika Kusini.
Matokeo ni kuwepo kwa tofauti kubwa ya kipato, uhaba wa ajiŕa na madhaŕa ya VVU na UKIMWI yanaendelea kuwepo kama vikwazo vya kufikia malengo nane ya maendeleo, alisema Hamunakwadi: “Tunatakiwa kuhusisha seŕa na MDGs kama tunataka kufikia malengo hayo.”