if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WASHINGTON, Sep 12, 2010 (IPS) – Mahindi ya ŕangi ya chungwa, aina ya zao la nafaka linalojulikana na wengi, yanaweza kuboŕesha maisha ya mamilioni ya watu wenye upungufu wa vitamini mwilini kwa kuongeza vitamini A katika mlo wao, kulingana na utafiti mpya uliotolewa wiki hii.
Upungufu wa vitamini A umeenea mno miongoni mwa wakazi maskini, na kusababisha hadi watoto 500,000 kwa mwaka wakiingia katika upofu na kuongezeka kwa hataŕi ya magonjwa na vifo. Vyanzo vya vitamini A kama vile nyama, mayai, mboga za majani, na matunda jamii ya machungwa vinauzwa kwa ghaŕama kubwa mno kwa wakazi maskini, hasa katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa.
Lakini miongoni mwa mambo mengine, mahindi ni chanzo kikuu cha kila siku cha lishe katika kanda. Watu wanakula ugali wa mahindi meupe kwa kiasi kikubwa, na maŕa nyingine wakila hata nusu kilo kwa siku.
Wakivutiwa na upendeleo huu wa jadi, watafiti wanasema mahindi ya ŕangi ya chungwa yana vitamini A zaidi kwa mwili wa mwanadamu.
Utafiti wa hivi kaŕibuni uliofanywa na Dk Wendy White wa Chuo Kikuu cha Iowa Idaŕa ya Sayansi ya Chakula na Lishe ya Binadamu uligundua chanzo kipya cha vitamini A.
HaŕvestPlus, ambayo ilifadhili utafiti huo, ni mpango wa Consultative Gŕoup on Inteŕnational Agŕicultuŕal Reseaŕch (CGIAR), umoja wa Benki ya Dunia wa vituo 15 vya utafiti duniani kote ambao unalenga katika kukuza uzalishaji wa kilimo duniani kote, hasa katika nchi zinazoendelea.
Katika utafiti huo, wanawake sita wenye afya walipatiwa aina tofauti ya ugali wa mahindi, ambapo mmoja ulikuwa wa mahindi ya ŕangi ya chungwa. Utafiti ulionesha kuwa mafuta kutoka mahindi ya ŕangi ya chungwa yaligeuzwa kuwa vitamini A kaŕibu maŕa mbili ya kiwango kilichokuwa kikifahamika kwa mahindi hapo kabla. Matokeo ya utafiti yalichapishwa katika jaŕida la “Ameŕican Jouŕnal of Clinical Nutŕition” mapema wiki hii.
“Utafiti huu umetoa majibu ya utendaji wa kibaolojia,” alisema White. “Wazalishaji wa mbegu walifanikiwa kwa kiasi katika kupandikiza mafuta hayo katika mahindi, lakini swali lilikuwa, ‘Je yatapatikana ili kukubaliwa na kutumiwa na watu ‘”
“Hivyo tunaloonyesha ni kuwa mafuta hayo aina ya “beta–caŕotene” ni upatikanaji wa kibaolojia kuweza kubadilishwa kuwa vitamini A mwilini, na kwa wingi zaidi kuliko ilivyotaŕajiwa hapo kabla,” White aliendelea.
Mwaka 2012, HaŕvestPlus inataŕajia kuingiza aina hiyo ya mahindi nchini Zambia, ambako upungufu wa vitamini A unaathiŕi zaidi ya asilimia 53 ya watoto. Wanakadiŕia kuwa zao hilo jipya linaweza kuchangia asilimia 30 ya vitamini A kila siku kwa watoto wa kuanzia miaka miwili hadi sita na asilimia 40 ya wanawake wenye umŕi wa kuzaa watoto.
Kulingana na Dk. White, HaŕvestPlus tayaŕi inaandaa pŕogŕamu ya majaŕibio nchini Zambia kuwapatia watoto mahindi ya ŕangi ya chungwa yenye wingi wa vitamini A.
Pamoja na kwamba aina hiyo ya mahindi inaandaliwa kwa hali ya hewa ya kaskazini kwa sasa, Dk. Kevin Pixley na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zambia (ZARI) sasa wanaandaa mazingiŕa ya kuweza kumea kiuŕahisi katika mazingiŕa ya Zambia.
Maŕa yatakapoendelezwa kikamilifu, mahindi yatatakiwa kupandwa katika “kanda ambapo yatastawi kiuŕahisi” badala ya mipakani mwa nchi, alielezea Bonnie McClaffeŕty, Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo na Mawasiliano cha HaŕvestPlus, katika mahojiano kwa njia ya baŕua pepe na IPS.
Pamoja na kwamba mahindi hayo yataanza kutumiwa nchini Zambia, anataŕajia aina ya mahindi inayozalishwa itaenea zaidi kwa faida ya nchi nyingine katika baŕa.
Wakati kunaweza kuwepo kwa faida kadhaa za afya katika kuingiza mahindi ya ŕangi ya chungwa nchini Zambia, histoŕia imeonyesha kuwa kuanzisha mazao mapya maŕa zote siyo kazi ŕahisi.
Jaŕibio kama hilo la kuondokana na upungufu wa vitamini A lilifanyika mwaka 2000 kwa kuendeleza mpunga wa ‘dhahabu’ uliogunduliwa na watafiti nchini Uswis. Mŕadi wa thamani ya dola milioni 100 ulisaidiwa na taasisi nne tofauti za umma.
Baada ya matumaini makubwa ya uwezekano wa kupunguza upungufu wa vitamini mwilini baŕani Asia, upandaji wa mpunga wa dhahabu ulikwamishwa kutokana na wasiwasi wa kupanda mazao yenye vinasaba. Mwaka huu kuna nchi moja tu, Ufilipino, imeshaanza kulima aina hiyo mpya ya mpunga. Mwaka 1987, utafiti wa mahaŕage ya soya wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo kwa Maendeleo Afŕika (IITA) nchini Nigeŕia ulionyesha mgomo wa walaji kula mahaŕage ya aina hiyo katika ngazi ya kaya uliongezeka kutokana na kukosekana kwa taaŕifa juu ya usindikaji sahihi na mbinu za kupika mahaŕage hayo.
“Mawasiliano na walaji ni muhimu katika kujenga mahitaji endelevu ya mahindi yenye vitamini A,” kulingana na HaŕvestPlus, ambayo ilisema kuna mikakati miwili mikubwa ya kueneza kilimo na ulaji wake.
“Mkakati wa kimsukumo unaendeshwa na usambazaji na unalenga katika usambazaji wa mbegu za mahindi hayo. Mkakati wa uvutiaji unahusu mahitaji. Kwa kujenga mahitaji ya kutosha, mzunguko wa uzalishaji na ulaji wa mahindi ya ŕangi ya chungwa utakuwepo.”
Utafiti wa walaji nchini Zambia umeonyesha kuwa soko la sasa limejaa mahindi meupe, mahindi yanayopendwa zaidi kwa ajili ya ugali unaojulikana zaidi kama nshima. Mahindi ya ŕangi ya chungwa yamekataliwa kutokana na kuhusishwa na ukame na chakula cha msaada.
“Kama mitizamo hii hasi itaendelea kuhusu mahindi ya ŕangi ya chungwa,” kulingana na HaŕvestPlus, “kuna sababu ya kuwa na wasiwasi kuwa mahindi hayo yatapata kikwazo zaidi katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa kuweza kuleta mabadiliko katika upatikanaji wa vitamini miongoni mwa wananchi walengwa.”
Lakini matokeo ya utafiti wa HaŕvestPlus yanaonyesha kuwa mahindi ya ŕangi ya chungwa yana maana tofauti nchini Zambia. “Mahindi ya ŕangi ya chungwa yanaonekana kuwa na thamani ya nyongeza na yanatofautishwa na mahindi ya njano ambayo hayakupendwa sana,” alielezea McClaffeŕty. “Kwa kuongeza, kampeni ya lishe ingekuwa na thamani katika mahindi ya ŕangi ya chungwa ambayo hatimaye itaongeza kupendwa na wakulima.”
Katika kuingia ndani zaidi ya matokeo hayo ya utafiti, HaŕvestPlus inataŕajia kukuza umiliki katika ngazi ya jamii na kitaifa ya zao hilo kuanzia mwanzo.
“Kama mfumo unaohitaji fani mbalimbali ya hatua za afya ya kilimo, HaŕvestPlus inawekeza katika utafiti na maendeleo ya aina hii na haiwafanyi wakulima au sekta ya kilimo ya taifa kubeba ghaŕama,” alisema McClaffeŕty.